Tafuta

2020.08.23 Sala ya Malaika wa Bwana 2020.08.23 Sala ya Malaika wa Bwana 

Papa Francisko:Matendo ya mshikamano yasiondoe mtazamo wa maskini na Yesu!

Yesu anawataka wafuasi wake wapige hatua madhubuti kwenye uhusiano na Yeye.Anamfunulia Simoni maana ya jina Petro yaani jiwe mahali ambapo anapenda kujenga Kanisa lake na Jumuiya yake.Ni kiini cha Tafakari ya Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana akiwaalika waamini wajiulize kama Yesu ni kitovu cha maisha na jitihada binafsi.Hata katika shughuli za mshikamano lazima kutazama mwingine sawa na mtazamo wa Yesu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Injili ya Dominika hii, kutoka (Mt16,13-20) inajiwakilisha wakati ambapo Petro anakiri imani yake kwa Yesu kuwa ni Masiha na Mwana wa Mungu. Kukiri kwa Mtume kumesababishwa na Yesu mwenyewe ambaye anatawaka wafuasi wake kuwapeleka kufanya uzoefu wa kupiga hatua madhubuti ya uhusiano na Yeye. Kiukweli katika safari ya Yesu na wale wanaomfuata hasa wale kumi na mbili ni safari ya elimu ya imani. Ndiyo tafakari ya Papa Francisko aliyoanza nayo katika Jumapili ya XXI ya liturujia ya mwaka, kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji na waamini waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican  tarehe 23 Agosti 2020.

Yesu alitambuliwa kama nabii

Papa Francisko katika kuendelea na tafakari hii anasema, awali ya yote, Yesu anawauliza “je watu hunena kuwa mwana wa Adamu ni nani?  Mitume walipenda kuzungumza juu ya watu kama ilivyo kawaida yetu sote. Maneno tunayapenda. Kuzungumzia juu ya wengine siyo kazi ngumu na ndiyo maana tunapenda; hata kama katika muktadha huu, swali lilikuwa ni kwa mtazamo wa imani na siyo kwa sababu ya masengenyoPapa amesisitiza, hivyo Yesu anaomba kujua nini watu wanasema kuhusu yeye. Na wafuasi wake utafikiri walikuwa wakifanya mashindano ya kuelezea maoni na siyo ajabu kwa kiasi fulani wao walikuwa wakishirikishana mawazo hayo hayo. Kiukweli Yesu wa Nazareti alikuwa anatambuliwa kama nabii (Mt 16,14,)

Swali la pili linafikirisha kwa kitambo na Petro anajibu

Katika swali la Pili, Papa Francisko ameongeza kusema “Yesu anawagusa kiukweli kwani anawauliza “Ninyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Kutokana na hili utafikiri waliangukia katika ukimya kwa kitambo. Kwa sababu kila mmoja aliyekuwapo alialikwa kujiuliza mwenyewe kwa kuonesha sababu ambayo inamfanya kumfuata Yesu; kwa maana hiyo ni halali kuwa na ukimya huo. Papa ameongeza kusema kwamba “Hata kama mimi naweza kuuliza Yesu kwenu ni nani? Lazima kidogo kusita”. Anayevunja kimya hicho ni Simoni mbaye alitoa uthibitisho kuwa “Wewe ndiye Kristo Mwana wa Mungu aliye hai(16).   Na kutokana na jibu lenye ujazo wa namna hiyo na mwanga, haukuwa umetokana na uwezo wake yeye binafsi hata kama alikuwa mkarimu kiasi gani, katika utamaduni kwa kile ambacho alijifunza. Hapana hakukufunuliwa.  Papa amesema na badala yake ni “tunda la neema maalum kutoka kwa Baba wa Mbinguni aliyekufunulia”. Na kiukweli Yesu mwenyewe anasema: “heri wewe Simoni wa Baliyona kwakuwa mwili na damu havikukufunulia hili bali baba yangu aliye mbinguni”( Mt 16,17). Kukiri Yesu ni neema ya Baba. Kusema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu aliye hai, ambaye ni mwakozi ni neema ambayo sisi lazima tuiombe kwamba:” Baba naomba neema ya kikiri Yesu”, Papa Francisko amebainisha.

Yesu alitambua jibu la Petro kutoka kwa Mungu

Na wakati huo huo  Bwana kwa kuwa alitambua jibu la Simoni limetokana na neema, hivyo aliongeza msisitizo mkuu  na kumwambia “Wewe ni Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda”(Mt 16, 18). Katika Uthibitisho huo Yesu anafamfanulia Simoni atambue maana ya jina jipya alilopewa “Petro”, yaani imani ambayo mara moja aliioinesha kuwa ni “jiwe lisiloanguka ambalo juu yake  Mtoto wa Mungu anataka kulijenga Kanisa lake, yaani Jumuiya yake. Na Kanisa linakwenda mbele daima kwa kufuata imani ya Petro, imani ambayo Mungu anatambua na inayotambuliwa na Yesu na kumfanya kuwa kharifa mkuu wa Kanisa.

Kila mmoja anaulizwa swali hilo hilo

Papa Francisko amesema  leo hii tuhisi kuulizwa kila mmoja wetu swali la Yesu “je ninyi mwaninena kuwa mimi ni nani? Kila mmoja wetu lazima atoe jibu na siyo la kinadharia, badala yake linahusiana na imani, yaani la maisha kwa sababu imani ni maisha! Jibu moja ambao linatakiwa hasa sisi kama walivyokuwa wafuasi wa kwanza kwa kusilikiliza kwa undani sauti ya Baba na kulinganisha na ile ya Kanisa ikiwa imeunganika kuzungukia Petro ili kuendelea kutangaza. Hii ina maana ya kutambua Yesu ni nani kwetu sisi. Ikiwa yeye ni kitovu cha maisha yetu na mwisho wa jitihada zetu katika Kanisa na katika jamii. Ni kujiuliza Yesu Kristo ni nani kwangu? Ni nani kwako?... ni jibu moja ambalo tunatakiwa kutoa kila siku, Papa Francisko amesisitiza

Shughuli za kichungaji zisiondoe mtazamo wa maskini na Yesu

Kuweni makini Papa Francisko ameonya kwani ni muhimu shughuli za kichungaji  na kijumuiya  zinafunguliwa kwa maskini wengi na dharura. Upendo daima ni njia mwalimu wa ukamilifu. Lakini Papa Francisko amebainisha kuwa ni lazima matendo ya mshikamano, matendo ya upendo tunayofanya yasiondoe mawasiliano na Bwana Yesu. Upendo wa kikristo siyo jambo rahisi tu bali kwa upande mmoja ni kutazama sehemu nyingine kwa macho sawa na Yesu na kwa upande mwingine ni kutazama Yesu katika uso wa  maskini. Na hii ndiyo njia kwanza  ya upendo kikristo, yaani ya  daima kuweka Yesu katikati. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amesema Maria Mtakatifu mwenye heri aliyeamini, awe kiongozi na mfano katika safari ya imani kwake Kristo na atusaidie kutambua kuwa imani katika Yeye inatoa maana kamili katika upendo wetu na katika maisha yetu yote.

23 August 2020, 12:17