Tafuta

Vatican News
2020.09.24 Nembo ya Global Compact on Education (Mkakati wa elimu kimataifa) 2020.09.24 Nembo ya Global Compact on Education (Mkakati wa elimu kimataifa)  

Kwa pamoja tutazame zaidi kupitia elimu!

Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki kwa mara nyingine tena limeanza maandalizi ya mkutano wa mpango mkakati Elimu 2020(Global Compact on Education)ambao unataka kuleta mfumo mpya wa uchumi duniani.Tarehe 15 Oktoba utafanyika Mkutano kwa njia ya mtandao ukifunguliwa na ujumbe wa Papa Fracisko.

VATICAN

Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki kwa mara nyingine tena limeanza maandalizi ya mpango mkakati wa Elimu 2020(Global Compact on Education) ambao unataka kuleta mfumo mpya wa uchumi duniani.  Kutokana na hilo tarehe 15 Oktoba utafanyika Mkutano kwa njia ya mtandao kwa utanguzli wa ujumbe wa Papa Fracisko. Hata hivyo Mkutano huo, ulikuwa ufanyike Mwezi Mei 2020, kwa utashi wa Papa Francisko ili kuweza kuzalisha, kupitia elimu, na mabadiliko ya mawazo katika ngazi ya kisayari. Kutokana na janga la corona ambalo lililazimisha kufutwa kwa tukio hili hata hivyo mara kwa mara kusikika wito wa nguvu wa Papa Francisko kuwa tunahitaji kuunganisha juhudi kwa ajili ya nyumba ya pamoja ili elimu iweze kuwa muundaji wa udugu, amani na haki.

Kwa maana hiyo tarehe 15 Oktoba 2020 saa 8.30 mchana majira ya Ulaya, utafanyika mkutano kwa njia ya mtandao, na ambao uko wazi kwa wote na utakuwa moja kwa moja kupitia Youtube ya Vatican na wakati huo huo utatolewa ujumbe kwa njia ya video wa Papa Francisko, pamoja na ushuhuda na uzoefu wa kimataifa, ili kutazama upeo zaidi kwa njia ya ubunifu.

Tukio hili limeandaliwa na Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki ambalo linajumuisha shule katoliki 216,000 ambazo zinaudhuriwa na wanafunzi milioni 60 na vyuo vikuu katoliki 1.750 vyenye  wanafunzi zaidi ya milioni 11. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti hii www.educationglobalcompact.org.

24 September 2020, 16:23