Tafuta

Vatican News
2020.05.27 Katekesi ya Papa Francisko 2020.05.27 Katekesi ya Papa Francisko  (Vatican Media)

Papa Francisko:Sala ni kizuizi cha uovu na inaweza kuandika hatma tofauti !

Katika tafakari ya katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 27 Mei 2020 amejikita kuzungumzia juu ya sura za kwanza za kitabu cha Mwanzo ambapo amekumbusha kwamba wakati uovu unazidi kusambaa kama mafuta,sala ya mwenye haki ina uwezo wa kurudisha tumaini.Sala ni mnyororo wa maisha,ni kizuizi cha uovu na inaweza kuandika hatma tofauti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ishara ya Mungu mbele ya mwanadamu ni nzuri lakini katika mambo yetu ya kila siku tunafanya uzoefu wa uwepo wa ubaya. Katika sura za kwanza za kitabu cha Mwanzo,kinasimulia maendeleo ya kukua kwa dhambi katika mambo ya mwanadamu. Adamu na Eva ( rej. Mw 3,1-7) walipata mashaka juu ya  ukarimu wa Mungu na kufikiria kuwa wanaye Mungu  mwenye wivu, anayewazuia furaha yao. Na ndipo kiburi kikaanzia hapo. Hawakuamini tena Muumba mkarimu, ambaye anatamani furaha yao. Moyo wao uliangukia katika kishawishi cha ubaya, “tutakuwa kama Mungu” ( Mw 3,5.). Lakini uzoefu wao ukaenda kinyume kwani macho yao yalifunguka na kugundua kuwa wako uchi (rej. Mw, 3,7). Ndiyo Mwanzo wa tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko tarehe 27 Mei 2020 akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume mjini Vatican, ikiwa ni mwendelezo wa katekesi kuhusu kitabu cha Mwanzo.

Historia ya udugu wa kwanza kuishia katika mauaji:Kaini dhidi ya Abeli 

Papa Francisko amefafanua kuwa ubaya unageuka kwa mara nyingine kuendelea hata kwa kizazi cha pili cha mwanadamu. Hiyo ni katika tukio la Kaini na Abeli (rej. Mw 4,1-16). Kaini alikuwa na wivu wa nduguye, licha ya kuwa kifungua mimba, lakini alikuwa anamwonaAbeli kama mshindani wake na kama anayekwaza ukuu wake. Ubaya unaanza namna hiy  na kuingia katika moyo, mawazo daima ya kutazama vibaya mwingine na kumshuku. Hiyo pia inakuja katika mawazo, ya kufikiria ‘huyo ni mkatili, atanifanya vibaya’. Ubaya huo ukamsonga ndani ya moyo wake na Kaini akashindwa kujithibiti. Na kwa maana hiyo historia ya udugu wa kwanza ikahitimishwa kwa mauaji. Papa Francisko amebainisha jinsi gani anafikiria udugu wa kibinadamu na vita kila  sehemu.

Ubaya unasambaratika kama mafuta

Katika uzao wa Kaini kulikuwa kunakuzwa kazi na sanaa, lakini hata kukua kwa vurugu, kama anavyoelezwa katika wimbo wa Lameki ambaye alikuwa anaimba wimbo wa kulipiza kisasi  kuwa:“maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha, kijana kwa kunichubua(…). Kaini atalipiwa kisasi mara saba lakini hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba (Mw,4,23-24).” Kulipiza kisasi Papa anaongeza, alifanya na kulipa. Lakini hiyo hakusema hakimu bali, ninasema mimi. Mimi ninajifanya hakimu wa kila hali”. Kwa namna hiyo ubaya ukapanuka yakasambaratika kama  mafuta ya petroli hadi kufikia kila kona. “Bwana akaona kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote ( Mw 6,5).

Katika picha za gharika kuu na mnara wa Babeli, kuna haja ya ujio wa Kristo

Papa Francisko akiendelea na ufafanuzi wa ubaya amesema, picha kubwa zinazohusu Gharika kuu (katika sura ya 6-7) na ile  ya mnara wa Babeli (sura ya 11) vinaonesha kuwa kuna haja ya kuwa na  mwanzo mpya wa uumbaji mpya ambao utakamilika katika Kristo. Na zaidi katika kurasa za kwanza za Biblia kumeandikwa historia nyingine, isiyojitambulisha sana. Ni nyenyekevu sana, na yenye ibada ambayo inawakilisha ukombozi wa matumaini. Ikiwa hata karibu kila mtu anafanya kwa njia ya kikatili, na kufanya chuki na kushinda injini kubwa ya mambo ya wanadamu, kuna watu wenye uwezo wa kusali kwa Mungu kwa uaminifu, wenye uwezo wa kuandika hatma ya mwanadamu kwa njia tofauti. Abeli alimtolea Mungu dhabihu ya matunda ya kwanza.

Ni muhimu kuomba tuokolewa na tamaa mbaya

Papa Francisko akiendelea kufafanua  amesema kuwa baada ya kifo chake Abeli, Adamu na Eva walipata mtoto wa tatu Seth na kwake yeye akazaa mwana akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo walipoanza kuliita Jina la Bwana (Mw, 4,26). Baadaye akatokea Henoko na ambaye alikwenda na Mungu lakini baadaye akatoweka kwa maana Mungu alimtwaa (Mw 5, 22.24). Na mwisho kuna historia ya Nuhu, alikuwa mtu wa haki ambaye alikuwa anatembea na Bwana (Mw 6,9), mahali ambapo Mungu alikuwa amependekeza kumfutilia mbali mwanadamu, japokuwa Nuhu akapata neema machoni pa Bwana (Mw 6,7-8). Katika kusoma simulizi hizi, inafanana kwamba sala ndiyo mwanga, ndiyo kimbilio la mwanadamu mbele ya mawimbi yaliyojaa ubaya ambao unakua katika ulimwengu. Kwa kutazama vizuri hayo Papa anasema , tuombe  ili tuweze kuokolewa sisi wenyewe. Ni muhimu! Omba: “Bwana, tafadhali, niokoe mimi mwenyewe, dhidi ya matamanio yangu na tamaa zangu. Niokoe mimi mwenyewe”.

Waombaji wa kwanza walikuwa wahudumu wa amani

Waombaji wa kwanza katika kurasa za kwanza za Biblia, ni watu wahudumu wa amani, ambainisha Papa. Kiukweli sala ni ya kweli kiwa ni  huru dhidi ya vurugu za ndani,  na ni mtazamo unolekeza kwa Mungu, kwa sababu aweze kurudi kuutunza moyo wa mwanadamu. Katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki inasomeka hivi: ubora wa sala hii umefanyiwa uzoefu na wenye haki  kwa wengi katika dini zote (KKK, 2569). Sala inatunza kiota cha kuzaliwa katika mahali ambapo mtu amekuwa na uwezo wa kupanua jangwa.

Kufundisha kusali watoto wakiwa wadogo

Papa Francisko amekumbuka historia  ya mtu mmoja  kiongozi mkuu wa serikali ,lakini siyo wa enzi hizi bali zilizopita. Alikuwa ni mkana Mungu kwa maana hawa na maana yoyote ya dini ndani ya moyo wake. Akiwa mdogo lakini  alikuwa anasikia bibi yake anasali, jambo ambalo lilibaki ndani ya moyo wake. Siku moja katika wakati wake mgumu wa maisha, alirudia kukumbuka ndani ya moyo wake na kusema “lakini bibi alikuwa anasali…”. Na yeye alianza kusali akirudia mambo ambayo alikuwa anasikia bibi yake anasema na hapo aliweza kukutana na Yesu.  Papa Francisko katika hili amesema “Sala ni mnyororo wa maisha daima. Wanawake na wanaume ambao wanasali, wanapanda maisha, Sala inapanda maisha. Sala ndogo…”

“Kwa namna ilivyo muhimu sala, wafundisheni watoto kusali”. Kwa mujibu wa Papa anahuzunika anapomwona mtoto hajuhi kufanya ishara ya msalaba. Knjia hiyo amesisitiza “ Wafundisheni kusali vizuri ishara ya msalaba maana ndiyo sala ya kwanza. Lakini muhimu watoto wajifunze kusali. Na labda wanaweza kusahau na kuchukua njia nyingne; lakini kile ambacho walijifunza wakiwa wadogo kinabaki ndani ya mioyo kwa maana ni maisha, ni mbegu ya mazungumzo na Mungu” amesema Papa Francisko.

Ukuu wa Mungu unazunguka kama mnyororo kwa wanawake na wanaume wasiotambuliwa

Na ndiyo maana ukuu wa Mungu unazunguka katika mnyororo wa wanaume na wanawake ambao mara nyingi hawatambuliwi au wamewekwa pembezoni mwa dunia! Safari ya Mungu katika historia ya Mungu inajikita kupitia kwao; imepita kwa ajili ya kinachobaki cha ubinadamu ambao unatimiza miujiza yake na hasa kubadili mioyo yetu kama  jiwe kuwa moyo wa nyama(rej 36,26). Hii inasaidia sala, kwa maana sala inafungua mlango wa Mungu na ili iweze kubadili moyo wetu ambao mara nyingi umekuwa  wa mawe uweze kuwa wa nyama. Inahitajika ubinadamu mwingi na ubinadamu unaosali vizuri.” Ameihitimisha

27 May 2020, 13:01