Tafuta

Vatican News
Kipindi cha janga la virusi vya covid-19 nchini Lebanon. Kipindi cha janga la virusi vya covid-19 nchini Lebanon.  (ANSA)

Msaada maalum kutoka kwa Papa kwa ajili ya nchi ya Lebanon!

Kwa njia ya Ofisi ya Katibu wa Vatican na Baraza la Makanisa ya Mashariki wameazimia kutuma katika Ubalozi wa Kitume nchini Lebanon,jumla ya dola za kimarekani 200.000 ili kufadhili mafunzo ya wanafunzi 400.Ni matumaini kuwa msaada huo unaweza kuwa mshikamano makini na matarajio kwamba wadau wa kitaifa na kimataifa waweze kuendeleza jukumu lao kwa ajili ya wema wa kizazi nchini Lebanon.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa  utambuzi na upendo mkuu wa Papa Francisko  bado anaendelea kufuatilia kwa miezi hii hali halisi ya nchi ya Lebanon, iliyotajwa kwa mujibu wa  Mtakatifu Yohane Paulo II  aliitaja kama “Nchi ya Ujumbe”, na pia ni mahali ambaoo Papa Mstaafu Benedikto XVI alipata kutangaza Wosia wake wa Kitume baada ya Sinodi ya Makanisa ya Mashariki, na nchi ambayo imedumu daima na kuwa mfano mwema wa kuishi udugu ambao unaelezwa katika Hati kwa ajili ya Udugu wa Kibinadamu uliotolewa mwaka jana kwa ulimwenguni kote.

Matatizo ya kiuchumi nchini Lebanon

Mwaka huu katika nchi hiyo imejikita imedumbikia katika wakati mgumu sana, kipindi ambacho kimesababaisha mateso mengi kama vile umasikini na hatari ya kuibiwa matumaini kwa kizazi kipya cha vijana ambao hawaoni upeo wa wakati endelevu wao. Katika mantiki hiyo imekuwa vigumu sana hata kuwahakikisha watu Lebanon  na pia watoto na vijana kwenda shuleni hasa katika vituo vidogo vidogo na zaidi vinavyoendeshwa na Taasisi za Kikanisa.

Ishara ya ukaribu wa Papa

Kama ishara muhimu sana ya ukaribu  Papa Ftancisko kupitia ofisi ya Katibu wa Vatican na Baraza la Makanisa ya Mshariki wameazimia kutuma katika Ubalozi wa Kitume, jumla ya Dola za Kimarekani 200.000  ili kufadhili mafunzo ya wanafunzi 400, huku wakiwa namatumaini kuwa msaada huo unaweza kutimiza lengo la mshikamano na matarajio kuwa wadau wa kitaifa na kimataifa wanaweza kuendelezwa uwajibikaji wao  hasa katika kutafuta wema wa pamoja ili kushinda migawanyiko na kuweka pembeni maslahi binafsi.

Msaada huo unajumuishwa na mchango wa Baraza la Makanisa ya Mashariki

Kwa mujibu wa taarifa za Vatican, zinabainisha kuwa msaada huo unajumuishwa hata mchango mwingine ambao  umekusanywa katika Mfuko wa Dharura wa Baraza la Makanisa ya Mashariki (CEC) kwa siku hizi ambapo wanaendelea kukabiliana na dharura ya janga la covid-19. "Mama wa Mungu ambaye analinda Lebanon kutika mlima wa Harissa, awalinde watu hawa wa Lebanon pamoja na watakatifu wapendwa wa Nchi hiyo".

14 May 2020, 13:33