Tafuta

Papa Francisko ameomba mshikamano kwa ajili ya ukanda wa Sahel kutokana na ukame Papa Francisko ameomba mshikamano kwa ajili ya ukanda wa Sahel kutokana na ukame  

Papa Francisko:mshikamano kwa Sahel unahitajika kudhibiti ukame!

Papa Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malkia wa Mbingu amekumbuka tarehe muhimu za bara la Ulaya hasa katika kumbukizi la mwanzo wa mchakato wa ushirikishwaji,pia bara la Afrika mahali ambapo umeanzishwa mpango wa kupanda miti kwa ajili ya kuwasaidia watu washinde ukame katika ukanda wa Sahel.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari la Neno la Mungu la Dominika ya V ya Kipindi cha Pasaka na Sala ya Malkia wa Mbingu, tarehe 10 Mei 2020, Papa Francisko akiwa katika Jumba la Maktaba ya Kitume amegeukia dunia kwa  kusema" Wazo langu leo hii linakwenda kwa Ulaya na kwa Afrika. Ulaya ni katika fursa ya kuadhimisha miaka 70 tangu Tamko la Schuman kunako tarehe 9 Mei 1950. Tamko hili linajika kufuata mchakato wa ushirikishwaji wa Ulaya kwa kuruhusu mapatano ya watu katika bara, baada ya Vita ya Pili ya Dunia na kipindi kirefu chenye msimamo na amani ambayo leo hii tunafaidika. Roho ya Tamko la Schuman isikose kwa wale ambao wanahusika katika Umoja wa Ulaya na ambao wanaalikwa kukabiliana katika roho ya mapatano na kushirikishana na matokeo ya kijamii na kiuchumi yaliyosababishwa na janga."

Papa Francisko akielekeza mawazo kwa bara la Afrika

Papa Francisko akiendelea pia amesema "Kwa mtazamo mwingine pia unakwenda hata Afrika, kwa sababu kunako tarehe 10 Mei 1980, yaani miaka 40 iliyopita Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa ziara yake ya kwanza ya kichungaji katika bara hilo  alitoa sauti ya kilio cha watu wa Kanda ya Sahel, wakati wa wanajaribiwa na ukame. Leo hii ninawapongeza vijana ambao wanajikita katika jitihada za kuanzishwa kwa “Laudato Si’ Alberi”. yaani "Miti ni Sifa kwa Bwana'. Lengo la mpango huo ni kupanda miti isiyopungua milioni moja ambayo itapelekwa katika kanda ya Sahel na kuwezesha sehemu hiyo kubwa kuwa “uwanda wa kijani wa Afrika” . Ni matumani  yangu kuwa wengi wanaweza kufuata mfano wa mshikamano wa vijana hawa" Papa Francisko amesema.

Papa akumbuka sikukuu  ya mama   

Vile vile Papa hakuishia hapo kwani akikumbuka  kilele cha siku hii amesema "Leo hii katika nchi nyingi zinaadhimisha Siku kuu ya Mama. Ninapendelea kukumbuka kwa shukrani na upendo wote mama wote nikiwakabidhi kwa ulinzi wa Maria, Mama  wa Yesu wa Mbinguni." Wazo pia linawaendea mama wote ambao wametangulia katika maisha mengine, na wanao tusindikiza Mbinguni. "Tufanye ukimya kidogo kwa ajili ya kuwakumbuka kila mmoja mama yake…" Na kwa kuhitimisha Papa Francisko amewatakia Dominika njema, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake. 

10 May 2020, 14:31