Tafuta

2020.07.08 Misa ya Papa Francisko katika kumbukizi za ziara yake huko Lampedusa 2013. 2020.07.08 Misa ya Papa Francisko katika kumbukizi za ziara yake huko Lampedusa 2013. 

Papa Fracisko:Bikira Maria atusaidie kugundua uso wa Bwana kupitia ndugu wakimbizi!

Papa katika kukumbuka miaka 7 tangu atembelea Lampedusa kunako mwaka 2013,ameadhimisha Misa takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican kwa kusisitiza juu ya kutafuta yote hayo.Utume unakwenda kwa njia ya mbili .Bikira Maria tulizo la wahamiaji atusaidie kugundua uso wa Mwanae kwa ndugu wote wanaolazimaka kukimbia ukosefu wa haki ambao unaleta migogoro ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican 

Kiitikio cha Zaburi leo hii kinatualika kutafuta mara kwa mara uso wa Bwana: “Siku zote mtafuteni uso wake Bwana. Mtakeni Bwana na nguvu zake. Utafuteni uso wake siku zote” (Zab 104). Utafutaji huu inajikita katika mtindo wa kina wa maisha ya muamini ambaye anatambua kuwa mwisho wa maisha yake yote ni kukutana na Bwana. Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Papa Francisko katika kukumbuka miaka 7 tangu atembelee Lampedusa kunako mwaka 2013. Ilikuwa ni safari yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Papa na safari hii ilikuwa ni kwa ajili ya wahamiaji ambao wanahatarisha maisha yao kwa kukatisha bahari ya Mediterranea. Ibada ya Misa imefanyika katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican, tarehe 8 Julai 2020 na kutangazwa moja kwa moja kwa njia ya vyombo vya habari Vatican na mitandao na majukwa mengine. Kutokana na tahadhari zilizopo za kuzuia maambukizi, walioudhuria Misa hiyo ni kitengo cha Wahamiaji na wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu.

Uso wa Bwana na ni nyota kuu ili tusipoteze njia

Papa Francisko akiendelea na mahubiri yake amesema, kutafuta uso wa Mungu ndiyo uhakika wa hitimisho jema la safari yetu, katika ulimwengu huu ambao ni wa mpito kuelekea katika Nchi ya ahadi ya kweli yaani  nyumbani kwetu mbinguni. Uso wa Mungu ndiyo hatma na ndiyo hasa nyota kuu ambayo inaturuhusu tusipoteze njia. Watu wa Israeli wanaolezwa na Nabii Hosea katika somo (Hos 10,1-3.7-8.12) kwa wakati ule  watu hao walikuwa wamepotea na kupoteza mtazamo wa Nchi ya ahadi na walikuwa wakienda huku na kule katika jangwa la maovu. Matarajio na utajiri mkubwa wa Bwana, kwa Waisraeli hawa walikuwa wameyatupilia mbali katika mioyo yao na walikuwa wamejijaza na uongo na ukosefu wa haki

Upyaisho wa uongofu

Papa Francisko kwa kufafanua zaidi amesema  kuwa hii ni dhambi ambayo kwayo hata sisi wakristo, wakristo wa leo, hatuko nje ya hili. “Utamaduni wa ustawi ambao unatupelekea kujifikiria binafsi, unatufanya kutohisi vilio vya wengine, unatufanya kuishi kama povu la sabuni, ambalo ni zuri, lakini siyo kitu, ni mambo yasiyo na maana, ya kitambo na ambayo utupelekea kuwa na sintofahamu kwa wengine na zaidi utupelekea katika utandawazi wa sintofahamu.” (Mahubiri ya Papa huko Lampedusa, 8 Julai 2013). Wito wa Hosea unatufikia leo hii kama upyaisho  wa mwaliko wa uongofu ili kugeuza macho yetu kwa Bwana na kuutambua uso wake. Nabii anasema “Jipandieni katika haki, nanyi mtavuna upendo; limeni mashamba yaliyo achwa maana wakati wa kunitafuta mimi Bwana umefika, nami nitawanyeshea baraka”(Hos 10,12).

Kutafuta uso wa Mungu ni kutokana na chachu ya kukutana binafsi

Utafutaji wa uso wa Mungu unatokana na chachu ya kukutana binafsi na Bwana, kwa upendo wake mkuu na nguvu yake ya wokovu. Mitume kumi na mbili wanaozungumziwa katika Injili ya siku ya leo (Mt 10,1-7) walipata neema ya kukutana naye moja kwa moja katika Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili. Yeye aliwaita kwa jina, mmoja mmoja, akiwatazama usoni; na walimtazama uso wake, walisikia sauti yake, na kuona miujiza yake. Kukutana binafsi na Bwana ni wakati wa neema na wa wokovu ambao unapelekea katika utume. Yesu aliwaagiza akisema: “katika kuenenda kwenu hubirini mkisema ufalme wa Mungu umekaribia” ( Mt 10,7).

Mkutano huo binafsi na Yesu Kristo unawezekana hata kwetu sisi, wafuasi wa milenia ya tatu. Katika kudhamiria utafutaji wa uso wa Bwana, tunaweza kumtambua kupitia uso wa maskini, wagonjwa, walioachwa peke yao na wageni ambao Mungu anatujalia katika safari yetu. Na mkutano huo unakuwa hata kwetu sisi  fursa ya neema na wokovu, kwa kujikita moja kwa moja katika utume ambao ndiyo ule ule aliowakabidhi Mitume wake, Papa Francisko amesisitiza.

Kumbukizi la ziara ya Lampedusa

Papa Francisko akiendelea katika tafakari yake amejikita juu ya kumbukizi ya mwaka wa saba tangu atembelee Lampedusa. Katika mwanga wa Neno la Mungu, ametaka kurudia aliyowaambia washiriki wa Mkutano uliokuwa na mada ya “ uhuru dhidi ya hofu” kunako mwezi Februari mwaka jana: “kukutana  na mwingine ni sawa na mkutano na Yesu,kwani Yeye  mwenyewe alisema. Ni yeye anayebisha katika milango yetu, mwenye njaa, kiu, mgeni, uchi, mgonjwa, mfungwa, akiomba ili aweze kukutana na kusaidiwa. Na ikiwa bado kuna mashaka Papa amesema tazama neno lake ni wazi “Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”( Mt 25, 40). "Kadiri yote mliyofanya….” Mema na mabaya! Onyo hilo linajionesha lenye kuchoma katika hali halisi ya leo hii. Tunatakiwa kulitumia wote kama msingi wa kujitafiti dhamiri zetu kila siku. Papa Francisko katika hili amefikiria huko Libia katika kambi ya wafungwa, wanyanyaswaji, vurugu na kutumia nguvu na kwamba  vyote hivyo vinawakumba waathirika wahamiaji ambao  wako  katika safari ya matumaini, kwa waokoaji na wale wanaowakataa. “Yote hayo mliyowatendao hao… mlinitendea mimi”.

Watu wanateseka sana Libia katika kutafuta njia ya matumaini

Papa Francisko aidha metoa ushuhuda wa kusimuliwa na mmoja  wa manusura  kuhusu  mateso wanayoyapata huko Libia. Anakumbuka aliyekuwa anatafsiri kutokana na lugha aliyokuwa anatumia. Lakini alipofika nyumbani, mchana aliweza kuambiwa na mtu kutoka Ethiopia kuwa yale aliyosimuliwa  yalikuwa ni  kidogo tu kulingana na shida nyingi wanazozipata huko Libia. Ni maelezo kidogo kulingana na masumbuko mengi katika vituo vya kufungwa wahamiaji hao. Watu hao walikuwa wanakuja kwa matumaini huku wakikatisha baharí amesisitiza Papa. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko, ameomba Bikira Maria tulizo wa wahamiaji(Solacium migrantium), atusaidie kugundua uso wa Mwanae kwa ndugu kaka na dada wanaolazimika kukimbia nchi zao kutokana na ukosefu wa haki ambao ndiyo migogoro ya ulimwengu wetu.

08 July 2020, 11:30