Tafuta

Vatican News
2020.06.24 Zawadi ya Papa ya baiskeli kwa  Unitalsi 2020.06.24 Zawadi ya Papa ya baiskeli kwa Unitalsi  

Papa atoa zawadi ya Baiskeli ya umeme kwa Chama cha Unitalsi

Papa Francisko ametoa zawadi ya baiskeli ya umeme kwa chama cha Unitalsi kwa ajili ya mnada wa kufadhili wa watoto katika hospitali ya Policlinico Gemelli,Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika ya harakati nyingi za kuhamasisha msaada wa kibinadamu kwa watu wenye matatizo ya kiafya kuna hata baiskeli ya umeme ya kisasa ambayo Papa Francisko ametoa zawadi kati ya vitu ambavyo ni vya kuweka kwenye mnada kwa ajili ya ufadhili  ulioandaliwa na kitengo cha Chama cha kusadia wagojwa katika hija mbali mbali za kitaifa na kimataifa kwa chama cha  UNITALSI cha Roma mkoani Lazio nchini  Italia. Taarifa zimetolewa na Chombo cha hisani  kimethibtisha  kuwa fedha zitakazopatikana zitasaidia kupelekea hija ya Lourdes watoto wagonjwa  wa Hospitali ya Gemelli Roma.

“Baba Mtakatifu daima yuko karibu na watoto”, kwa mujibu wa Preziosa Terrinoni, Rais wa Unitalsi kitengo cha Wilaya ya Roma Mkoani Lazio , Italia. Aidha kiongozi huyo amekumbuka juu mkutano wao wa faragha kunako tarehe 31 Mei 2013 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican kati ya Papa Francisko  na watoto 22  wagonjwa waliokuwa wanapata matibabu yao katika Hospitali ya Policlinico Gemelli, Roma.

Aliyewakilisha ufadhili huo ni Katibu maalum wa Papa, Monsinyo Yoannis Lahzi Gaid, ambaye amewakabidhi wahusika wa kitengo hicho, kwa ishara kubwa ya upendo kwa upande wa Baba Mtakatifu, na ambaye kwa miaka hii ya utume wake kama Papa ameweza kuonesha kwa namna nyingi ukaribu na chama hiki cha Unitalsi.  Hata hivyo, shughuli mbali mbali za hisani zinaweza hata kufanyiwa kupitia mtandaoni kwa kutembelea tovuti ya UNitalisi www.unitalsiromanalaziale.it Ambayo imeundwa kwa ajili ya zoezi hilo.

24 June 2020, 14:03