Tafuta

2020.05.30  Sala  ya Rosari katika Groto ya Lourdes kwenye bustani za Vatican 2020.05.30 Sala ya Rosari katika Groto ya Lourdes kwenye bustani za Vatican 

Rosari ya Papa na madhabahu duniani kuomba Maria ili kuondokana na janga!

Kwa mara nyingine tena Papa Francisko katika Groto ya Lourdes kwenye bustani za Vatican,amesali rosari huku akiungana na waamini kumwomba Mama Maria ili tukombolewe dhidi ya Covid-19.Sala hii imetangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari kwa kuunganisha madhabahu mbalimbali ulimwenguni.Matendo ya rosari yameongozwa kwa namna ya pekee familia na wawakilishi ambao wamejitolea na kuguswa na virusi hivi kwa karibu.

Na Sr Angela Rwezaula -  Vaticani

Kwa mara nyingine tena, tarehe 30 Mei 2020 saa 11.30 majira ya Ulaya katika Groto ya Lourdes kwenye bustani za Vatican, ameonekana Papa Francisko na waamini wakisali rosari kwa ajili ya kumwomba Mama Maria ili janga la covid-19 liishe. “Ni mama wa Yesu na ni mama yetu, kwani Yeye kila karne amekuwa kimbilio na anaomba msaada si tu huo peke yake, lakini kwa hakika na zaidi ya yote yupo wakati kivuli cha kifo na maumivu vinapokaribia mwanadamu . Ni maneno ya Papa Francisko na  mara baada ya maadhimisho hayo ya rosari, Papa amesalimia kwa namna ya pekee kwa lugha ya kisapanyola waamini wengi waliokuwa walioungana kusali katika Madhabahu ya Amerika Kusini. Katika lugha yake ya kuzaliwa amewashukuru pia kwa ukaribu na kuwatakia usindikizwaji mwema wa Bikira Maria wa Guadalupe.

Maombi kwa mama Maria ili tuepushwe na janga lililopigisha magoti mwanadamu

Hata hivyo katika sala hii inaelekeza kwa mama Maria kufuatia na ulimwengu uliojaribia na janga la virusi vya corana au covid-19 na kusababisha karibu milioni 6 ya maambukizi na zaidi ya vifo karibia 360.000 ulimwenguni. Kwa hakika ni janga ambalo limepigisha magoti ubinadamu wote. Katika sala hiyo kwenye moyo wa Vatican imeunganishwa na ulimwengu mzima kwa madhabahu makuu na zaidi moja kwa moja kuanzia Częstochowa hadi  Fatima, kutoka kwa  mama Yetu wa  Guadalupe, Mexico hadi Lujan, nchini Argentina, kutoka Pompei hadi Lourdes. Lakini hata hivyo madhabahu mengine ya Mama Maria Mkingiwa dhambi  ya asili jijini Washington, kama pia ya  Elele, nchini Nigeria na nyingine zilizoonekana kwenye skrini katika Bustani zaVatican. Ni ushuhuda wa Ulimwengu katika muungano wa sala kwenye  madhabahu ya Bikira Maria Mama yetu wa Mninguni.

Sala ya mwanzo na mwisho kwa mama Maria 

Tukio hili limeandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya, pia tukio hili litafuatia hata la mkesha wa Pentekoste mara baada ya mwezi wa rosari ambao kwa kawaida umetolewa kwa ajili ya Mama Maria. Mwanzoni mwa sala na hata mwishoni, Papa Francisko katika kipindi hiki cha janga ameandika  sala ambayo ameisali  na ambayo inafafanua kwa kina kile ambacho kinatoka ndani ya moyo ili kumkabidhi uchungu wa ubinadamu chini ya miguu yake na kuomba msaada wake.

Mama tunakukabidhi afya ya wagonjwa 

“ Ewe Maria, utuangaze sisi kila wakati kwenye njia yetu kama ishara ya wokovu na tumaini. Tunakukabidhi kwako, Afya ya wagonjwa, ambao wamehusishwa msalabani na maumivu ya Yesu, kwa kudumishwa na  imani yako. Wewe ni Wokovu wa watu wa Waroma, unajua kile tunachohitaji na tuna uhakika kwamba utatutimizia kama ilivyokuwa katika arusi  ya Kana ya Galilaya.Furaha na sherehe zinaweza kurudi baada ya wakati huu wa jaribu. Utusaidie, ee Mama wa Upendo wa Kimungu, kufuata mapenzi ya Baba na kufanya kile ambacho Yesu anatwambia, ambaye alichukua mateso yetu juu yake na kubeba uchungu wetu ili kutuongoza, kupitia msalabani, na kuvuka kwa shangwe ya ufufuo. Amina.

“Tunaukimbilia ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini Ee Bikira mtukufu mwenye baraka”.

 

 

 

30 May 2020, 18:40