Tafuta

Vatican News
2020.08.30 Msaada wa Papa Francisko umefika katika hospitali ya Padre Orione ya Araguaína (Tocantins - Brazil Kaskazini. 2020.08.30 Msaada wa Papa Francisko umefika katika hospitali ya Padre Orione ya Araguaína (Tocantins - Brazil Kaskazini. 

Papa Francisko:Msaada mwingine wa vifaa vya kiafya kufika Brazil Kaskazini!

Vifaa vya kimatibabu vimepelekwa katika hospitali 8 za kidini katika maeneo Brazil Kaskazini na miongoni mwake ni Hospitali ya Padre Orione huko Araguaína.Huu ni msaada kwa mara nyingine kutoka kwa Papa Francisko kwa ushirikiano wa Chama cha Tumaini.Mwakilishi wa chama hicho,tarehe 23 Agosti,Dk.Taccone,amekabidhi katika Hospitali mashine 3 za kupumulia mapafu zenye uwezo mkubwa.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Mashine tatu za kupumulia zenye uwezo mkubwa na ultrasound vilivyotumwa na Papa Francisko kwa ajili ya dharura ya virusi vya corona au covid-19. Vifaa hivyo  vimepelekwa katika hospitali ya Padre  Orione huko Araguaína-Tocantins, nchini Brazil Kaskazini. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Msimamizi wa Mfuko wa Kitume, Kardinali Konrad Krajewski, amesema kuwa kwa ajili ya kuendelea kuisaidia nchi ya Brazil ili kupambana na janga la virusi vya corona, Papa Francisko kwa mara nyingine tena ametuma mashine za kupumulia 18 aina ya draeger kwa ajili ya wagonjwa katika  vyumba mahututi na ultasound 6 za mikono aina ya fuji. Ni msaada wa thamani kubwa katika wakati huu ambao pia  shukrani kwa jitihada za shirika liitwalo “Tumaini”, lisilo la kiserikali nchini Italia lenye uwezo mkuu wa kitaalam  katika  mipango ya kibinadamu na kwa ajili ya afya na elimu, kwani wanatengeneza vifaa vya kimatibabu ili kuokoa  maisha kwa njia ya  teknolojia ya hali ya juu. Na usafirishaji wake ni  kwa njia ya hisani za watu  ili kuweza viweka katika mahospitali husika.

Vifaa vya Kimatibabu vimepelekwa katika mahospitali 8 ya kidini katika maeneo nchini Brazil na miongoni mwaka ni Hospitali ya Padre Orione huko Araguaína. Tarehe 23 Agosti Dk. Paolo Taccone, alifika kutoka Milano nchini Italia  kama mwakilishi wa Shirika hilo ‘Tumaini’ na kukabidhi katika Hopitali hiyo ya watawa wa Orione, mashine tatu za kupumulia mapafu zenye uwezo mkubwa yaani za kisasa na Ultrasound ya mikono. Zawadi za haraka zimetumwa katika Jimbo la Tocantinópolis, kutokana na mazungumzo na Balozi wa kitume Giovanni D’Aniello na Askofu Giovane Pereira de Melo, wa jimbo ambaye ameelezea jinsi gani mawasiliano yamesaidia na kwamba hospitali hizo za Orione zimejengwa kwa njia ya mchakato wa wahisani.

“Ni heshima kubwa na mchango muhimu wa umoja katika mapambano dhidi ya Covid-19 na vitanda ambavyo pia vitasaidia kwenye vyumba vya mahututi vyenye  mfumo wa kiafya wa hali ya juu. vile vile vifaa hivyo vitachangia kwa kiasi kikubwa na kusaidia wagonjwa hasa walio katika hali ngumu”,  kwa mujibu wa mkurugenzi wa hospitali hiyo Padre Jarbas Assunção Serpa ambaye anatoa pia shukurani kubwa kwa msaada huo wa dhati.

30 August 2020, 11:00