Tafuta

Vatican News
2020.06.10 Katekesi ya Papa Francisko 2020.06.10 Katekesi ya Papa Francisko   (Vatican Media)

Papa Francisko:Utakuwepo usiku wa kukutana na Mungu ukiwa peke yako!

Katika katekesi ya Papa Francisko amendeleza mada kuhusu sala kwa kutazama sura ya Yakobo akipambana na Mungu usiku mzima na ambaye aliweza kumbadili kutoka mtu mjanja na akagundua udhaifu wake uliokumbatiwa na huruma ya Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika tafakari ya Papa Francisko Jumatano tarehe 10 Juni 2020, kama kawaida yakatekesi yake akiwa katika maktaba ya Kitume mjini Vatican, ameendeleza mada kuhusu sala, kwa kuongozwa na somo kutoka kitabu cha Mwanzo 32,25-30 ambayo ni kifungo cha sehemu ya historia ya Yakobo na Esau watoto wa Isaka. Papa Francisko akianza tafakari amesema “Tuendelee na katekesi yetu kuhusu mada ya sala. Katika kitabu cha Mwanzo, kwa njia ya matukio ya wanawake na wanaume wa nyakati mbali zinasimulia historia ambayo tunaweza kuiangazia maisha yetu”. Kwa kufafanua zaidi amesema katika mzunguko wa mababa, tunakutana hata na mwanaume ambaye alikuwa ametengeneza kwa ujanja talanta bora zaidi, yaani Yakobo. Biblia inasimulia kuhusu uhusiano mgumu wa Yakobo aliokuwa nao na kaka yake Esau, hawawalikuwa  ni mapacha . Tangu wakiwa wadogo, kati yao kulikuwa na mashindano na wala baadaye hayakumalizika. Yakobo alikuwa ni mtoto wa pili, lakini kwa ujanja aliweza kuiba baraka kwa baba yake Isaka na iliyokuwa ni zawadi ya kifungua mimba (Mw 25,19-34). Ni baada tu ya mfululizo wa ujanja wa mwanaume  huyo ambaye anasadikiwa kuwa mwenye uwezo. Hata kwa jina la Yakobo maana yake ni yule anaye jishughulisha lakini siyo moja kwa moja, maana yake ni kujishughulisha kwa ujanja.

Yakobo alitajirika kwa ujanja na kupata kile alichotamani

Papa Francisko akiendelea kufafanua juu ya historia ya Yakobo anasema, kwa kulazimika kukimbia kwenda mbali na kaka yake, katika maisha yake aliweza kufanikiwa kila jambo. Alikuwa ni mwenye uwezo wa kibiashara, akajitajirisha sana na kuwa na zizi kubwa la wanyama. Kwa uvumilivu mkubwa aliweza kuoa binti mzuri sana wa Labani ambaye alikuwa amempenda sana. Yakobo, kwa maana nyingine Papa anabainisha “unaweza kusema kwa lugha ya kisasa alikuwa mwanaume ambaye amejitengeneza mwenyewe, kwa ujanja wake aliweza kupata kila kitu alichokitamani. Lakini alikuwa anakosa kitu. Alikuwa anakosa uhusiano ulio hai na mizizi yake mwenyewe. Siku moja akasikia kuitwa nyumbani mahali alipozaliwa zamani, mahali ambapo alikuwa bado anaishi Esau, kaka yake ambaye walikuwa wamevunja  uhusiano wao kwa sababu alikuwa amemwibia baraka yake.  Yakobo alianza safari ndefu akiwa na msafara wa idadi kubwa ya watu na wanyama, hadi kufikia hatua ya mwisho katika kijito cha Jabbok. Hapo katika kitabu cha Mwanzo kinatoa sura za kukumbuka sana( 32,23-33). Kinasimulia kuwa Patriaki baada ya kukatisha kijito na watu wake wote na wanyama alibaki yeye peke yake kwenye mwambao wa kigeni.

Maswali ya Yakobo juu ya kukutana na nduguye na mapambano na Mungu

Na kufikiria je ni kitu gani kinamsubiri kesho yake? Ninamna gani ataweza kukutana na kaka yake Esau? Akajazwa na mawazo akilini mwake bila kutoka… Na wakati ulipoingia giza, kwa haraka akasikia anavutwa mguu na hasiyejulikana na kuanza kupambana naye. Katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki  inafundisha kuwa “Mapokeo ya kiroho ya Kanisa yalitazama historia  hii kama ishala ya maombi katika mapambano ya imani na ushindi  wa kuvumilia (KKK,2573). Papa Francisko amesema Yakobo alipambana usiku mzima bila kumwachia ushindi mpinzani wake. Hatimaye akashindwa lakini kwa kuachwa amevunjwa paja la mguu wake na tangu hapo atachechemea maisha yake yote. “Hutaitwa tena Yakobo, Papa akaongeza,  hutakuwa mwanaume ambaye anatembea hivi hivi  moja kwa moja. Akambadili jina, akambadili maisha, akambadili tabia na kamwaita Israeli, “ maana umeshindana na, Mungu, na watu, nawe umeshinda. (Mw 32,28)”. Kwa maana hiyo Yakobo akamwuliza “ Niambie, tafadhali, jina lako? Naye akamwambia na  baadaye akambariki. Na  Yakobo akajitambua ya kwamba amekutana uso kwa uso na Mungu( 32,30-31).

Kupambana na Mungu

Kupambana na mungu ni mfano wa sala. Mara nyingi Yakobo alikuwa amejionesha mwenye uwezo wa kuzungumza na Mungu, wa kuhisi kama uwepo wa rafiki na ukaribu. Lakini usiku ule aliupitia katika mapambano ambayo yaliendelea muda mrefu na ambayo karibu alikuwa anaona anamezwa, Patriaki huyo aliondokana akiwa amebadilika. Alipambana lakini wakati huo akiwa na hofu.  Kwa mara hii yeye siyo bwana wa hali halisi, siyo mwanaume tena mwenye kuwa na  mikakati na kuhesabu; Mungu anampeleka katika hali yake ya ukweli wa kifo ambacho kinatetemesha na kuwa na hofu. Kwa mara nyingine Yakobo hana zaidi ya kuwakilisha Mungu udhaifu wake na kutoweza kwake. Na ndiyo maana Yakobo alipokea kutoka kwa Mungu baraka, ambayo anaingia katika nchi ya ahadi akiwa anachechemea, mwathirika, na aliye athiriwa, lakini na moyo mpya.  Papa Francisko ameongeza kusema “Siku moja nilisikia mtu mzee , na mwema, mkristo mwema , lakini  mdhambi! ambaye alikuwa anaimani kubwa kwa Mungu , Na yeye akikuwa anasema “Mungu atanisaidia; hatanicha peke yangu. Nitaingia mbinguni nikiwa nachechemea, lakini nitaingia”. Yakobo mwanzo alikuwa anajiamini, na kuamini ujanja wake, lakini kiukweli alikuwa na hofu. Alikuwa ni mtu asiyewezekana kupata neema, na kinzani kwa huruma. Lakini Mungu akamwokoa alichokuwa amepoteza. Kwa kuhitimsha Papa Francisko amesema kila mtu katika maisha anao muda wake wa usiku na kipindi cha giza nene, kipindi cha dhambi na wakati wa kukosa mwelekeo… pale kuna wakati na Mungu daima.

Mungu anakutana na sisi mahali tusipotarajia

Mungu anatuangazia katika wakati ule ambao sisi hatutarajii, amesisitiza Papa Francisko na kwamba ni mahali ambao atatukuta tukiwa kweli peke yetu! Katika usiku ule, wa kupambana na asiyejulikana, tutakuwa na dhamiri ya kuwa kweli watu maskini. Lakini wakati huo huo ndiyo hatutapaswa kuogopa, kwa kuwa katika wakati huo Mungu anatuuliza kwa upya majina yetu, ambayo ndani mwake yana maana ya maisha yetu; Yeye atatupatia baraka yake aliyoiweka kwa yule ambaye anaacha abadilishwe naye. Huo ndiyo mwaliko wa kujiachia ubadilishwe na Mungu, Yeye anajua kufanya, kwa sababu anajua kila mmoja wetu, “Ee Bwana wewe wanijua” na kila mmoja anaweza kusema: “Ee Bwana, wewe wanijua mimi, nibadili!" Amehitimisha Papa Francisko tafakari yake.

10 June 2020, 13:16