Tafuta

Vatican News

Papa Francisko:Janga la corona lisisahaulishe janga la wahamiaji na wakimbizi!

Katika Ujumbe wa Papa Francisko wa siku ya 106 ya wakimbizi na wahamiaji itakayo adhimishwa tarehe 27 Deptemba 2020 imejikita kufafanua majanga ya hali halisi ya watu waliolundikana ndani.Papa anaandika kuwa nyuso zao zinaangaza yule Yesu aliyekuwa mkimbizi nchini Misri.Maneno sita yaliyounganishwa yamesaidia kufafanua ujumbe huu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Tarehe 15 Mei 2020 Ujumbe wa Papa Francisko umetangazwa wa siku ya 106 ya Siku ya Wahamiaji na wakimbizi itakayo adhimishwa tarehe 27 Septemba 2020 unaongozwa na kauli mbiu “Kama Yesu Kristo wanalazimika kukimbia”. Kukaribisha, kulinda, kuhamasisha na kushirikisha waliorundikana ndani. Papa Francisko katika ujumbe wake amesema mwanzoni mwa mwaka huu katika hotuba ya wanadiplomasia wawakilishi wa nchi zao mjini Vatican, katika changamoto za ulimwengu wa sasa alipyaisha wito wake kuhusiana na janga la mlundikano wa ndani wa wahamiaji na wakimbizi. “Migogoro na dharura za kibinadamu, zinaongezeka na machafuko ya hali ya hewa, kuongeza idadi ya watu waliorundikana ndani na kuathiri watu ambao tayari wanaishi katika hali ya umaskini mkubwa. Nchi nyingi zilizoathiriwa na hali hizi zinakosa miundo ya inayofaa na kutosha na ambayo inaruhusu kukidhi mahitaji ya wale ambao wamelundikana”(hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia  9 Janauari 2020).

Mtazamo wa ujumbe kuhusu mlundikano wa watu wa ndani

Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Watu Papa Francisko anasema kuwa walitangaza “Mwongozo wa Kichungaji kuhusu Mlundikano wa ndani”( Rej Vatican 5 Mei 2020), hati ambayo inapendekeza na kuhamasisha matendo ya kichungaji ya dhati  ya Kanisa kwa namna ya pekee katika mantiki hiyo. Kwa sababu hiyo Papa Francisko ameongeza kusema kuwa “nimeamua kujikita katika ujumbe huu kuhusu janga la mlundikano wa ndani, balaa ambalo mara nyingi halionekani, na kwa sababu ya mgogoro wa kidunia uliosababishwa na COVID-19 umesizidisha zaidi”. Mgogoro huu, kiukweli, kwa hali yake, uzito na kiwango chake cha kusambaa kijiografia, kimepunguza zile dharura nyingine za kibinadamu zinazosumbua mamilioni ya watu zinazotakiwa kufanya hatua muhimu na za haraka za kimataifa na misaada ya kuokoa maisha, chini ya ajenda za kisiasa za kitaifa.

Huu siyo wakati wa kusahau mgogoro, wapo wengi wanaishi uzoefu wa shida

Papa Francisko katika ujumbe wake anasema lakini “siyo wakati huu wa kusahau, kipindi cha mgogoro tunachokabiliana nacho kisitufanye tusahau dharura nyingne ambazo zinahitajika kwa ajili ya matendo kwa watu wengi” (Rej Ujumbe wa Urbi et Orbi, 12 Aprili 2020). Katika mwanga wa matukio ya mahangaiko ambayo yamekumbwa mwaka 2020, Papa Francisko anaelekeza ujumbe wake kwa watu waliolundikana wa ndani, kwa wale wote ambao wamejikuta wanaishi na hadi sasa wanaishi uzoefu wa shida, wa upweke, wa kuacha pembeni na kukataliwa kwa sababu ya COVID-19.

Kwa kufafanua zaidi ujumbe wake amepende kuanzia na picha iliyomsadia Papa Pio XII katika kuandika Wosia wa Kitume wa Exsul Familia (1Agosti 1952). (Yaani Familia iliyokimbia). Katika kukimbilia Misri Mtoto Yesu alifanya uzoefu pamoja na wazazi wake wa hali ngumu ya kulundikana na mkimbizi ambaye anajikuta na hofu, ukosefu wa usalama na kutojiamini (taz Mt Mt 2,13-15.19-23).  Kwa bahati mbaya Papa anathibitisha, katika siku zetu, milioni ya familia nafsini mwao wanaweza kujitambua katika huzuni halisi huu. “Karibu kila siku, televisheni na magazeti, yanatoa taarifa za wakimbizi ambao wanakimbia njaa, vita na hatari kubwa, katika kutafuta usalama na maisha yenye hadhi kwa ajili yao na ya familia” (Taz sala ya Malaika wa Bwana, 29 Desemba 2013).

Tunaalikwa kutambua Kristo mwenye njaa katika nyuso za wakimbizi

Katika kila mmoja wao yupo Yesu aliyelazimika wakati wa kipindi cha Erode  kukimbia ili ajiokoe. Kwa maana hiyo Papa anasema katika nyuso zao tunaalikwa kutambua uso wa Kristo mwenye njaa, kiu, uchi, mgonjwa, mgeni na mfungwa anayetuomba (Mt 25,31-46). Ikiwa tutatambua hilo tutatakiwa kumshukuru, kwa sababu ya kukutana naye, kumpenda na kumhudumia. Watu waliorundikana wanatupatia fursa hii ya kukutana na Bwana, hata ikiwa macho yetu yanakuwa  nivigumu kumtambua akiwa na nguo zilizochanika, miguu ikiwa michafu, uso ukiwa umeharibika, mwili uliodhoofika na hasiye na uwezo wa kuzungumza lugha yetu (taz Mahubri 15 Februari 2019). Hii ni changamoto ya kichungaji Papa anasisitiza na kwamba tunaalikwa kutoa jibu ya maneno aliyoelekeza katika ujumbe wa Siku kama hii, kunako mwaka 2018. Maneno hayo ni kukaribisha kulinda, kuhamasisha na kushirikisha na kwa hayo Papa amependelea kuongeze maneno mengi sita ambayo yanafanana na matendo ya dhati yanayounganishwa katika uhusiano wa sababu na matokeo.

Lazima kujua ili kuelewa

Kwa kuanza kufafanua Papa Francisko anasema “ni lazima kujua ili kuelewa. Maarifa ni hatua ya lazima ya kuelekea uelewa wa mwingine. Yesu mwenyewe anafundisha hayo katika tukio la mitume wa Emau: “Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia na kutembea nao. Lakini macho yao yalikuwa yamefumbwa wasimtambue”. (Lk 24,15-16). Kwa maana hiyo wanapozunguza kuhusu wahamiaji na walioundikana, mara nyingi ni kubakia katika idadi. Lakini hiyo siyo suala la idadi ni watu! Papa anabainisha.  Ikiwa tutakutana nao, tutafikia hatua ya kuwafahamu. Na katika kufahamu historia zao, tutaweza kuelewa. Inawezekana kwa mfano kutambua shida yao kama ambayo sisi tumefanya uzoefu na mateso kwa sababu ya janga, na ndiyo sehemu ya maisha ya watu waliolundikana.

Ni lazima kujifanya karibu ili kuwahudumia

Ni lazima kujifanya karibu kwa kuhudumia. Utafikiri ni mchezo lakini mara nyingi ndiyo hivyo anathibitisha Papa. Kwa kutumia neno la Mungu anaandika: “Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo karibu; na alipomwona akamhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. (taz Lk 10,33-34)”.  Kwa maana hii, hofu na hukumu ni nyingi ambazo zinatufanya kutengeza umbali na wengine, na mara nyingi unatuzuia kuwa karibu na wao na kuwahudumia kwa upendo. Kumkaribia jirani mara nyingi ina maana ya kuwa tayari kukabiliana na hatari, kama walivyotufundisha madaktari wengi na wauguzi katika miezi hii ya mwisho. Papa Francisko amebanisha kuwa, suala la kukaa karibu na kuhudumia, ni njia inayokwenda mbali zaidi kwa maana ya uwajibikaji, kwa mfano ni ule mfano mkubwa aliotuachia Yesu alipowaosha miguu wafuasi wake. Yeye alivua na kupiga magoti na kujichafua mikono yake(taz Yh13,1-15).

Ni lazima kujipatanisha ili kusikiliza

Kwa kujipatanisha ni lazima kusikiliza. Papa Francisko anasema anatufundisha Mungu mwenyewe aliyemtuma Mwanaye ulimwenguni, kwa sababu alitaka kusikiliza kilio cha ubinadamu kwa masikio ya binadamu. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee,(…) ili ulimwengu uokolewe katika yeye” (tz Yh  3,16-17).  Upendo ambao unapatanisha na kuokoa huanza kwa kusikiliza. Katika ulimwengu wa leo, ujumbe unazidi kuongezeka mara dufu, lakini unapoteza tabia za kusikilizwa. Ni  kwa njia ya unyenyekevu tu wa kusikiliza na umakini ambao unawezesha kufikia mapatano ya kweli. Kwa wiki hizi za mwaka 2020  zimeonyesha ukimya katika barabara zetu. Balaa la kimya na mahangaiko, lakini vilimetoa fursa ya kusikiliza kilio cha walioathirika zaidi, waliolundikana na sayari yetu iliyougua vibaya sana. Na kwa kusikiliza, tumekuwa na fursa ya kupatana na jirani, na wengi waliobaguliwa, sisi wenyewe na Mungu ambaye hachoki kutukirimia huruma yake

Ili kukua ni lazima kushirikishana

Ili kukua ni lazima kushirikishana. Papa anaandika kuwa, katika Jumuiya ya kwanza ya kikristo, moja ya mambo yake msingi yalikuwa ni kishirikishana.  Na watu waliokuwa wamekiri kuwa waamini “walikuwa na moyo mmoja na roho moja na  wala hapakuwapo na mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali vitu vyote vilikuwa ni vya pamoja”. (Mdo 4,32).  Mungu hakutaka kuwa rasilimali za sayari yetu ziwe mali binafsi kwa baadhi. Hapana, hilo Bwana hakulitaka! Papa Francisko kwa maana hiyo amesisitiza. “Ni lazima tujifunze kushirikishana ili tuweze kukua pamoja, bila kuacha yoyote nyuma! Janga limetukumbusha jinsi gani  sisi sote tulivyo katika mtumbwi mmoja. Kujikuta na wasiwasi na hofu za zinazo tuunganisha wote  zimetuonyesha kwa mara nyingine tena kuwa hakuna anayeweza kujiokoa mwenyewe. Ili kukua kiukweli, lazima tukue pamoja, tushirikishane kile tulicho nacho, kama yule kijana aliyempatia Yesu mikate mitano na samaki wawili…. Ilitosha kwa watu elfu tano(taz Yh 6,1-15)!

Ni lazima kuhusisha ili kuhamasisha

Ni lazima kuhusisha ili kuhamasika. Papa Francisko katika kipengele hiki anasema kuwa kwa hakika Yesu alifanya hivyo kwa mwanamke msamaria(taz Yh 4,1-30). Yesu alimkariba, alimsikiliza, alizungumza kwa moyo wake, na baadaye kumwongoza katika ukweli na kumbadili  kuwa mtangazaji wa Habari Njema hadi kufikia kusema: “Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?”, (taz 4,29). Papa Francisko ameongeza, kusema, mara nyingine mwamko hai wa kuhudumia wengine unatuzuia kutazama utajiri wao. Ikiwa tunataka kweli kuhamasisha watu ambao tunawasaidia, lazima tuwahusishe na ili waweze kujikimu na kujikomboa. Janga linatukumbusha jinsi ilivyo msingi wa uwajibikaji na ni kwa mchango wa wote hata kwa wale ambao hawafikiriwi, inawezekana kwa hakika kukabiliana na mgogoro. Inabidi kutafuta ujasiri wa kufungua nafasi ambazo wote wanaweza kuhisi wameitwa na kuruhusu mitindo mipya ya ukarimu wa kidugu na wa kimshikamano (Tafakari ya Papa katika Uwanja wa  Mtakatifu Petro 27 Machi 2020).

Ni lazima kushirikiana ili kujenga

Ni lazima kushirikishana ili kujenga. Katika kifungu hiki Papa anasema, jambo hili ni kama kile alichosema Mtume Paulo kwa kuwashauri Jumuiya ya Korintho kwamba: “Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mnene katika nia moja, shauri moja na kusikiliza(taz 1 Kor 1,10).  Kujenga Ufalme wa Mungu ndiyo jitihada ya pamoja kwa wakristo wote na kwa maana hiyo ni lazima kujifunza kushirikiana bila kuacha kujaribiwa na wivu, kukosa maelewano na migawanyiko. Na katika muktadha wa sasa lazima kurudia kusema “siyo wakati wa ubinafsi, kwa sababu changamoto ambazo tunaendelea kukabiliana nazo, tunafanana wote na hazibagui mtu. ( Ujumbe wa Urbi et Orbi, 12 Aprili 2020).  Ili kutunza nyumba yetu ya pamoja na kuweza kuifanya ifanane na mpango asili wa Mungu, tunatakiwa kujibidisha  na kuhakikisha ushirikiano wa kimataifa, wa mshikamano kimataifa na jitihada mahalia bila kuacha nyuma yoyote yule.  Papa Francisko kwa kuhitimisha ujumbe wake amependa kupendekeza sala kwa mfano wa Mtakatifu Yosefu , kwa namna ya pekee alipolazimika kukimbilia nchini Misri ili kumwokoa Mtoto.

Sala kwa Mtakatifu Yosefu

Katika Sala hiyo ni inasema:“Baba Wewe ulimkabidhi Mtakatifu Yosefu kile ulichokuwa  nacho cha thamani zaidi, Mtoto Yesu na mama yake ili kuwalinda na kutoka katika vitisho vya waovu. Tunakuomba utusaidie hata sisi kufanya uzoefu wa ulinzi wake na msaada wake. Yeye aliyefanya uzoefu kama yule anayekimbia kwa sababu ya chuki ya wenye nguvu, wawezeshwe faraja na walindwe wale kaka na dada wote ambao kwa msukumo wa vita, umasikini na mahitaji, wameaacha nyumba zao na nchi zao na kujikita katika safari kama wakimbizi kuelekea mahali pa usalama zaidi.

Kwa njia ya maombezi yako wawe na nguvu za kwenda mbele, kufarijiwa wakati wa huzuni na ujasiri katika majaribu. Uwape kidogo huruma wale wanaowapokea kama baba huyo mwenye haki na hekima ambaye alimpenda Yesu kama vile mtoto wake wa kweli na kumsaidia Maria katika safari ndefu. Yeye alikuwa akipata mkate kwa njia ya kazi ya mikono yake, aweze kuwapatia hadhi ya kazi wale wote ambao wameondolea kila kitu na utulivu wa nyumba. Tunakuomba hayo kwa njia ya Yesu Kristo Mwanao ambaye Mtakatifu Yosefu alimwokoa wakati wa kukimbilia Misri na kwa maombezi ya Bikira Maria ambaye alimpenda mchumba wake mwaminifu kwa mujibu wa mapenzi yako Amina. 

15 May 2020, 13:46