Tafuta

Vatican News
Argentina:mtu anayeishi akiokota mabox yuko hatari ya kuambukizwa na virusi vya corona Argentina:mtu anayeishi akiokota mabox yuko hatari ya kuambukizwa na virusi vya corona   (ANSA)

Papa Francisko kwa “Curas villeros”waliombukizwa na virusi vya corona,Argentina

Papa Francisko anaonesha ukaribu wake wa sala kwa maparoko wanaotoa huduma yao katika mitaa ya Buenos Aires,walioambukizwa na virusi vya Covid-19.Hisia hizo zimeelezwa katika ujumbe mfupi kwa njia ya video akiwaomba hata waamini wote kusali kwa ajili ya mapadre hao wa Curas villeros”, wa mitaa ya jiji kuu la nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Ukaribu wa  kuwasindikiza kwa sala  ndizo hisia za Papa Francisko alizozitoa katika ujumbe mfupi kwa njia ya video, kwa wa “Curas villeros”, yaani maparoko wa  “Villas miserias”,  wa mitaa ya watu wa mji” wa Buenos Aires, waliopata pigo la  janga la corona. Maoadre watatu kati yao wameambukizwa na virusi vya Covid-19, kwa kwa namna ya pekee Papa ujumbe wake umewaendea hao.

“Ninataka kuwambia kuwa niko karibu nanyi na kwamba ninasali kwa ajili yenu na  kuwasindikiza katika wakati huu. Ninajua ambavyo mnapambana na sala na msaada wa madaktari”. Ndivyo anasema Papa kwa njia ya  video iliyotangazwa tanagere 9 Julai 2020 kwenye ukurasa wa Mapadre hao.

Wazo la Papa Francisko linamwendea hasa Padre Basilicio Brítez, anayejulikana kwa jina  “Bachi”: kwa kumja  kama  “shujaa wa  mtaa wa Villa Palito”, leo hii  unaitwa ‘Barrio Almafuerte’, ambao ni moja ya mitaa masikini sana ya jiji, ambapo Papa Francisko amemkabidhi kwa Bwana katika wakati huu mgumu. Na hatimaye ujumbe kwa kwa wamini wote Papa Francisko amewaomba kumshukuru Mungu kwa ajili ya ushuhuda wa mapadre hao na kusali kwa ajili ya afya yao.

Kikundi  hiki cha “Curas villeros” kilizaliwa mwishoni mwa miaka ya 60 ambacho kilipata mwamko na kutiwa moyo kwenye miaka ya 90 , tangu wakati, Askofu Mkuu  wa Buenos Aires  akiwa ni Jorge Mario Bergoglio yaani Papa Francisko.

Kikundi hiki kwa sasa kina jumla ya mapadre 22 ambao wanatoa huduma yao katika mitaa 8 ya mji mkuu wa Argentina, katika maeneo yenye maelfu na maelfu ya wakazi. Miongoni mwa wale wanaojulikana sana ni Padre Josè Maria Di Paola, kwa jina  “padre Pepe”. Hata Papa Mwenyewe alimtolea mfano wakati wa kukutana na  Maparoko wa Jimbo la Roma kwenye mkutano wa  tarehe 2 Machi 2017 katika Kanisa Kuu la  Mtakatifu Yohane Laterano.

11 July 2020, 14:01