Tafuta

Vatican News
Mama Maria wa Czestochowa nchini Poland Mama Maria wa Czestochowa nchini Poland  (Vatican Media)

Papa Francisko awakabidhi wanapoland na binadamu wote chini ya ulinzi wa Maria wa Czestochowa!

Mara baada ya Tafakari ya Papa Francisko wakati wa katekesi yake Jumatano tarehe 26 Agosti 2020, amewakabidi waamini wa Poland na ubinadamu wote chini ya ulinzi wa Mama Maria wa Czestochowa.Amekumbuka ziara yake nchini humo miaka 4 iliyopitia na kutembelea madhabahu hiyo wakati wa fursa ya Siku ya Vijana dunania na kuungana na mamia elfu ya mahujaji,familia,taifa na ubinadamu wote chini ya ulinzi wake wa kimama.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari Papa Francisko Jumatano tarehe 26 Agosti 2020 amewasalimia waamini wa mataifa kwa lugha mbali mbali kama vile Wapoland ambao Kanisa lao siku hii  linaadhimisha Siku kuu ya Mama Maria wa Czestochowa. Akikumbuka ziara yake nchini humo na kutembelea madhabahu hiyo miaka 4 iliyopita wakati wa fursa ya Siku ya Vijana dunani, ameungana na mamia elfu ya mahujaji, familia, taifa na ubinadamu wote kujikabidhi chini ya ulinzi wake wa kimama. “Salini kwa Mama Mtakatifu ili aweze kutuombea sisi na hasa wale ambao kwa namna moja au nyingine wanateseka kwa sababu ya janga la corona na kuwapatia kitulizo”, Papa amesema.

Watakatifu Monika na Agostino: tusukumwe na mfano wao kutafuta ukweli wa kiinjili

Papa Francisko  katika salam zake pia kwa wanaozungumza  lugha ya kiitaliano, amewashauri wote kuwa wakarimu katika kila mahali wanapokuwa na kushuhudia upendo wa Mungu. Hakusahau wazee, vijana, wagonjwa na wenzi wapya wa ndoa. Amewakumbusha juu ya liturujia ya kumbu kumbu ya watakatifu Monika na mwanaye Agostino kwa wiki hii, 27/28 Agosti na kwamba  “waliunganika katika nchi na vizingiti vya kifamilia na mbinguni katika hatima moja ya utukufu. Mfano wao na maombezi visukume kila mmoja kutafuta kwa dhati ukweli wa Kiinjili.”

Kwa waamini wa lugha ya kiarabu:tukitunza mali tuliyopewa na muumba ni kuhifadhi matumaini

Papa Francisko amewakumbusha waamini wa lugha ya kiarabu ya kwamba ikiwa watahifadhi mali ambazo Muumba ametoa na ikiwa wataweka kile walicho nacho kwa pamoja na kwa namna ya kwamba  hakuna anayekosa, basi hapo kweli wataweza kuelekea katika matumaini ili yazae ulimwengu wenye afya na usawa. Amewabari na kuwaombea Bwana awalinde na dhidi ya ubaya wote.

26 August 2020, 14:18