Tafuta

Katika kipindi hiki cha kihistoria  hakuna maandamano ya mahujaji kwa Bikira Maria wa Fatima Katika kipindi hiki cha kihistoria hakuna maandamano ya mahujaji kwa Bikira Maria wa Fatima  

Fatima:Papa amesema tuungane na Bikira Maria kusali ili janga liishe!

Katika salamu zake Papa Francisko mara baada ya Katekesi yake kwa lugha mbali mbali amekumbuka siku kuu ya Bikira Maria wa Fatima,ikiwa ni kukumbuka lile tokeo la kwanza kwa watoto wachungaji watatu kunako tarehe 13 Mei 1917.Papa ameshauri kusali kwa Bikira Maria kwa ajili ya janga liweze kuisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari ya katekesi, Papa Francisko wamewakumbusha watu wote juu ya kumbukizi ya tokeo la Bikira Maria wa Fatima kwa watoto watatu wachungaji kunako mwaka tarehe 13 Mei 1917. Papa amawalika waamini kumwomba Bikira Maria, kila mmoja aweze kutunza upendo wa Mungu kwa jirani.Amewakumbuka kwa namna ya pekee vijana, wazee , wagonjwa na wana  upendo na huruma kimbilio hakika katika matatizo. Na katika lugha ya kingereza ameungana na watu wote akiwaombea katika kipindi hiki cha Pasaka, furaha na nguvu zitokazo kwa Kristo mfufuka. Na Bwana awabariki

Kwa kuendelea na kuzuia usambaaji wa covid -19, Madhabahu ya mama Maria nchini Ureno mwaka huu maadhimisho yanafanyika moja kwa moja kupitia vyombo vya habari,luninga na mitandao ya kijamii. Katika ujumbe kutoka kwa msimamizi wa Madhabahu ya Fatima Kardinali António Augusto dos Santos Marto na Gambera,Padre Carlos Cabecinhas, wanasema tarehe 13 Mei katika madhabu hiyo ina ukuu muhimu ulimwenguni na kwa maana hiyo wanaalikwa kuungana kiroho hata kwa njia ya mitandao.

Inakumbukwe  hata mwaka 1917 kulikuwa na janga la virusi kwa jina  spanyola. Lakini wakati huo kule Fatima kulitokea ujumbe wa matumaini katika kipindi sawa na hiki cha matatizo, waanaandika wasimamizi hao. Na  ujumbe uliotolewa kwa Lucia kutoka kwa Maria ulikuwa unasema “usikate tamaa  na mimi sitokuacha. Katika moyo wa Maria asiye na doa kutakuwa na kimbilio na safari itakayo kufikisha hadi kwa Mungu”. Na hayo ndiyo matumaini ya ujumbe huo wa Fatima kwa watu wote wanawake na wanaume duniani kote.

Hata hivyo tarehe 13 Mei  inakumbusha siku ile ile ya mwaka 1917  ambapo Bikira Maria aliwatokea kwa mara ya kwanza ndugu watatu, Francis, Lucia na Yasinta kwa kuwatuma ujumbe wa kutubu na kuiamini Injili, kwenye Kijiji cha Cova da Aria, Fatima, Ureno. Baada ya matukio mbali mbali na uthibitisho mwaka 1930, Jimbo Katoliki la Leira, likakubali ukweli wa Watoto watatu wa Fatima, kumwona Bikira Maria na ndiyo ukawa mwanzo mkuu wa ibada za Bikira Maria wa Fatima kwa miaka  Kunako mwaka 1942 Papa Pio wa XII akauweka ulimwengu wote chini ya ulinzi na tunza ya Moyo Safi wa Bikira Maria. Mtakatifu Yohane Paulo II amekuwa na ibada kuu kwa maombezi ya Bikira Maria wa Fatima kutokana na kunusurika kwa kifo baada ya kupigwa risasi kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican  tarehe 13 Mei 1981.

Madhabu ya Fatima yametembelea na mapapa wengi na mara ya mwisho  Papa Francisko alifanya hija ya kitume kuanzia tarehe 12- 13 Mei 2017, nchini Ureno kwa kushiriki Jubilei ya miaka 100 tangu Bikira Maria alipowatokea Watoto wa Fatima, na wakati huo huo akawatangaza Wenyeheri Francis na Yacinta Marto kuwa watakatifu.  Hija ya kitume ya Papa iliongozwa na kauli mbiu “Papa Francisko mjini Fatima pamoja na Bikira Maria kama mahujaji wa matumaini na amani”.

13 May 2020, 13:50