Tafuta

Vatican News
2020.08.24:Papa katika sala kwenye Picha ya Mama Maria kwa ajili ya Wagonjwa wa virusi vya corona (11.03.2020) 2020.08.24:Papa katika sala kwenye Picha ya Mama Maria kwa ajili ya Wagonjwa wa virusi vya corona (11.03.2020) 

Papa Francisko:Acha utazamwe kwa undani na Mungu maana shetani anaweka ukungu na uongo!

Katika kusali acha utazamwe ndani ya moyo wako na Mungu bila kudanganya au kutafuta sababu kwani shetani anaweka ukungu na uongo,lakini Mungu ni mwanga na ukweli.Ndiyo ushauri wa Papa Francisko alioutoa tarehe 24 Agosti 2020 katika ujumbe kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya mitandao ya kijamii JUatatu tarehe 24 Agoati 2020 anakazia juu ya kusali kwa uwazi kwamba “ni lazima kuacha utazamwe kwa ndani na Mungu bila kudanganya, bila kutoa sahamahani; kwa sababu kutoka kwa shetani anaweka ukungu na uongo na kutoka kwa  Mungu kuna mwanga na ukweli”. Hata hivyo Papa Francisko anapozungumzia juu ya kusali, anao mtazamo mpana sana na mara kadhaa amezungumzia juu ya sala  na juu ya njama za ibilisi mkubwa, mdanganyifu na mlaghai. Ni mara ngapi katika misa za asubuhi alizozifanya katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, ameweka bayana kuhusu kuwa mkweli mbele ya Mungu wetu?

Ukamilifu katika sala ni kujiweka wazi mbele ya Mungu

Kwa Mfano Papa Francisko  akitafakari juu ya Injili ambamo Kristo anawaalika wafuasi wakimbilie ukamilifu wa Bwana, yeye anakazia kuwa   ni lazima kusali kwa ajili ya watu wasio tutakia meema  yaani maadui “ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu” (Mt 5:45). Ni jambo ambao utafakiri linakwenda kinyume na mantiki ya kibinadamu, lakini ndiyo hali halisi na zaidi awali ya yote kama mkristo lazima asali kwa kujifunua wazi mbele ya muumba wake ajuaye kila kona yake ya moyo wake, ajuaye utupu wake, udhaifu wake, nguvu zake na hata matarajio na taabu.  Hii itamsaidia kuwa bora na itamfanya yule anayesali kuwa mwana wa Baba zaidi, alisisitiza Papa Francisko.

Kuombea hata maadui ndiyo ncha katika hitimisho la upendo

Papa Francisko akifafanua kuhusu sala na namna ya kuiishi sala anasema “Neno la Mungu lina mitindo ya aina mbili inyaokwenda sambamba ili kuweza kutambua zaidi na kujikita katika  matendo”. Kwa kutoa mfano anarudia maneno ya Yesu asemaye:  “mmesikia wanasema hivi, lakini mimi ninawambia hivi”... Kwa upande mmoja ni ubaridi sana na umbali uliopo hasa wa kuorodhesha mambo na uwajibikaji wa kufanya, katazo au sharti na upande mwingine kuna ushauri wa kupenda Bwana na ndugu zake kwa moyo wote hadi kufikia kusali kwa ajili ya adui ambao tunaweza kusema ndiyo ncha na hitimisho la upendo.

Ukweli, mwanga na ukungu vinajitkeza mara nyingi

Ukweli, mwanga na ukungu vinajionesha mara nyingi katika sala, kwani  hata inaonekana tangu mwanzo ambapo Yesu alipokuwa akianza shughuli ya kutangaza Neno, aliandamwa  na maadui wake waliotaka kumnyamazisha. Ukamilifu wa kikristo ambao Yesu alituelekeza vile vile  ni wenye ufunguo hasa wa kwenda kinyume na mantiki ya dunia  hii  kwa  kupenda ndugu na adui bila kutofautisha. Kwa maana hii anasema “ umesikia mchukie adui wako lakini mimi ninasema wapendeni adui zenu na kusali kwa ajili ya wale wanaowatesa”. Hiyo ndiyo njia na mwelekeo wa ukamilifu wa kikristo ulio mgumu, Papa alithibitisha.

Shetani yupo kwa sababu ya wivu wake dhidi ya mwana wa Mungu

Na mara kadhaa Papa Francisko amesisitiza kuwa shetani yupo na kwa sababu ya wivu wake kwa ajili ya Mwana wa Mungu aliyejifanya Mtu , anaendelea kupanda chuki ulimwenguni inayosababaisha vifo. Papa Francisko akitafakari juu ya Kitabu cha Hekima 2,23-3,9 anabainisha kuwa nabii anakumbusha kwamba “Mungu alituumba kwa mfano wake na sisi ni wana wa Mungu”, lakini baadaye anaongeza kusema “kwa sababu ya wivu wa shetani, kifo kiliingia ulimwenguni”. Wivu ni malaika mwenye kiburi ambaye hakukubali mwana Mungu ajifanye mtu, na umepelekea kuharibu ubinadamu. Na ndiyo maana katika mioyo yetu Papa alibainisha  paliingia mambo kama vile wivu, kiburi  husuda, majivuno na mambo mengine mengi yanayo tutengenisha na wakati ambamo tungeweza kuishi kama ndugu wote kwa amani.

Ukitaka kujua wivu wa shetani fungua Luninga

Papa Francisko kwa kuthibitisha hayo anautoa mfano na kusema  ni hali halisi ya sasa kwani ukitaka kujua inatosha  kutazama habari katika Luninga kwani unaona vita, uharibifu, watu ambao wanakufa kwenye vita  hata kwa sababu ya magonjwa.  Nyuma ya hayo yote kuna anayefanya jambo lolote alimradi mtu hasifanikiwe yaani ambaye anajulikana kama kishawishi. Ndani ya moyo kuna anayepanda uharibifu na kupanda chuki. Ni lazima kusema kwa uwazi kwamba wapo wapendaji wengi wa chuki ulimwenguni na ambayo inaharibiksa. Ni lazima kusali kwa Bwana, ili aweze kukuza ndani mwetu moyo wa imani katika Yesu Kristo mwanaye ambaye alichukua ubinadamu wetu na dambi zetu, akambambania na kushinda sheteni na ubaya. Imani hii itupatie nguvu za kutoingia katika mchezo mbaya wa wivu, uongo na wapandaji wa chuki.

24 August 2020, 13:30