Tafuta

Vatican News
2020.04.26 Regina Coeli 2020.04.26 Regina Coeli  (Vatican Media)

Papa Francisko,Malkia wa Mbingu:Tukimwelekea Mungu maisha yanabadilika!

Ni lazima kumfunguli moyo Yesu,kumsikiliza wakati wa kusoma Injili,kumwaomba kwa kuwa ni katika Yeye inapatikana njia.Ndyo ushauri kutoka katika Tafakari ya Papa Francisko wakati wa Sala ya Malkia wa mbingu akiongozwa na Injili ya Luka inayosimulia safari ya mitume wawili kuelekea kijji cha Emau.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Injili ya siku inajiwakilisha katika siku ya Pasaka katika kusimulia juu ya mitume wawili katika njia ya Emau (Lk 24,13-35). Ni historia ambayo inaanza na kuishia katika safari. Kwa hakika katika safari ya kwenda ya mitume ambao walikuwa na huzuni kufuatia na tukio la Yesu, huku wao wakiacha Yerusalemu na kurudi nyumbani kwao Emau kwa kutembea kilometa 11. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko, Jumapili tarehe 26 Aprili 2020 ambayo ni Dominika ya III ya kipindi cha Pasaka. Papa Francisko akifafanua, anasema hii ni  safari ambayo inafanyika wakati wa mchana na sehemu kubwa ilikuwa ni mtelemko wa kutembea kilomita kumi na moja lakini pia hata safari ya kurudi kutoka kijiji hicho kwa maana ya kilomita sawa za kwanza kwa jitihada za usiku nzima kutembea na kurudi tena Yerusalemu.

Safari ya mchana na usiku

Safari mbili, moja iliyokuwa rahisi wakati wa mchana na nyingine ya kuchoka ya usiku. Lakini  safari ya kwanza ilifanyika kwa huzuni na ya pili kwa furaha. Ya kwanza kulikuwa na Bwana aliyekuwa anatembea nao karibu, lakini bila kumtambua: ya pili hawakumwona tena, japokuwa walihisi ukaribu wake. Kwanza walikuwa wamekata tamaa na bila matumaini; ya pili walikimbia ili kupeleka habari njema ya kukutana na Yesu Mfufuka. Safari zote mbili tofauti za mitume wa kwanza zinaeleza  hata kwetu jambo sisi ambao ni mitume wa Yesu leo hii ya kwamba katika maisha tunayo mielekeo miwili tofauti. Kuna njia ya wale ambao, kama wale wawili waliokuwa wanakwenda kwa mguu wakiwa kama wamepooza na kukata tamaa za maisha lakini wakiendelea  mbele tu na masikitiko; na kuna njia ya wale ambao hawajiweki mbele wenyewe na shida zao, bali wanasubiri Yesu anayetutembelea na ndugu ambao wanangojea ziara yake, yaani ni kusema, ndugu wanaotusubiri tuwajali, Papa Francisko amebainisha.

Mapinduzi ya kuacha kujikunjia katika ubinafsi

Hapa kunahitajika mapinduzi ya  kuacha kujikunjia binafsi, na  kukata tamaa za zamani, juu ya mawazo ya kutoweza kutimilika na mambo mabaya mengi ambayo yametokea katika maisha yako. Lakini papa Fracisko anabainisha kuwa ni mara nyingi tunachukuliwa kuzungukia ndani humo … kwa maana hiyo anashauri kuwa “Acha hayo na uendelee kutazama ukweli mkuu wa hali halisi ya  wa maisha: Yesu yu hai, Yesu na ananipenda. Huo ndiyo ukweli mkubwa zaidi, na naweza kufanya jambo lolote kwa wengine. Ni ukweli mzuri, ulio chanya, unaongaza kama jua na  mzuri! Kubadilisha njia ndiyo ina maana ya  kuhama kutoka mawazo yangu binafsi  hadi kufikia ukweli wa Mungu wangu. Kwa maneno mengine kutoka katika fikra za “ikiwa” hadi  kufikia “ndiyo”.

Tuache tabia ya “ikiwa” na kufuata “ndiyo”

Je inamaanisha nini? Papa anaorodhesha: “Kama ingekuwa Yeye ndiye aliyetuokoa, ikiwa Mungu angenisikiliza, ikiwa maisha yangeenda kama nilivyotaka, ikiwa ningekuwa na hili na  na lingine… yaani kuwa na mzungukio wa malalamiko tu. Papa Francisko amesema, na kuonegaza : Hii “ ikiwa” haisadii na wala hazai matunda, haisadii sisi na wala wengine. Tazama hizo, yaani  “ikiwa zetu, sawa na zile za  wanafunzi wawili”. Lakini wao waliweza kupitia ile “ndiyo”: “Ndiyo, Bwana yu hai, anatembea na sisi. Ndiyo, sasa, na siyo kesho, tumerudi  katika njia ya safari kwa ajili ya kumtangaza. Ndiyo, ninaweza kufanya hivyo ili kuwafanya watu wafurahi zaidi, kuwafanya watu kuwa bora, kusaidia watu wengi.   Inaamana ya kutoka “ikiwa” hadi “ndiyo”, kutoka kulalamika hadi kufikia furaha na amani, kwa sababu wakati tunalalamika, hatuna furaha; tuko kwenye mawingu weusi, katika hali ya hewa ya kijivu kwa huzuni. Na hiyo haitusaidii na hata kukua vizuri. Kutoka “ikiwa” hadi “ndiyo”, kutoka kulalamika hadi furaha ya huduma”.

Tunahitaji mabadiliko kutoka umimi kwenda kwa Mungu

Mabadiliko haya ya hatua, kutoka umimi  kwenda kwa Mungu, kutoka ikiwa na kwa ndiyo, kama ilivyowatokea wanafunzi? Kwa kukutana na Yesu. Kwanza hawa wawili wa Emau walimfungulia mioyo yao; wakamsikiliza  akielezea maandiko; kwa njia hiyo  wakamkaribisha nyumbani. Kuna hatua tatu ambazo tunaweza pia kutimizwa hata katika nyumba zetu: kwanza, kufungua mioyo kwa Yesu, kumkabidhi mizigo, kazi ugumu, kukata tamaa za maisha, kumkabidhi zile “ikiwa”; baadaye hatua ya pili, ni kumsikilize Yesu, na chukua Injili mkononi, kusoma  kifungu cha  leo hii, katika sura ya ishirini na nne ya Injili ya Luka; Tatu, kuomba Yesu, kwa maneno yaleyale kama yale wanafunzi: “ Kaa nasi Bwana”(Lk 24, 29). Kaa nami Bwana. Kaaa na sisi sote Bwana, kwa maana tunakuhitaji Wewe ili kupata njia. Bila Wewe kuna usiku.”

Mama Maria kwa kupokea Neno atuonyeshe njia

Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema sisi tunakuwa njiani siku zote katika maisha. Na sisi huwa tunayoelekea. Tunachagua njia ya Mungu, na siyo ile ya ubinafsi; njia ya “ndiyo”, siyo ile ya “ikiwa”. Tutagundua kuwa hakuna kinasichotarajiwa, hakuna mpando, hakuna usiku ambao hauwezi kukabiliwa uso kwa uso na Yesu. Mama Maria Mama wa safari, ambaye kwa kukaribisha Neno alifanya maisha yake yote kuwa “Ndiyo tazama mimi” kwa Mungu, atuonyeshe njia.

26 April 2020, 13:42