Tafuta

2020.06.24 katekesi ya Papa Francisko 2020.06.24 katekesi ya Papa Francisko 

Papa Francisko:Daudi anatufundisha kuingia mazungumzo na Mungu!

Sala ina uwezo wa kuhakikisha kuwa na uhusiano na Mungu ambayo ni msindikizaji wa kweli wa safari ya mtu katikati ya mambo mengi ya maisha mema au mabaya.Daudi anatufundisha kuingia katika mazungumzo na Mungu kwa kila lolote.Furaha kama makosa,upendo kama mateso,uadui kama ugonjwa,yote hayo yanageuka kuwa neno ambalo tunaweza kusema wewe unasikiliza.Ni katika tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko akikita kutazama sura ya Daudi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mwendelezo wetu wa  katekesi kuhusu sala leo hii tunakutana na Daudi. Aliyependezwa na Mungu tangu akiwa kijana kwa kuchaguliwa katika utume wa kipee ambao unahusika katika jukumu msingi la  historia ya watu wa Mungu na imani yetu yenyewe. Katika Injili Yesu ameitwa mara nyingi “mwana wa Daudi”; kwa hakika kama yeye alivyo, alizaliwa Bethlehemu. Tangu uzao wa Daudi kwa mujibu wa ahadi alikuja Masiha. Ni mfalme kwa ujumla ambaye kwa mujibu wa moyo wa Mungu, ni mkamilifu wa utii wa Baba na  ambaye matendo yake yanatimizwa kwa uaminifu wa mpango wake wa wokovu(KKK 2579). Ni mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko Jumatano tarehe 24 Juni 2020 akiwa katika Maktaba ya Kitume mjini Vatican. Papa Francisko akiendelea amesema  Sala la Daudi ilianzia kwenye vilima karibia na Bethlehemu, mahali ambapo yeye alikuwa akichunga zizi la baba yake Yese. Alikuwa ni kijana mdogo wa mwisho kati ya ndugu zake.  Hadi kufikia kwamba Nabii Samueli kwa maagizo ya Mungu alianza kutafuta mfalme mwingine na utafikiri kwamba baba yake alikuwa amesahau yule mtoto aliye kuwa kijana zaidi (1Sam 16,1-13). Alikuwa anafanya kazi mahali palipo wazi.  Tunamfikiria kama rafiki wa upepo, mvumo wa asili na mionzi ya jua. Alikuwa na msindikizaji wake wa kusaidia roho yake, yaani kinubi. Na kwa siku nzima ya upweke alikuwa anapenda kupiga kinubi na kuimba kwa Mungu wake pia alikuwa anacheza na manati.

Daudi ni mchungaji analinda dhidi ya hatari

Daudi awali ya yote ni mchungaji, Mtu ambaye anawatunza wanyama na anawalinda wasifikiwe na hatari na kuwatafutia malisho yao. Wakati Daudi alikuwa aanze kushughulikia watu kwa mujibu wa Mungu, hakutenda kinyume na hayo. Na ndiyo maana katika Biblia picha ya mchungaji inajitokeza mara nyingi. Hata Yesu anajifanya kuwa “mchungaji mwema, matendo yake ni tofauti na yale ya mfanyakazi; Yeye anatoa maisha yake kwa ajili ya kondoo wake, anawaongoza, anajua majina ya kila mmoja wao (taz Yh 10,11-18). Katika kazi yake ya kwanza, Daudi alijifunza sana. Kwa namna hiyo Nabii Natana alipomjulisha kuhusu dhambi yake kubwa (2Sam 12,1-15) Daudi alitambua kwa haraka sana kwamba yeye amekuwa mchungaji mbaya, aliyerarua mtu mwingine pekee kama kondoo ambaye yeye alikuwa anampenda na hakuwa tena mtumishi mnyenyekevu, bali mgonjwa wa madaraka, mjangili anayeua na kupora.

Roho ya Daudi kama mtunzi na nyimbo za sifa kwa Mungu

Sehemu ya pili ambayo inajiwakilisha katika wito wa Daudi ni roho yake ya utunzi. Kwa kufafanua zaidi juu ya kile kilichotokea, Daudi hakuwa mtu mchafu, kama vile mara nyingi inawezekana kuona mtu analazimika kuishi kwa muda akiwa pweke katika jamii. Kinyume chake alikuwa ni mtu makini, ambaye alipenda muziki na nyimbo. Kinubi chake kilimsindikiza daima. Wakati mwingine aliinua nyimbo zake kwa Mungu za furaha (2 Sa 6,16) na wakati mwingine alijieleza kwa kulalamika au kuungama dhambi zake mwenyewe (zab 51, 3). Ulimwengu ambao unajiwakilisha machoni pake siyo tamasha la kimya. Mtazamo wake unatambua nyuma yake ya kufunua mambo ya fumbo kubwa. Sala inazaliwa kwa dhati hapo kutokana na kuamini kwamba maisha siyo jambo ambalo linatelezea nyuma, bali ni fumbo la kushangaza, ambalo kwetu sisi linawakilisha shairi, muziki, shukrani, sifa, au kulalamika na kuomba. Ikiwa mtu anakosa ile sehemu ya kishairi, Papa Francisko ameongeza kusema roho huumia”. Utamaduni kwa maana hiyo unataka kwamba Daudi awe kiongozi mkuu wa utunzi wa zaburi. Zaburi hizi mara nyingi mwanzo zinaelekeza kwa Mfalme wa Israeli na badhi katika matukio mengine zaidi au ambayo siyo mema katika maisha yake.

Ndoto ya Daudi kuwa mchungaji mwema

Daudi kwa maana hiyo anayo ndoto, ya kuwa mchungaji mwema. Mara nyingine aliweza kufikiria hali ya juu ya kazi hiyo na mara nyingine hakuweza, lakini kile chenye maana, katika muktadha wa historia ya wokovu ni ile ya kuwa nabii wa mfalme mwingine, ambapo yeye ni mtangazaji na mfananisho tu. Tutazame Daudi, tufikirie Daudi. Mtakatifu na mdhambi, mtesi na mteswaji, mwathirika na mnyongaji. Ni utata! Lakini Daudi alichukua nafasi zote hizo! Hata sisi tunajirekodi katika maisha yetu ambayo mara nyingi yana utata. Katika kuishi kwetu, watu wote wanatenda dhambi mara nyingi bila kukubaliana nayo. Papa Francisko amerudia kukazia  Daudi mtakatifu, anasali; Daudi mdhambi anasali; Daudi ameteswa, anasali; Daudi anatesa, anasali; Daudi ni mwathirika, anasali. Hata Daudi ni myongaji, anasali. Kuna mstari mmoja mwekundu, katika maisha yake yote Daudi ambaye anatoa umoja wa kile ambacho kinatendeka, katika sala yake. Mwanaume anayesali. Ile ni sauti ambayo haizimiki kamwe. Na ambayo inachukua sauti ya furaha kubwa au ya kulalamika daima ni sala, japokuwa sauti zinabadilika tu. Na kwa kufanya hivyo Daudi anatufundisha kuingia katika mazungumzo na Mungu kwa kila lolote. Furaha kama makosa, upendo kama mateso, uadui kama ugonjwa, yote hayo yanageuka kuwa neno ambalo tunaweza kusema “Wewe” ambaye unasikiliza, Papa Francisko amesisitiza.

Sala ni nguvu kwa wale wanaotoa nafsi yao

Daudi ambaye alijua upweke, lakini hali halisi haikuwa hivyo kamwe!  Papa Francisko amefafanua kuwa, sala kwa kina ni nguvu kwa wale wote ambao wanatoa nafasi yao katika maisha yao kujikita ndani mwake. Maombi yanakupa heshima na Daudi ni mwenye kuheshimika kwa sababu alisali. Lakini yeye alikuwa ni mnyongaji anayeomba, na kutubu na heshima ikarudi kutokana na maombi. Aidha sala ina uwezo wa kuhakikisha kuwa na uhusiano na Mungu ambayo ni msindikizaji wa kweli wa safari ya mtu katikati ya mambo mengi ya maisha mema au mabaya. Lakini daima ni sala na shukrani kwa Bwana. Bwana ninaogopa. Bwana nisaidie. Bwana nisamehe. Imani ya Daudi ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba wakati alipoteswa na ilimbidi kukimbia, hakumruhusu mtu yeyote kumtetea. “Ikiwa Mungu wangu ananinyenyekeza hivi, anajua”, kwa sababu ukuu wa sala unatuacha mikononi mwa Mungu.  Katika mikono ile iliyojaa majeraha ya upendo na mikono pekee ya usalama tuliyo nayo, amehitimisha Papa Francisko. 

24 June 2020, 13:44