Tafuta

Vatican News
Yamefanyika mazishi ya Monsinyo Georg Ratzinger kaka yake na Papa Mstaafu Yamefanyika mazishi ya Monsinyo Georg Ratzinger kaka yake na Papa Mstaafu 

Ujerumani:Salam za mwisho kwa Mons.Georg Ratzinger.Ujumbe kutoka kwa Papa mstaafu

Ibada ya mazishi ya Monsinyo Georg Ratzinger,imefanyika katika Kanisa Kuu la Regensburg,aliyefariki tarehe Mosi Julai akiwa na umri wa miaka 96.Ujumbe wa buriani kutoka kwa kaka yake Papa mstaafu umesomwa na Monsinyo Georg Gänswein wakati wa misa.Ikumbukwe Papa Mstaafu Benedikto XVI alikwenda kumwona tarehe 18 Juni kabla ya mauti yake kumfikia.

Na Sr. Angela Rwezaula,-VATICAN.

Katika barua hiyo aliyomwelekeza Askofu Rudolf Voderholzer, wa jimbo la  Ratisbona na  ambayo imesomwa na Monsinyo Georg Gänswein, Papa Mstaafu Benedikto XVI anasema katika masaa ambayo walikuwa wanatoa huduma yake ya mwisho ni kama kumpatia mwongozo kuhusu maisha yake hapa duniani, na kwamba alikuwa anajua yuko nao. “Ninapata msukumo wa kutoa neno la shukrani kwa yote mliofanya na ambayo mmefanya katika wiki hizi za buriani. Shukrani ziwandee wale wanaliomjua kimwili na wasioonekana ambao kwa wiki hizi wameonesha shukrani kwa kile amba ambacho amefanya na kuteseka kwa ajili ya maisha yake.

Marudio akilini mwake ya maisha yake na kazi yake yamejitokeza kwa njia ya kupokea barua nyingi, telegram na barua pepe  ambavyo vyote hivyo Papa Mstaafu anasema hakuwahi kufikiria. Watu kutoka Nchi nyingi, wa kijamii na kitaaluma wamemsindikiza kwa namna ambayo imemgusa moyo wake. Na kwa wote hao Papa amependelea kuwajibu kila mmoja lakini kwa bahati mbaya anasema, hana nguvu na muda wa kufanya hivyo, japokuwa kwa kutumia fursa hiyo anawashukuru kwa kumsindikiza katika masaa yote ya siku hizi. Papa Mstaafu amekumbuka sentensi ya Kardinali Newman isemayo “cor ad cor loquitur”. Kwa maana hiyo yeye ametumia karatasi ili aweze kuzungumza moja kwa moja na kila mmoja.  Kwa mujibu wa Papa Mstaafu amesema tabia za kaka yake zilikuwa za aina tatu ambazo zinawakilisha na kuangaza hata wasifu wake na hisia za muda huo aliokuwa nao akiandika barua ya buriani.

Awali ya yote amesema mara nyingi walikuwa wanasema kaka yake alipata wito wake wa kikuhani kama wito wa muziki. Na hata hivyo tayari huko Tittmoning, katika miaka ya kwanza ya maisha yake ya shule, sio tu kwamba alijifunza kwa uangalifu kuhusu muziki wa Kanisa, lakini pia alichukua hatua za kwanza kujifunza yeye mwenyewe. Huko Tittmoning au Aschau aliuliza kuhusu jina la taaluma ambayo kuhani wa Kanisa kuu alifanya kuwa muziki wa Kanisa. Katika Papa Mstaafu anaendelea kuandika kuwa fursa hiyo alijifunza jina la Domkapellmeister, ambaye kwa njia fulani aliona mwelekeo ambao maisha yake yalikuwa yanamwelekeza. Wakati alipoteuliwa kweli kuwa kiongozi wa kwaya ‘Kapellmeister’ ya Kanisa kuu la Regensburg, ilikuwa kwake furaha na uchungu ,kwa sababu ndiyo wakati “mama yetu alikuwa ameitwa kutoka ulimwengu huu na wakati huo huo kaka yake aliitwa na Domkapellmeister Schrems.

Ikiwa mama angepona, Papa Mstaafu amebainisha  labda asingekubali wito  wa  kuwa kiongozi wa Regensburger Domspatzen. Huduma hii lakini ilizidi kuwa furaha kwake, ambaye, kiukweli ilibidi kulipwa na mateso mengi. Uadui na kukataliwa havikukosekana, hasa mwanzoni. Wakati huo huo, baadaye aligeuka kuwa  baba wa vijana wengi, ambao walibaki naye na  shukrani kama Domspatzen. Papa Mstaafu ameongeza  “Shukrani zangu za moyoni pia ziende hata  kwa wote ambao kwa wakati huu wameniwezesha kupata uzoefu na kuona tena jinsi alivyokuwa mara zote mtu kuhani, kwa kuwa kuhani na mwanamuziki”.

Papa Mstaafu katika ujumbe huo anasema “Napenda pia kutaja sehemu nyingine ya kaka yangu. Kwa upande mmoja, alikuwa mtu wa kufurahisha, ucheshi wake, furaha yake kwa zawadi nzuri za uumbaji. Wakati huo huo, hata hivyo, alikuwa mtu wa kauli moja, hasa alipokuwa akionyesha waziwazi imani yake. Aliishi kwa karibu miaka 20 katika upofu, kwa  muda wote na kwa hivyo ni kama  alitengwa na sehemu nzuri ya ukweli. Sehemu hii ya kutengwa ilikuwa ngumu kwake, lakini yeye akikubali na kuishinda kwa ndani. Mwishowe lakini alikuwa  daima  mtu wa Mungu. Hata kama hakuonyesha udini wake, alikuwa na busara na uaminifu katika kitovu cha uhalisia wa maisha yake”.

Papa Mstaafu katika barua yake hatimaye anasema “ninapenda kukushukuru kwa kuniruhusu niwe nawe tena katika siku za mwisho wa maisha yako. Nilikuwa ninahisi kuwa ni wakati wa kwenda kwake kumwona tena. Ninashukuru sana kwa ishara hii ya ndani ambayo Bwana amenipatia. Wakati nilipomuaga asubuhi ya Jumatatu 22 Juni, tulijua kuwa ilikuwa ndiyo kwaheri kutoka katika ulimwengu huu milele. Lakini pia tulijua kuwa Mungu mwema, ambaye alitupatia muungano katika ulimwengu huu, pia anatawala katika ulimwengu mwingine na atatupatia muungano mpya. Asante, Giorg mpendwa, kwa yote ambayo umefanya, na ambayo  umeteseka na  yale uliyonipatia. Na asante  Askofu Rudolf mpendwa, kwa jitihada ambazo umetimiza  katika wiki hizi, ambazo hazikuwa rahisi kwa sisi sote wawili. Kwa dhati, wako Benedikto XVI. Hata hivyo  (Monsinyo. Gänswein ameonekana akitoa machozi wakati wa kumaliza kusoma ujumbe wa Papa mstaafu).

08 July 2020, 16:09