Tafuta

Vatican News
Papa Francisko katika sala Papa Francisko katika sala   (Vatican Media)

Shiriki na Papa Francisko kusali Rosari Jumamosi 30 Mei saa 11.30 jioni!

Jumamosi,tarehe 30 Mei 2020 saa 11.30 jioni majira ya Ulaya Papa Francisko ataongoza sala ya Rosari itakayotangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari kutoka Grotto ya Lourdes katika bustani ya Vatican ili kumwomba Bikira Maria tuepushwe na janga hili.Madhabahu mengi ulimwenguni,Makanisa makuu yote na waamini wanaalikwa kushiriki katika tukio hili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mada ambayo itaongoza Papa Francisko katika kusali rosari, siku ya Jumamosi tarehe 30 Mei 2020, ni “Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Maria mama yake Yesu na ndugu zake (rej. Mdo 1,14)”. Papa ataungana na madhabahu yote ulimwenguni ambayo kutokana na dharura ya kiafya yamelazimika kusitisha shughuli zao za kawaida na hija zao. Sala hiyo ya rosari itakayoonyesha mubashara kutoka Grotto ya Lourdes katika bustani ya Vaticani saa 11.30 majira ya Ulaya, ambapo Papa kwa mara nyingine tena atakuwa karibu na binadamu wote katika sala ili kumwomba Bikira Maria msaada na kimbilio dhidi ya janga.

Wawakilishi wa familia na vitengo husika walioguswa na janga wataongoza matendo ya rosari

Mpango huo umeandaliwa na Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya na ambao utaona ujumuishwaji wa familia na wawakilishi wa kike na kiume  wa sekta mbali mbali zinazohusika zaidi na kwa namna ya pekee walioathirika na janga hili, ambao watakabidhiwa kuongoza matendo ya Rosari. Kwa njia hiyo ni pamoja na madaktari na wauguzi, wagonjwa waliopona na wagonjwa walioteseka katika kuomboleza kwa ajili ya  ndugu zao, mkuu wa hospitali na mtawa mmoja muuguzi, mfamasia na mwandishi wa habari, na mwishowe mmoja wa kujitolea kutoka katika kikosi cha Ulinzi na usalama wa Jamii na familia yake,  pia familia moja ambayo ilishuhudia kuzaliwa  mtoto hasa katika wakati mgumu zaidi, ili kuelezea tumaini kwamba hakuna ulazima wa kushindwa na kukata tamaa.

Chini ya miguu ya Mama wa mbingu, atakabidhiwa hofu na uchungu wa binadamu

 “Katika hitimisho la Mwezi ambao umetolewa kwa ajili yake chini ya miguu yake kwa uhakika  Mama wa mbingu, hatakosa msaada wake”, kwa mujibu wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya  na kwamba Papa Francisko ataweka mashaka na uchungu wa ubinadamu.

Madhabahu:Lourdes,Fatima,Lujan,Milagro,Guadalupe,Mtakatifu Giovanni Rotondo na Pompei

Hata hivyo kuhusiana na maeneo makubwa hivi kutoka mabara matano wataungana na madhabahu mengi kwa namna ya pekee kuanzia Lourdes, Fatima, Lujan, Milagro, Guadalupe, Mtakatifu Giovanni Rotondo na Pompei, Nigeria na sehemu nyingine nyingi. Katika barua, Askofu Mkuu Rino Fisichella, Rais wa Baraza Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya,  ameilekeza moja kwa moja kwa wasimamizi wa Madhabahu akiwaalika kuandaa na kuhamasisha wakati huu maalum wa sala ukiambatana sawa na itifaki za sasa za afya na kuwa makini katika masaa kulingana na muda huo.

 

 

26 May 2020, 15:59