Tafuta

Vatican News
Askofu George Cosmas Zumaire Lungu, wa Jimbo  Chipata na raisi wa Baraza la Maaskofu Zccb nchini Zambia Askofu George Cosmas Zumaire Lungu, wa Jimbo Chipata na raisi wa Baraza la Maaskofu Zccb nchini Zambia 

Papa atoa msaada kwa Baraza la Maaskofu Zambia kwa ajili ya watu wenye njaa na shida!

Bisheni mfatunguliwa anasema Yesu katika Injili ndivyo anavyoanza kuuandika katika barua ya Rais wa Baraza la Maaskofu chini Zambia,Askofu George Lungu na rais wa Baraza hilo kufuatia na kupokea msaada kutoka kwa Papa Francisko kiasi cha Euro 100elfu ili wawasaidie watu wenye njaa katika Nchi hiyo hivi karibuni.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Bisheni mtafunguliwa anasema Yesu katika Injili, ndivyo anavyoanza kuandika katika barua ya Rais wa Baraza la Maaskofu chini Zambia, Askofu George Lungu, akishukuru na  ambaye kwa hakika anaona uchungu kwa sababu ya hali halisi ya milioni ya wazalendo wao ambao hawana vyakula kutokana na kipeo cha vyakula ambacho pia kimetangazwa na Umoja wa Mataifa (UN) kuwa ni kipeo ambacho hakijawahi kusikika na ambacho sasa wanapaswa kupambana lakini pia hata mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Mlango umefunguliwa

Mlango ambao Askofu Lungu alibisha hivi karibuni ulikuwa ule wa Papa Francisko. Na ambaye ameufungua kwa kutoa msaada kwa Kanisa mahalia, kiasi cha jumla ya Euro 100,000 kwa ajili ya dharura za haraka kwa watu wenye matatizo magumu zaidi.

Kati ya maombi mengi yamesikika ya Kanisa la Zambia

Aliyetangaza ishara hii nzuri ya Papa Francisko kupitia ukurasa wa Facebook wa Baraza la Maaskofu ni Katibu mkuu wa Baraza hilo la Zambia, Padre Cleophas Lungu. Kwa mujibu wa kile kilichoandikwa “kati ya maombi mengi ambayo Papa Francisko amepokea, amechagua kujibu maombi ya Zambia. Fedha hizi zitagawanywa kupitia majimbo ili kuweza kuwafikia wenye kuhitaji zaidi hasa wale ambao wanaendelea kuteseka katokana na ukame na mafuriko ya hivi karibuni”.

Ukarimu wa Papa ni neema inayookoa maisha

Ili kuweza kukabiliana na madhara ya janga la maambukizi, mwishoni mwa mwezi Julai, Papa alikuwa ametoa tayari katika Nchi za Bara la Afrika kupitia ubalozi wa kitume, mashine tatu za kupumulia na maelfu ya barakoa za kimatibabu na zaidi ya vifaa vya usafi.  Ukarimu huo kwa mujibu wa Padre Lungu katika ukurasa  wa facebook amesema ni neema ambayo imeokoa maisha ya watu wengi.

17 August 2020, 13:51