Tafuta

Vatican News
2020.06.29 Safari ya Santiago ya Compostela 2020.06.29 Safari ya Santiago ya Compostela  

Papa mshukuru kijana mlemavu katika hija ya Santiago.Ni shuhuda jasiri!

Jitihada zake zimechochewa na imani na hamu ya kujiombea mwenyewe na kwa wengine, ndiyo iliyotekelezwa na Alvaro,kijana mwenye umri wa miaka 15 kutoka Malaga nchini Uhisipania.Nguvu yake maalum ya ndani imemshangaza pia Papa Francisko na ambaye amependa kumshukuru binafsi kwa kumuandikia barua, asante kwa ujasiri wako, umetia chachu ya matumaini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kijana mmoja aitwaye Alvaro Calvente, mwenye umri wa miaka 15 asili yake ni huko Malaga, nchini Uhispania ni mwenye ulemavu wa kiakili. Licha ya ulemavu wake, siku chache zilizopita kijana huyo amefanya matembezi ya hija iitwayo “safari ya Santiago” kwa kusindikizwa na Baba yake na rafiki wa familia. Jitihada zake hizi pia zimeweza kupongezwa na Papa Francisko ambaye amwandikia Barua iliyotagazwa kwenye Tovuti ya Jimbo la Malaga.

Ujasiri wa Alvaro

Katika barua hiyo anampongeza kijana na kumshukuru kwa ushuhuda wa kijasiri. “Mpendwa Alvaro nimepokea barua kutoka kwa baba yako ambaye ameniambia mlivyomaliza kufanya zafari ya Santiago na kwamba katika mfuko wako wa safari ulipeleka nia si, tu zako binafsi, bali hata za watu wengine ambao waliungana nawe katika hisia hizi wakikuomba usali kwa ajili yao”. Ninakushukuru kwa kuwa na ujasiri na kutembea na kwa kuwaalika wengine wengi watembee na wewe.”

Ushuhuda wa sala

Papa Francisko katika baru hiyo aidha ameongeza kuandika “Katikati ya janga ambalo tunaishi, ukweli wako, furaha na urahisi wako, umewezsha  chachu ya matumaini kwa watu wengi ambao ulikutana nao katika safari yako ndefu, au kwa njia ya mitandao ya kijamii”. Papa ameendele kuandika umekwenda katika hija na kuwafanya watu wengi wawe kwenye hija huku ukiwatia moyo wasiwe na hofu au kutafuta furaha kwa sababu katika njia hatutembei kamwe peke yetu”. “Bwana anatembea daima kandoni mwetu. Asante kwa ushuhuda wako na sala zako”. Barua ya Papa inahitimishwa kwa baraka na kumwomba Mama Maria wa mlima Karmeli na wakati huo huo kutoa ombi: “Usisahau kusali kwa ajili yangu”.

Uhai katika imani

Hata hivyo safari ya Alvaro kwa hakika imeshirikishwa na baba yake kwenye Twitter, kupitia ukurasa wake wa @CaminodeAlvaro. Kijana huyo wa miaka 15 ni mtoto wa saba kati ya ndugu zake kumi ambao wanaishi wilaya ya Huelin na ni mjumbe wa Chama cha Wakatekuminali katika Parokia mahalia ya Mtakatifu Patriki. Licha ya ulemavu wake, kwa mujibu wa jimbo katoliki la Malaga, linabainisha kuwa “kijana anaudhuria kwa uhai wote shughuli za parokia na zaidi,ushuhda wake wa imani na furaha yake ni ushuhuda kwa wale wote ambao wanamfahamu”.

24 July 2020, 09:13