Tafuta

Papa Francisko katika katekesi yake amehimiza juu ya uhusiano wa kina wa Mungu katika sala ya kikristo Papa Francisko katika katekesi yake amehimiza juu ya uhusiano wa kina wa Mungu katika sala ya kikristo 

Papa katika katekesi yake anasema Mungu ni mwaminifu tunaweza kumwomba kila kitu!

Papa Franciko katika katekesi ya mwendelezo wa mzunguko kuhusu sala ya kikristo ameomba waamini kuweka mikono yao katikakati ya huduma ya Mungu na sala ya kikirsto inazaliwa kutoka kwake ambaye alijidhihirisha na kuwa na uhusiano na sisi. Katika salamu zake amekumbusha100 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II itakayotimia kilele chake siku ya Jumatatu tarehe 18 Mei 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Leo tuendelee na mchakato wa safari ya Katekesi kuhusu sala iliyoanza wiki iliyopita. Sala inawagusa wote, watu wa kila dini na labda hata wale hawakiri lolote. Sala inazaliwa katika siri ndani mwetu, katika eneo la kiundani na mara nyingi walimu wa kiroho wanaiita “moyo”(Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2562-2563). Kusali kwa upande wetu siyo jambo kandonina siyo la pili kuwekwa pembeni, bali ni fumbo la kina litokalo  ndani mwetu. Hisia za ndani zinaomba, lakini huwezi kusema kuwa sala ni hisia tu. Akili inasali, lakini huwezi kusema kuwa ni tendo la kiakili tu. Mwili unasali, lakini huwezi kuzungumza na Mungu hata katika ulemavu mbaya. Kwa maana hiyo ubinadamu wote unasali ukiwa unasali kwa “moyo. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko, Jumatano tarehe 13 Mei 2020 akiwa katika Maktaba ya Kitume Vatican, kwa wakati huu wa janga.   Papa Francisko ameendeleza tafakari kuhusiana na sala katika mzunguko huo aliouanza wiki iliyopita kuhusu “sala ya kikristo”.

Sala ni maombi yanayokwenda zaidi ya nafsi yetu

Sala ni mwamko, ni maombi ambayo yanakwenda zaidi nafsi yetu binafsi. Ni jambo ambalo linazaliwa ndani ya kina cha utu wetu na kuelekea kwa sababu ya kuhisi ukosefu wa kukutana. Sala ni sauti ya “mimi anayetafuta na ambaye hutulia, katika kutafuta “Wewe”. Kinyume chake, sala ya mkristo, inazaliwa kutokana na maonyesho. Ile ya “wewe haikubaki imeviringishwa katika fumbo, bali iliingia katika uhusiano na sisi, amesema Papa. Ukristo ni sababu ambayo inaadhimisha kila wakati yale “ maonesho ya Mungu yaani tokeo lake. Hii yote inaonekana katika sikukuu za mwanzo wa mwaka wa liturujia ambazo ni sherehe za Mungu huyo ambaye hakubaki mafichoni, bali ni anayetoa urafiki wake na watu. Mungu anajionesha utukufu wake katika umaskini wa Bethlehemu, katika kusujudiwa na Mamajusi, katika ubatizo huko Yordanina katika miujiza ya harusi ya Cana. Papa Francisko ameongeza kusema, Injili ya Yohane inahitimisha na uthibitisho wa taarifa fupi katika wimbo mkuu wa Dibaji “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua” (Yh 1,18).

Usiano wa Mungu katika sala na sura ya upole wa kukuondolea woga

Sala ya kikristo inaingia katika uhusiano na Mungu kwa sura ya upole ambao unataka kuondoa kila woga wa watu. Hiyo ndiyo tabia ya kwanza ya sala ya kikristo amethibitisha Papa. Ikiwa watu daima walikuwa wamezoea kukaribia Mungu kidogo na wasiwasi, wakiwa  na woga wa fumbo hili la kushangaza, na la kiajabu, ikiwa watu walikuwa wamezoea kumtukuza na tabia ya utumwa sawa sawa na yule anayeongozwa na ambaye hataki kukosea heshima kwa bwana wake, kinyume chake wakristo wanamwendea wakimwita kwa imani jina lake  “Baba”. Kwa uhusiano wa Mungu ulio katika ukristo uliondoa uhusiano wowote  wa kimadaraka. Na katika urithi wa imani yetu hauna kielekezo ambacho kinaonesha kuwekwa chini, ya “utumwa au kulipwa kwa sababu ya kulindwa, japokuwa yapo maneno kama ya “agano”, urafiki”na “muungano”.  Katika hotuba yake ndefu ya buriani kwa wafuasi, Yesu aliwambia hivi: “Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kudumu; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. (Yh 15,15-16).

Mungu ni rafiki, mshiriki na bwana harusi

Mungu ni rafiki, mshiriki na Bwana Harusi. Katika sala inawezekana kudumisha uhusiano makini na Yeye na kwa udhirisho huo katika sala ya “Baba Yetu”, Yesu analitufundisha kumwomba baadhi ya mambo. Papa Francisko amesisitiza kuwa kwa upande wa Mungu tunaweza kumwomba kila kitu, kumweleza kila kitu na kumsimulia yote. Haijalishi ikiwa katika uhusiano na Mungu tunahisi kuwa na kasoro, kwa mfano sisi siyo marafiki wema, ni watoto tusio kuwa na utambuzi, sisi siyo bi na bwana harusi waaminifu. Lakini Yeye anaendelea kutupenda. Na ndicho Yesu anajionesha wakati wa Karamu  ya mwisho aliposema: “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu” (Lk 22,20). Katika ishara hiyo ya Yesu, alikuwa anatanguliza katika karamu Kii fumbo la Msalaba. Papa Francisko ameongeza kusema, Mungu ni agano aminifu, ikiwa watu wanaacha kupenda, lakini Yeye anaendelea kupenda, hata kama upendo wake ulimfikisha Karvari.

Tujaribu kusali kwa kuonga katika fumbo la Agano

Kwa kuhitimisha Papa Francisko amehimiza kwamba “tujaribu wote kusali na kwa kuingia katika fumbo la Agano. Kujikita katika sala katikati  ya mikono ya huruma ya Mungu na kuhisi tumeviringishwa ndani ya fumbo lile la furaha ambalo ni maisha ya utatu, na kuweza kuhisi kama wale walioalikwa, lakini bila kustahili heshima kubwa. Na kurudi kwa Mungu, katika mshangao wa sala. Je inawezaka kwamba “Wewe kujua upendo tu? Yeye hachui chuki. Alichukiwa lakini hakujua kuchukia. Yeya anajua upendo tu. Huyo ndiyo Mungu tunaye mwomba, ndiyo nuru kuu ya kila sala ya Mkristo. Mungu wa upendo, Mungu wetu ambaye anatusubiri na kutusindikiza.

13 May 2020, 13:46