Tafuta

2020.06.10 Wito wa Papa Francisko katika mapambano dhidi ya ajira za watoto wadogo. Tulinde watoto kwa maana ni kizazi endelevu cha maisha. 2020.06.10 Wito wa Papa Francisko katika mapambano dhidi ya ajira za watoto wadogo. Tulinde watoto kwa maana ni kizazi endelevu cha maisha. 

Papa Francisko:Tulinde Watoto ni kizazi endelevu cha maisha!

Papa Francisko ametoa wito wa nguvu taasisi zote kwa ajili ya watoto wengi ambao wanalazimika kufanya kazi za suruba katika umri wao mdogo.Amethibitisha katika matazamio ya Siku ya Kimataifa ya kupinga Ajira za utotoni inayoadhimishwa kila tarehe 12 Juni ya kila mwaka.Katika mkutadha huu amebainisha kuwa ni mtindo wa utumwa na sisi sote tu wahusika na lazima kulinda kizazi endelevu cha maisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni lazima kulinda watoto dhidi ya unyonyaji wa ajira za utoto. Wao ni wakati endelevu wa familia ya binadamu.Ndiyo wito uliotolewa si tu katika taaasisi mbali mbali, lakini pia kwa wote ambao Papa Francisko amewageukia kila mmoja mara baada ya tafakari ya Katekesi yake Jumatano tarehe 10 Juni 2020 kwa kutazama janga kubwa sana la unyanyasaji na unyonyaji kwa watoto katika kazi zenye suruba. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kimataifa la Watoto UNICE, libainisha kuwa karibia milini 150 za watoto kati ya miaka 5-14 wamekumbwa janga hili la ajira.  Ni tukio ambalo anasisitza Papa kuwa linazuia watoto wa kike na kiume kukua vizuri na kufurahia utoto wao ambao kutokana na kuwa hatari ya kukosa maendeleo fungamani, na kusababisha mateso ya kimwili na kiakili.

Siku ya Kimataifa ya kupinga ajira za watoto wadogo

Ijumaa tarehe 12 Juni 2020, ni Siku ya Kimataifa  ya kupinga ajira iza utotoni, iliyoanzishwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2002 kwa dhumuni la kutoa elimu na kufanya utetezi kuzuia ajira kwa watoto. Shirika la kazi kupitia Mkataba wa Kimataifa Na. 138, liliweka umri wa ajira kuwa miaka 15 na kuendelea na katika mkataba Na. 182 liliorodhesha ajira zisizokubalika kwa watoto na ambazo zinatakiwa kuzuiwa. Kwa mujibu wa Papa Francisko, amefikira hata  hali halisi ya kiafya iliyosababishwa na Janga la covid-19. Katika Nchi nyingi anasema,watoto wengi sana wanalazimika kufanya kazi zisizo stahili umei wao kwa ajili ya kusaidia familia zao katika hali ngumu ya umasikini.

“Kwa kesi kama hii ni ana ya utuma na ubaguzi  na matokeo yake ni mateso kimwili na kiakili. Sisi sote tu wahusika wa hili. Ninatoa wito kwa taaisis zoete ili waweze kuongeza jitihada za kulinda watoto wadogo, na kuzia mapengo ya uchumu na kijamii ambayo  ndiyo sababu kubwa inayosababisha hali halisi kwa bahati mbaya hii. Wtoto ni wakati endelevu wa familia ya binadamu, Sisi sote ni kazi yetu kuwasaidia makuzi , afya na utulivu”.

Sheria zipo lakini watoto wanafanyishwa kazi

Japokuwa sheria zipo wazi, lakini watoto wengi hufanyishwa kazi ngumu na zisizofaa, tena katika umri ambao hauruhusiwi kisheria na mara nyingi zadi ya muda uliowekwa kisheria. Watu wengi hawaelewi ukubwa wa madhara ya ajira kwa watoto. Sababu nyingi za ajira kwa watoto ni pamoja na umasikini, kutokuwa na uelewa juu ya madhara ya ajira kwa watoto na hali hii inaathiri zaidi watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kwani wanahitaji kufanya kazi ili waweze kukimu mahitaji yao  na familia zilizo maskini sana na wengi wao hawahudhurii shule kabisa. Watoto wanaofanyishwa kazi wanapitia changamoto nyingi ikiwemo kukosa masomo, kupitia katika ukatili wa kingono na kimwili, kunyonywa kiuchumi, matatizo ya kiafya na athari zaidi katika ukuaji wao.

Janga limekomaa barani Afrika, Asia na Amerika ya Kusini lakini pia mabara mengine

Katika maeneo mengi maskini ulimwenguni watoto wengi wanafanyishwa kazi kwa mfano Bara la Afrika chini ya jangwa la sahara, lakini pia janga hili ni katika bara la Asia, Amerika ya Kusini na visiwa vya Carribien. Licha ya hayo hata katika nchi za Bara la Ulaya hazikosi hali halisi kama hiyo. Na kati ya mitindo ya unyanyasaji inaingia hata ile ya vurugu kwa watoto hadi kufikia biashara , unyanyasaji wa kingono na mambo ambayo yanamwondelea mtoto kabisa hadhi na haki yake . Vita na majanga ya asili yanazidi kuongeza na kukatisha elimu ambayo ni msingi na haki na kama kipaumbele kwa watoto. Kwa namna hiyo, wito wa Papa unawaalika wote kwa sababu watoto hao ni wakati endelevu maisha ya ubinadamu wote.

10 June 2020, 13:42