Tafuta

2020.06.21 Sala ya Malaika wa Bwana 2020.06.21 Sala ya Malaika wa Bwana 

Papa:Mitume wasiwe na woga maana ni moja ya adui mbaya sana wa maisha ya kikristo

Wakristo wanaoteswa ambao leo hii ni wengi zaidi kuliko wakati wa mwanzo wanawakilisha wafiadini wa nyakati zetu.Ni katika tafakari ya Papa Francisko kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana akiongozwa na Injili ya Matayo ambapo Yesu anawashauri mitume wake wasiwe na woga mbele ya changamoto za maisha na vizingiti vitakavyo jitokeza mbele yao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Injili ya Dominika ya leo kutoka Matayo 10,26-33, unasikika wito ambao Yesu anawambia mitume wake wasiogope, wawe na nguvu na imani mbele ya changamoto za maisha na kuwapa tahadhali ya misukosuko inayowasubiri. Neno la siku hii ni sehemu ya hotuba ya kimisionari ambayo Mwalimu wao anawaandaa mitume wake kabla ya kuanza uzoefu wa kutangaza ufalme wa Mungu. Yeye anawahimiza kwa nguvu zote wasiogope na kubainisha hivyo kwa hali tatu za dhati ambazo watakumbana na kukabiliana nazo. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko, Dominika tarehe 21 Juni 2020 wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican. Papa Francisko akiongozwa na Injili ya siku anafafanua hali hizo tatu kuwa,  awali ya yote ni  kukutana na kizingiti  kwa wale ambao wanataka kunyamazisha Neno la Mungu, kulitengua au kufanya wanyamazishe yule anayetaka kutangaza. Katika kesi hiyo Yesu anawatia moyo Mitume wake waeneze ujumbe wa wokovu ambao Yeye aliwakabidhi. Hadi wakati huo Yesu alikuwa ameeneza kwa uangalifu na karibu akiwa amejificha. Lakini wao watatakiwa kuutangaza  ujumbe katika mwanga, yaani kwa uwazi na kutangaza juu ya paa la nyumba ikiwa na maana kwa umma, Injili yake. Anawahimiza wasiwe na woga kwani ni moja ya adui mbaya sana wa maisha yetu  kikristo kwa maana hiyo Yesu anawashauri wasiwe na hofu.

Wapo wakristo wengi wanaoteseka ulimwenguni kuliko wafiadini wa kwanza

Tatizo la pili ambalo wamisionari wa Kristo watakutana nalo ni tishio la kimwili dhidi yao, yaani mateso ya moja kwa moja dhidi yao, hadi kufikia kuuawa. Unabii huu wa Yesu, Papa Francisko amebainisha, umetimizwa kila wakati. Ni hali halisi ya uchungu, lakini inayobainisha imani kwa mashuhuda. Ni wakristo wangapi wameteswa hadi leo hii ulimwenguni kote!  Wanateseka kwa ajili ya Injili na kwa upendo. Ni wafiadini wa nyakati zetu. Amesisitiza Papa na kuongeza kuwa “tunaweza kusema kwa uhakika kuwa hawa ni wafiadini ziaidi ya nyakati za kwanza. Ni wafiadini wengi kutokana na kuwa wakristo”. Kwa hawa, mitume wa jana na leo ambao wananapata mateso, Yesu anawashauri kuwa “msiwaogope wauuao mwili, wasioweza kuiaua na roho (Mt 10, 28). Hakuna kuogopeshwa na wale wanaotafuta kuzima nguvu ya uinjilishaji kwa maneno matupu  na kutumia nguvu, Papa Francisko amesisitiza. Hawa hawawezi katu kufanya lolote dhidi ya roho, yaani dhidi ya muungano na Mungu. Jambo hili hakuna ambaye anaweza uliondoa kwa wafuasi kwa sababu ni zawadi ya Mungu.  Hofu moja  ambayo wafuasi wanapaswa kuwa nayo ni ile ya kupoteza zawadi ya ukaribu na urafiki wa  Mungu na kuacha kuishi kwa mujibu wa Injili  na kutafuta namna hii  ya kifo maadili, ambayo ni matokeo ya dhambi.

Mitume walikabiliana na majaribu ya hisia za ndani

Aina ya tatu ya majaribu ambayo Mitume watakabiliana nayo, Yesu anaelekeza kuwa yamo ndani ya hisia hasa kwa baadhi ya wengine ambao wanaweza kuhisi ya  kwamba Mungu amewaacha na kuwa  mbali na ukimya. Papa Francisko  aanasisiza  kuwa  hata hapa Yesu anawashahuri wasiwe na woga  kwa sababu, licha ya kupitia mambo hayo, kama vizingiti vingi, maisha ya wafuasi yamo mikononi mwa Mungu ambaye anatupenda na kutulinda. Ni kama majaribu  haya matatu: kukosa kufundisha Injili na kuiondoa maana yake; pili , mateso na ya tatu, hisia kwamba Mungu ametuacha peke yetu. Yesu pia alipata jaribio kama hili katika bustani ya mizeituni na msalabani: “Baba, kwanini umeniacha?” Alisema Yesu. Wakati mwingine unahisi ukame huu wa kiroho. Hatupaswi kuogopa”. Papa Fracisko amesisitiza.

Mungu anatutunza kwani sisi ni wenye thamani machoni pake

Baba anatutunza sisi, kwa sababu thamani yetu ni kubwa mbele ya mcho yake. Hii inapelekea uwazi na ni ujasiri wa ushuhuda,  na wa imani wa Yesu mbele ya watu na kwenda mbele huku ukitenda mema,  ndiyo hali ya kuweza kutambuliwa na Yesu mbele ya Baba yake; hali ya wokovu ya maisha ya milele pamoja na Yeye mbinguni. Mama Maria mfano wa imani na kujikabidhi kwa Mungu wakati wa majaribu na hatari, atusaidie tusiangukie kamwe kukata tamaa, bali kumwamini daima Yeye ambaye neema ya Mungu daima ina nguvu zaidi ya ubaya, amehitimisha Papa Francisko.

 

22 June 2020, 08:04