Tafuta

2020.06.22 Papa atoa msaada katika mji wa Baixada nchini Brazil 2020.06.22 Papa atoa msaada katika mji wa Baixada nchini Brazil 

Mshikamano wa Papa kwa maskini wa Baixada Fluminense,Brazil

Katika serikali ya Rio de Janeiro,Kaskazini Mashariki ya Brazil ni eneo lenye watu wengi sana nchini humo ambapo janga la corona limeenea kwa kasi sana.Askofu Gilson Andrade ametoa shukrani kubwa kwa Papa Francisko kwa msaada wake alioutuma katika kipindi hiki kinachohitaji mshikamano wa safari ya matumaini kwa watu hao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Mkoa wa Baixada Fluminense nchini Brazil una historia ya umaskini, wa kutumia nguvu, watu kuachwa peke yao na zaidi katika kipindi hiki cha janga la kiafya eneo hilo limekuwa na pigo kubwa la covid-19 na ambapo Papa Francisko kati ya mshikamano anayoendelea kuitoa, pia msaada wake umeweza kuwafikia watu hao. Hata hivyo katika taarifa ya Kanisa hilo linabanisha kwamba licha ya jimbo la Nova Iguaçu kulazimika kufunga shughuli zake za kichungaji, kama vile maadhimisho ya misa kwa waamini na shughuli nyingine za kitume  lakini limeweza kuongeza jitihada zaidi hasa katika mipango ya kijamii ya Caritas jimbo, katika kituo kwa ajili ya haki za binadamu, matendo ya upendo  kijamii mingine ya maparokia ya waamini. Kadhalika imeongeza jitihada zake katika utume wa kutoa msaada ili kuweza kujibu ongezeko la maombi ya msaada kutokana na familia nyingi zinazohitaji.

Katika kuongeza nguvu zaidi ya mipango hiyo, jimbo hilo  hivi karibuni kwa njia ya Balozi wa kitume wamepokea kiasi cha 10,000 fedha za nchini humo kutoka kwa Papa Francisko. Msaada huu muhimu umetumiwa wote kwa ajili ya kununua vyakula na vifaa vya kujikinga ambavyo vimesambazwa kwa familia nyingi katika mitaa yenye kuhitaji zaidi ya Rio de Janeiro. Kwa mujibu wa Askofu wa Nova Iguaçu, Askofu Gilson Andrade, ameelezea shukrani nyingi kwa Papa Francisko kuwa kwa hakika wakati huu wa mshikamano ni matumaini ya safari kwa ajili ya watu wengi,  hivyo wanahisi kuwa na furaha kubwa ya kuweza kutegemea msaada wake.

Aidha Askofu amesisitiza kuwa Yeye ni mchungaji ambaye ameamsha ulimwengu na ili hasiwepo yoyote anayekuwa na sintofahamu za mateso ya wengine. Kanisa liko karibu na watu, si tu  wale wa mbali ,  pia  wa karibu ili kushirikishana na maisha yao ya dhati. Askofu pia amesema kuwa makuhani wanazidi kusisitizia juu ya utambuzi wa ndugu kaka  na dada walioko kwenye matatizo.  Baba Mtakatifu amenyosha mkono wake na upendo huo umeleta furaha  na matumaini kwa watu ambao wamekuwa wametengwa katika msaada. Kadhalika amesisitiza ni jinsi gani wanahisi kuwa na nguvu ya muungano na shukrani kubwa kwa Baba Mtakatifu. Upendo wake kwa ajili yao ni kuwatia moyo ili waweza kupata namna ya kutunza watu katika kipindi hiki kisicho na usalama  na chenye mateso.

24 June 2020, 14:53