Tafuta

Vatican News
Msaada wa Mashine za kupumulia kwa wagonjwa wa Covid-19 bado unahitajika katika maeneo mengi ulimwenguni Msaada wa Mashine za kupumulia kwa wagonjwa wa Covid-19 bado unahitajika katika maeneo mengi ulimwenguni  (ANSA)

Papa Francisko atoa mashine 35 za kupumulia katika dharura ya Covid-19!

Kuanzia Amerika ya Kusini kwenda Asia,kupitia Afrika hadi Ulaya ukaribu wa Papa Francisko usiochoka unazidi kuvuka mipaka yote kupitia kazi ya Sadaka ya Kitume ambayo inafikia kila kona ya ulimwengu hasa katika sehemu zenye mifumo ya shida kiafya katika wakati huu wa janga la corona.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mashine za kupumulia ambazo zimefika katika Nchi nyingi za Ulimwengu  wenye shida kubwa hasa zilizo na pigo kali la janga la virusi,vile vile maeneo yenye mgogoro wa mfumo wa kiafya, zinawakilisha kwa namna fulani ukaribu wa dhati na upendo wa ubaba wa Papa. Kwa kupitia Sadaka ya Kitume, taarifa imebainisha kuwa katika wiki za mwisho kupitia Ubalozi mbali mbali  wa kitume,  Papa Francisko amekwisha tuma mashine 35 za kupumulia.  Hizi ni mashine za kusaidia  hewa muhimu  ya mapafu katika kuokoa maisha ya wagonjwa walio hatarini zaidi kwa sababu ya  Covid- 19. Katika miezi ya hivi karibuni tumesikia  kuzungumza mara kwa mara, kila mahali juu yake kwa sababu idadi ya wale ambao wangehitaji imekuwa, hitaji kubwa kuliko upatikanaji wa hizi mashine ambazo kimsingi, kupitia uingizaji hewa ya mitambo, husaidia wagonjwa walio na shida ya kupumua moja ya dalili mbaya zaidi ya virusi vya corona

Amerika na  Afrika

Katika orodha iliyotolewa na Ofisi ya Sadaka ya Kitume kuanzia Bara la Amerika, Afrika hadi Ulaya na Asia,  Mashine 4 zimetumwa huko Haiti na “Jamhuri ya watu wa Dominica. Nyingine mashine nchini Bolivia na wakati mashinda 4 zimefika nchini Brazil, ambapo Papa Francisko anaendelea kuwahakikisha sala zake na zaidi pia kwa kuwapigia simu maaskofu na kuwakabidhi kwa Mama Maria wa Aparecida. Nchini Brazil ni mahali ambapo kwa sasa inajulikana kuwa kitovu cha virusi hadi kufikia waathiri 55,000 na zaidi ya milioni moja ya kesi zilizothibitishwa, vile vile hali mbaya na takwimu zimejionesha baada ya Marekani mahali ambapo wanahesabu karibia milioni 2  na nusu ya maambukizi na vifo 124,000. Tukibaki katika Bara la Amerika ya Kusini, Mashine nyingie tatu za kupumulia zilizotolewa na Papa Francisko zimefika nchini Colombia na 2 nchini Equador mahali ambapo maambukizi ni watu 4300. Mashine hizo, nchini Equadoro zimekabidhiwa kwa Waziri wa  Afya kwa mujibu wa Balozi wa kitume nchini humo, askofu Mkuu Andrés Carrascosa Coso, ambaye anasema kuwa hiyo ni ishara ya mafuta kwa watu.

Ulaya na Asia

Mashinde nyingine 3 zilifika huko Honduras, na  Mexico na 4 nchini  Venezuela,  mahali ambapo mgogoro wa kiafya umeunganishwa na hali ngumu sana ya kijamii na kiuchumi. Bado upendo wa Papa umezidi kuvuka mipaka hata ukaribu barani Afrika katika nchi ya Camerun na Zimbabwe kwa kutuma maishine 4. Barani Asia mashine 2 zimepelekwa nchini Bangladesh na pia kwa upande wa Ulaya, mashine 2 nchini Ukraine kwani  waathirika hadi leo ni zaidi ya watu 1000.

27 June 2020, 09:04