Tafuta

Papa Francisko amesikitishwa sana na mlipuko uliotokea huko Beirut nchini Lebanon na kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Anaungana kwa sala kuwaombea wote walioathirika. Papa Francisko amesikitishwa sana na mlipuko uliotokea huko Beirut nchini Lebanon na kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Anaungana kwa sala kuwaombea wote walioathirika. 

Papa: Mshikamano wa Huruma na Sala kwa Wananchi wa Lebanon

Hadi kufikia Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 zaidi ya watu 100 walikuwa wamekwisha kufariki dunia, watu 4, 000 wamejeruhiwa vibaya na wengine, 2500, hawana makazi maalum. Maghala ya hifadhi ya chakula kwa asilimia 85% ya chakula cha nafaka nchini Lebanon yameharibiwa vibaya sana na mlipuko huo. Habari zaidi zinasema kwamba, bandari ya Beirut imeharibiwa sana na maghala yake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 5 Agosti 2020, amezungumzia kuhusu ajali ya mlipuko mkubwa uliotokea kwenye eneo la bandari ya Beirut na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusali na kuwaombea wale wote walioguswa na kutikiswa na ajali hii mbaya. Wadau wote wa kisiasa, kijamii na kidini washirikiane na kushikamana katika kipindi hiki kigumu katika historia ya nchi yao. Kwa msaada wa Jumuiya ya Kimataifa, waweze kuvuka kipeo cha mateso na mahangaiko ambayo yatakuwa yamesababishwa na ajali hii kubwa.

Wakati huo huo, Waziri mkuu wa Lebanon Bwana Hassan Diab, amesema kwamba, mlipuko mkubwa uliotokea mjini Beirut nchini Lebanon, Jumanne tarehe 4 Agosti 2020 umesababisha madhara makubwa kwa watu na mali zao. Hadi kufikia Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 zaidi ya watu 100 walikuwa wamekwisha kufariki dunia, watu 4, 000 wamejeruhiwa vibaya na wengine, 2500, hawana makazi maalum. Maghala ya hifadhi ya chakula kwa asilimia 85% ya chakula cha nafaka nchini Lebanon yameharibiwa vibaya sana na mlipuko huo. Habari zaidi zinasema kwamba, bandari ya Beirut imeharibiwa sana na maghala yanayohifadhi dawa na vifaa tiba yameharibiwa vibaya sana, kiasi kwamba, kwa sasa Lebanon inahitaji msaada wa dharura ili kuweza kukabiliana na janga hili ambalo limejitokeza.

Waziri mkuu wa Lebanon anasema, mlipuko huo mkubwa ambao umesababisha madhara makubwa ni tani 2, 750 za madini ya “Ammonium Nitrate”, madini ambayo yanaweza kushika moto kwa haraka sana, yayonatumika kwa ajili ya kutengenezea mboleo ya viwandani pamoja na mabomu. Kwa muda wa miaka sita, yalikuwa yamehifadhiwa ghalani bila ya kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama. Idadi ya watu wanaohofiwa kupoteza maisha inawezekana kuendelea kuongezeka wakati ambapo jitihada za kuokoa watu waliofunikwa na vifusi bado zikiendelea kwa msaada kutoka ndani na nje ya Lebanon. Kukatika kwa umeme, kulisababisha kukwamisha zoezi zima la uokoaji wa watu waliokuwa wamefunikwa na vifusi.

Papa: Beirut

 

05 August 2020, 13:47