Tafuta

Vatican News
2020 06 25 Ecuador: mashine zilizotumwa na Papa nchini Equador, Balozi wa Kitume  Askofu Mkuu Carrascosa amezikabidhi waziri wa Afya 2020 06 25 Ecuador: mashine zilizotumwa na Papa nchini Equador, Balozi wa Kitume Askofu Mkuu Carrascosa amezikabidhi waziri wa Afya  

Kukabidhi msaada wa mashine za kupumulia nchini Equador

Msaada wa mashine mbili uliofika mwanzoni mwa wiki umepelekwa katika Hospitali ya Eugenio Espejo ya Quito nchini Equador ambapo Balozi wa kitume alimkabidhi Waziri wa Afya. Ishara ya Papa Francisko bado inaendelea kuwa kama mafuta kwa watu,kwa mujibu wa Askofu Mkuu Andrés Carrascosa Coso katika mahojiano na Vatican News.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Balozi wa Kitume wa Quito, nchini Equador Askofu Mkuu Andrés Carrascosa Coso, amejaribu kutafakari ishara za Papa Francisko ambaye ametoa zawadi ya mashine mbili za kupumulia nchini humo, katika harakati ya kupambana na virusi vya covid- 19 ambavyo katika nchi hii ya Amerika ya Kusini tayari kesi zaidi 53,000 zimerekodiwa na zaidi ya vifo 4.300. Kwa mujibu wake anasema:” Ni ishara ambayo inatafuta kufungua macho kwa wote ili wawe makini katika mahitaji ya mwingine anayeinua mikono yake kuomba msaada”.

Mashine hizo mbili zimefika wiki hii na kukabidhiwa  kwa  mamlaka ya hospitali  ya Eugenio Espejo huko Quito. Na hizi mashine zilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya nchini humo Bwana Juan Carlos Zevallos, na Askofu Mkuu mwenyewe Carrascosa Coso ambaye amesimulia ishara hiyo katika mahojiano na Vatican News, na kwamba katika dharura hii ya Covid-19 eneo la Guayaquil, mji mkuu wa wilaya ya Guayas juu ya Bahari ya Pasifiki na hata Quito zimekuwa kitovu cha maambukizi makali ya corona.

Jumatatu jioni tarehe 22 Juni 2020 mashine hizo zilifika, wakati Askofu Mkuu alikuwa tayari amekwisha zungumza na Waziri wa Afya wa nchi, Juan Carlos Zevallos, ili kujua ni mahali gani mashine hizo zinahitajika zaidi. Alikuwa amemweleza sehemu ya Quito katika hospitali ya Eugenio Espejo ya mji mkuu, ambacho ni kituo kikuu zaidi cha watu wote katika nchi hiyo. Jumatano, tarehe 24 Juni 2020 waliweza kukabidhi mashine hizo kwa waziri wa Afya, akiambatana na Makamu Waziri wa Mambo ya Nchi za nje, Cristian Espinosa, na Mkurugenzi wa Hospitali yenyewe Mercedes Almagro. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu amethibitisha jinsi afla hiyo ilivyosikika sana. Na kuongeza kusema “Hata kama ni tone la maji katika bahari, lakini mashine mbili zimepokelewa kwa furaha kubwa kwa sababu zimetokana na ishara ya kibaba na umakini mkubwa kwa upande wa Papa Fracisko katika nchi hiyo ambayo inateseka na hali halisi nyeti”.

Na kwa upande wa Askofu Mkuu amebanisha kwamba watu wa nchi ya Equador, wameona “zawadi ya Papa kama mafuta na ishara ya upendo”. Aidha akisimulia jinsi alivyozungumza na Papa binafsi ni kwamba ni nchi ambayo anaipenda kwa sababu kidogo inamkumbusha mambo mengi hasa wakati yeye alipokuwa Provinsi wa Shirika la Kijesuit nchini mwake alikubaliana na Mkuu wa Provinsi ya Equador kukaribishana wanafunzi katika michakato ya mafunzo yao. Na tangu wakati huo amekuwa akifuatilia nchi hiyo kwa karibu na Kanisa lake.  Lakini mbali na uzoefu wake binafsi ishara ya kipapa inaeleweka kwa namna nyingine yaani ya kiumwengu. Ishara hizo ambazo Papa yuko anatimiza katika hali hizo kwa nchi mbali mbali Askofu Mkuu anasisitiza kuwa zinatafuta kufungua macho yetu sisi sote ili tuweze kuwa makini zaidi kwa wale ambao wako karibu nasi na kuwasaidia kila wanapoomba msaada.

Mashine hizo mara baada ya kufika zilitakiwa mara moha kwenye kwenye vyumba vya mahututi kwa sababu wakati huo, mji wa Quito watu walikuwa wamejaa sana na kuwa na ukosefu wa vifaa. Waziri wa Afya alionesha wazi shukrani kubwa kwani alisema kuwa “kila mashine ni maisha na siyo mtu mmoja!  Kwa maana pana. Hiyo ni kweli na kwa maana namna nyingine inachukua  umuhimu wa ishara ya zawadi hiyo. Kila mashine ni maisha! Hata mkurugenzi wa Hospitali hiyo alithibitisha mara moja kuhusu vifaa hivyo kuwa muhimu sana.

27 June 2020, 08:41