Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ametangaza Mwaka maalum wa Laudato si wa kutafakari kuhusu Wosia juo wa Kipapa kuanzia tarehe 24 Mei 2020-24 Mei 2021. Papa Francisko ametangaza Mwaka maalum wa Laudato si wa kutafakari kuhusu Wosia juo wa Kipapa kuanzia tarehe 24 Mei 2020-24 Mei 2021. 

Papa Francisko:Mwaka maalum wa Laudato sì na utunzaji wa nyumba yetu!

Mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, Papa Francisko amekumbuka mwaka wa tano wa kutangazwa wa Laudato si ambapo kuanzia tarehe ya kuhitimisha Wiki ya Laudato 24 Mei ndipo pia umeanza mwaka maalum wa kutafakari juu ya utunzaji wa mazingira.Aidha amewawakikisha uwezekano mwingine wa kwenda jimbo la Acerra mahali ambapo alitakiwa kwenda lakini kwa sababu ya dharura za janga haikuwezekana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika tukio la kilele cha miaka 5 tangu kutangaza kwa Wosia wa  Kitume wa Laudato sì  Papa Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, amekumbusha ni kwa jinsi gani katika Wosia huo alitaka kutoa umakini wa kilio cha sayari na cha maskini. Ameshukuru jitihada na mipango iliyoanzishwa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo ya watu kuhusu “Wiki ya Laudato si” ambayo imeanza tangu tarehe 16 hadi 24 Mei.  Kwa maana hiyo Papa Francisko amesema “utachanua mwaka maalum wa Laudato sì, mwaka Maalum wa kutafakari kuhusu “ Wosia  kuanzia  tarehe 24 Mei hadi tarehe 24 mwaka kesho.  Papa Francisko kwa maana hiyo ametoa mwaliko wake kuwa “ ninawaalika watu wote wenye mapenzi mema kujongea ili kuweza kutunza nyumba yetu ya pamoja, na ndugu zetu, kaka na dada waadhaifu zaidi. Katika Tovuti Papa Franceso amebanisha kwamba watatangaza sala ambayo imetolewa kwa ajili ya Mwaka huo. Kwa maana hiyo itakuwa vizuri sana kuisali”, ameshauri.

 Sala iliyopendekezwa katika fursa hii:

Mungu anayempenda, Muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo. Fungua akili zetu na uguse mioyo yetu, ili tuweze kuwa sehemu ya uumbaji, zawadi yako. Uwepo kwa wahitaji katika nyakati hizi ngumu, hasa maskini na walio dhaifu zaidi.

Utusaidie kuonyesha mshikamano wa ubunifu katika kukabiliana na athari za janga hili la ulimwengu. Utujalie tuwe na ujasiri wa kukumbatia mabadiliko yanayolenga kutafuta wema wa pamoja.

Na sasa, zaidi kuliko hapo awali, tunaweza kuhisi kuwa sote tumeunganishwa na kutegemeana. Utufanye kana kwamba sisi tunaweza kusikiliza na kuitikia kilio cha dunia na kilio cha masikini.

Mateso ya sasa yanaweza kuwa maumivu ya kuzaa ulimwengu wa kidugu na endelevu. Chini ya mtazamo wa upendo wa mama Maria msaada wa wakristo, tunakuomba kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Sikukuu ya Mama Maria Msaada wa wakristo

Papa Francisko Pia amekumbuka Siku Kuu ya Mama Maria msaada wa wakristo, kwa maana hiyo amewatumia salam kwa upendo mkuu Wasalesiani wote kike na kiume. Anakumbuka kwa uhai, mafunzo ya kiroho aliyopata kutoka kwa watoto wa Mtakatifu Don Bosco.

Papa akumbuka ziara ya kichunganji iliyositishwa huko Acerra

Papa Francisko amekumbusha ni kwa jinsi gani leo hii alikuwa aende huko Acerra ili kuwaitia imani watu  na jitihada  kwa wale wanao hamasisha kupingana na janga uchafuzi wa mazingira kwa kile wanachokiitia “ ardhi ya moto”. Ziara yake imesitishwa lakini pamoja na hayo wamesalimia maaskofu, mapadre, familia na jumuiya nzima ya jimbo na kwamba baraka yake  na kuwatia moyo katika matarajio ya kukutana tena mara ikiwezekana.

24 May 2020, 14:15