Papa Francisko:Ili kuhudumia kwa furaha kazia mtazamo wa Yesu!
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Maisha ya kitawa ni suala la kuwa na mtazamo wa macho. Kuwa katikati ya watu, mtawa anaweza kuishi utume wake akiwa na mtazamo wake kwa Mungu au wa ulimwengu. Suluhisho la kutopuuzwa ni sawa sawa na la siku zote daima hasa katika kutoa kipaumbele cha sala. Ndivyo Papa Francisko anaeleza katika barua aliyotuma kwa Baraza la watawa nchini Brazil, chombo ambacho kimeandaa Wiki ya Maisha ya Kitawa katika nchi hiyo kuanzia tarehe 16 hadi 22 Agosti pia kupitia majukwaa ya kidigitali.
Wito katika furaha
Hata hivyo Papa Francisko kiukweli alianza jana, Jumapili tarehe 16 Agosti 2020 alipotamka “mbele!" kwa kuwageukia kikundi cha watawa waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro wakiwa wameshika bendera ndani ya umati mkubwa wa mahujaji na waamini. Mwakilishi katika jitihada za kufuatilia kazi hiyo kutoka Roma anaendelea kwa maelfu ya watawa na waamini wa mashirika mengi yaliyopo huko Brazili ambayo Papa Francisko amewaomba kuwa na ukweli wa maisha, akikumbuka, kwamba safari ya wito ina asili yake katika uzoefu wa kujua kuwa wamependwa na Mungu na kwamba wito ni furaha na hivyo hupatikana tu katika zawadi ya kujitoa binafsi kwa wengine.
Kuishi ili kutumikia
Kwa upande mwingine Papa Francisko anatazama mbele ya kukabiliana na changamoto zilizowekwa na jamii ya sasa, ambayo inaendelea kuleta mabadiliko ya wakati na kusema kuwa “lazima tuwe macho ili kuepusha vishawishi vya kuwa na maono ya kidunia, ambayo yanatuzuia kuona neema ya Mungu kama mhusika mkuu wa maisha na kutuongoza kwenda kutafuta mbadala wowote ule”. Udhibitisho uliobora zaidi wa kishawishi hiki anasema Papa, ni kutoa kipaumbele cha sala katikati ya shughuli zetu zote na hakika kwamba wale ambao wanakazia mtazamo wao kwa Yesu wanajifunza kuishi kwa ajili ya kutumikia.
Na moyo wa Mungu
Katika ujumbe huo Papa Francisko aidha anatoa swali la kujiuliza na ambalo ni sawa na lile alilokuwa amekwisha toa na kuwakumbusha :Nilipendekeza katika Barua ya Kitume ya mwaka wa 2014 kwa watawa, kwamba je Yesu ndiye upendo wa kwanza na wa pekee, kama tulivyopendekeza wakati tulikuwa tukitoa viapo wakati wa nadhiri zetu? “Ikiwa tutafanya hivyo tu, anahitimisha Papa, tutakuwa na uwezo kama jukumu letu, kumpenda kweli kila mtu ambaye tunakutana naye kwenye safari yetu, kwa sababu tutakuwa tumejifunza kutoka kwake ni nini maana ya upendo na jinsi ya kupenda. Tutajua jinsi ya kupenda, kwa sababu tutakuwa na moyo wake”.