Tafuta

Vatican News
Ushemasi kijamii ni njia moja ya kutoa huduma kwa wengine Ushemasi kijamii ni njia moja ya kutoa huduma kwa wengine   (©Pixel-Shot - stock.adobe.com)

Papa Francisko:tutazame mahitaji ya wengine hatuko peke yetu duniani!

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa 600 wa kozi ya kiroho iliyoandaliwa tarehe 25 Julai kwa majimbo ya Argentina katika mkoa wa Patagonia,ikiongozwa na mada ya ushemasi kijamii” ikiwa na maana ya jinsi gani ya kutunza aliye jirani kwa mfano wa Injili ya Msamaria mwema.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuwa katika huduma ya wengine na kuzungatia wale wenye kuhitaji na kuelewa kuwa sisi hatupo peke yetu ulimwenguni, ndiyo moyo wa ujumbe alioutuma Papa Francisko tarehe 24 Julai 2020 kwa washiriki ya  Kozi ya nne ya Kiroho iliyo andaliwa na Jimbo la Comodoro ya Rivadavia, katika Mkoa wa Patagonia nchini  Argentina.

Ujumbe kwa njia ya video, umetangazwa na Kanisa mahalia kupitia YouTube.  Kozi ya mafunzo ya kiroho imefanyika kwa njia ya mtandao na ambayo imejikita katika mada ya “ uongofu wa ushamasi kijamii” nada inayoangaza na Hati ya Tume ya Kitaalimungi kimataifa ya Sinodi ya pamoja  katika maisha na utume wa Kanisa”. Katika sura ya nne ya Hati hiyo kiukweli inafafanua maana ya uongofu kwa ajili ya upyaishwaji wa  umoja. ‘Uongofu wa kishemaji  kijamii' ni jina linaloweza kutafakariwa amesema Papa katika ujumbe wake kwa njia ya video na hiyo kwamba ikiwa ina maana ya  kutambua kuwa ni lazima kuwahudumia wengine, kwa kugundua kuwa ‘mimi siyo mmoja yangu  ulimwenguni’, na kwamba lazima niangalie kile ambacho mwingine  anahitaji. , hayo yake mahitaji yake  kimwili na  mahitaji yake ya kiroho .

Kwa kuongeza amesema kwa sababu ya ubinafsi, tumezoea kupita bila kuona anayeteseka na kutazama sehemu nyingine, lakini Yesu anatuomba kuwa watumishi wa wengine kama Msamaria mwema ambaye hatujuhi jina lake, mtu haisye n ajina ambaye aliweza kumtunza aliye mkuta kalala pembeni mwa barabara. Papa Francisko amewahimiza waguswe mioyo yao na  kusisitiza kuwa  kando kando ya safari ya maisha kila wanaume na wanawake kama sisi, kuna wazee na watoto ambao wanatuomba kutazamwa  na kuwasaidiwa.

Kwa maana hiyo Papa anawatia moyo katika mchakato wa uongofu kishemasi yaani kuwa shemasi katika kuhuduma wengin , kwa sababu Yesu alisema “atakaye mpatia kikomba cha maji kwa jina langu ,hatakosa thawabu mbinguni (Mt 10, 42)”. Papa Francisko katika ujumbe huo anawatia moyo na kuwaomba wachunguze mioyo yao na kutazama kutenda mema  na mengine mengi  yatakuja kwa ziada. Ujumbe wake kwa njia ya video unafunga kwa kuwapa baraka na kuomba msaada wa Bikira Maria na vilevile wasisahau kumwombee. Katika kozi ya kiroho wameshiriki karibia wahudumu 600 wa kichungaji kwa majimbo yote.

Naye Askofu mahalia, Joaquin Gimeno Lahoz, amekumbuka kwamba  tangu mwanzo wa Papa akiwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Buenos Aires, aliendelea kuonyesha ukarimu na upendo kwa kichungaji  kwa  eneo la Patagonia, na kuonesha ukaribu wake na msaada katika Seminari ya Kipatagoniki. Na Ujumbe kwa njia ya video ni kuonesha kwa kiasi kikubwa ukaribu huo wa kuwatia moyo ili  mkoa huo usisahauliwe.

25 July 2020, 15:11