Tafuta

Kardinali Pietro Parolinm, Katibu mkuu wa Vatican baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na Papa Francisko ameamua kufanya mabadiliko katika Kitengo cha CED na APSA. Kardinali Pietro Parolinm, Katibu mkuu wa Vatican baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na Papa Francisko ameamua kufanya mabadiliko katika Kitengo cha CED na APSA. 

Papa Francisko afanya Marekebisho CED na APSA

Papa Francisko afanya mageuzi: Shughuli zilizokuwa zinatekelezwa na Kituo cha Takwimu cha Vatican, “Centro Elaborazione Dati, CED” ambacho kwa wakati huu ni Kitengo kilichoko kwenye Utawala wa Hazina ya Vatican, APSA, kuanzia sasa zitahamishwa kwenye Sekretarieti ya Uchumi ya Vatican, SPE, kwa kuzingatia itifaki ya makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa Taasisi hizi mbili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, katika mazungumzo ya faragha na Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni, wamegusia umuhimu wa kuunganisha habari za kiuchumi na kifedha mjini Vatican, ili kuweza kuwa na mfumo imara zaidi wa habari kwa kurahisisha shughuli mbalimbali zinazotekelezwa mjini Vatican. Lengo ni kuimarisha udhibiti wa takwimu ili kuhakikisha kwamba, Sekretarieti kuu ya Vatican na Taasisi zake, inaweza kutekeleza kikamilifu majukumu yake. Kumbe, shughuli zilizokuwa zinatekelezwa na Kituo cha Takwimu cha Vatican, “Centro Elaborazione Dati, CED” ambacho kwa wakati huu ni Kitengo kilichoko kwenye Utawala wa Hazina ya Vatican, APSA, kuanzia sasa zitahamishwa kwenye Sekretarieti ya Uchumi ya Vatican, SPE, kwa kuzingatia itifaki ya makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa Taasisi hizi mbili.

Hawa ni Askofu Nunzio Galantino pamoja na Mheshimiwa Padre Juan Antonio Guerrero Alves, S.J, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi Vatican. Maafisa na wafanyakazi wote wa CED kuanzia sasa watawajibika moja kwa moja kwenye Sekretarieti ya Uchumi ya Vatican, SPE, kwa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa. Sekretarieti ya Uchumi ya Vatican itasimamia shughuli zote pamoja na kuhakikisha kwamba, APSA inatekeleza dhamana na majukumu yake barabara. Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa rasmi tarehe 1 Juni 2020, baada ya kuchapishwa kwenye Gazeti la L’Osservatore Romano, toleo la tarehe 20 Mei 2020.

Kardinali Parolin
22 May 2020, 13:35