Tafuta

Vatican News
2020.06.07 Sala ya Malaika wa Bwana 2020.06.07 Sala ya Malaika wa Bwana  (Vatican Media)

Papa atoa wito wa kusimamisha vita duniani ili jitihada ziwe za janga

Papa Francisko baada ya Sala ya Malaika wa Bwana anatoa pongezi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao wamechukua jukumu la kusimamisha migogoro yote iliyomo ulimwenguni na kuweza kusaidia nchi zile zilizo na janga la covid-19 na ambazo tayari zilikuwa katika hali ngumu ya kibinadamu na kiafya.Maamuzi hayo yanatakiwa sasa na kwa haraka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wiki hii Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limechukua uamuzi ambao unapendekeza baadhi ya hatua za kuchukua katika harakati za kukabiliana na majanga yaliyosababishwa na virusi vya corona au covid-19, kwa namna ya pekee katika maeneo ambayo tayari yamekwisha kuwa uwanja wa migogoro. Ni jambo jema la kuomba kusimamisha vita duniani na kwa haraka ili kuruhusu amani na usalama unaohitajika kwa ajili ya kutoa huduma ya kibinadamu ambayo ni ya dharura. Ndiyo wito wa Papa Francisko alioutoa mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro tarehe 5 Julai 2020.

Papa Francisko akiendelea na  wito huo “ni matumani kuwa maamuzi hayo yaweze kuzingatiwa na kwa wakati kwa ajili ya wema wa watu wengi ambao wanateseka. Maamuzi haya ya Baraza la Usalama yanaweza kugeuka kuwa hatua ya kwanza ya ujasiri kwa ajili ya wakati ujao wa amani. Hali kadhalika amewasalima kwa moyo watu wote wa Roma na mahujaji kutoka sehemu mbali mbali. Na kwa namna ya pekee wapoland amewabariki na familia kubwa ya hija ya Radio Maria katika Madhabahu ya Częstochowa ambao wataadhimisha Jumamosi ijayo miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II kwa kuongoza na kauli mbiu “Kwa yote namkabidhi Maria”.

05 July 2020, 13:42