Tafuta

Vatican News
COVID-19  kuchukua vipimo COVID-19 kuchukua vipimo  (ANSA)

Papa Francisko:msimsahau waathiriwa wa virusi vya corona!

Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana Papa amekumbuka mateso ya familia,madakatari,wauguzi,watawa na mapadre waathiriwa wa janga la virusi vya corona lakini hata walionusurika na tetemeko la ardhi nchini italia kunako 2016.Ushauri wa Papa ni kuharakisha ukarabati ili watu waweze kuishi kwa utulivu na amani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe Jumapili tarehe 23 Agosti 2020 amekumbuka hata tukio la tetemeko la ardhi nchini Italia ya Kati lilotokea miaka minne iliyopita yaani 2016. Amepyaisha maombi yake kwa Mungu, kwa ajili ya familia na jumuiya ambazo walipata madhara makubwa ili waweze kwenda mbele kwa mshikamano na matumaini. Ni matumaini ya Papa Francisko kuwa ukarabati unaweza kuharakishwa ili watu waweze kurudi kuishi kwa utulivu katika eneo lao zuri.

Tusisahau waathirika wa virusi vya corona

Ni katika kivuli ambacho hakipiti, virus vilivyosambatarika  ulimwenguni, adui mdogo dhidi ya idadi kubwa ya maambukizi na vifo. Kwa maana hiyo Papa anakumbusha mara baada a sala ya Malaika wa Bwana kwa karibu kuonesha  uchungu wake akirudia rudia kusema. “Na tusishahu! Tusisahau waathirika wa virusi vya corona. Leo hii asubuhi nimesikiliza ushuhuda wa familia ambao wamepoteza bibi na babu bila kuwasindikiza na kuwaaga kwa siku moja. Mateso ni mengi ya watu ambao wamepoteza maisha, waathiriwa wa ugonjwa na watu wengi wa kujitolea, madaktari, wauguzi, watawa, mapadre ambao pia wameaga maisha. Tukumbuke familia ambazo zimeteseka kwa ajili hiyo.

Tetetemo: sala kwa ajili ya matumaini

Ni jeraha la wazi, lakini kuna uchungu mbaya zaidi kwamba ikiwa wakati unaanza kupungua, kumbukumbu  kwa kawaida inarudisha uchungu huo na kuufanya uwe wazi. Hii inakumbusha wale waliokuwa wanaishi katika kilima kati ya Accumoli na Arquata ya Tronto  nchini Italia ambapo usiku wa kuamkia tarehe, 24  Agosti miaka minne iliyopita,  waliona nyumba zinakuwa magofu maisha yanakatika na kuona utupu kufuatia na tetemeko. Kwa njia hiyo mawazo ya Papa Francisko yamewaendea.

“ Kesho pia ni miaka minne tangu tetemeko la ardhi lilipotokea Italia ya kati. Ninasasisha sala zangu kwa familia na jamuiya mbazo zilipata uharibifu mkubwa, ili waweze kwenda mbele kwa mshikamano na tumaini na ninatumahi kuwa ujenzi huo utaharakisha, ili watu waweze  kuishi kwa amani katika maeneo haya mazuri ya vilima. Aidha pongezi ambayo Papa amewalekeza miongoni mwa wengine  walikokuwapo kwenye viwanja ni kwa  vijana wa Parokia ya Cernusco ya Naviglio, walitokea  Siena nchini Italia kwa baiskeli na wamefika leo Roma kupitia njia iitwayo Francigena, kwa maana hiyo amewapongeza kutoka dirishani kwa safari na kusema :“mmefanya vizuri!. Kama kawaida yake ni kumalizia akiwatakia Jumapili njema, mlo mwema na wasisahau kusali kwa ajili yake!

23 August 2020, 13:30