Tafuta

Fra Giacomo Dalla Torre Fra Giacomo Dalla Torre  

Papa atuma salam za rambi kutokana na kifo cha Fra Giacomo Dalla Torre

Katika telegram Papa Francisko anazungumzia marehemu kwamba alikuwa na upendo kwa wenye shida na uaminifu wa Injili kiongozi huyo wa chama cha kitume cha Malta aliyeaga dunia mjini Roma tarehe 29 Aprili 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ametuma telegem ya salam za rambi rambi  kufuatia na kifo cha aliyekuwa amiri jeshi mkuu wa Chama Cha Kitume cha Kijeshi cha Malta (Smonm), Fra Giacomo Dalla Torre del Tempio di Sanguinetto kilichotokea mjini Roma tarehe 29 Aprili 2020. Telegram hiyo imetumwa kwa Padre Francesco  ambaye ni amiri jeshi mkuu wa mpito wa chama cha kitume cha kijeshi cha Malta na Fra’ Ruy Gonçalo Do Valle Peixoto de Villas Boas.

Katika telegram hiyo Papa anaonyesha masikitiko yake makubwa kufuatia na kifo cha amiri jeshi mkuu huyo na kwa maana hiyo anawapa salam za rambi rambi kwa chama cha kitume cha kijeshi. Aidha akielezea wasifu wa hayati huyo anasema alikuwa ni mwanaume thabiti wa utamaduni, imani na imara katika uaminifu wa Kristo na kwa Injili, ikiwa ni pamoja na ukarimu wa jitihada zake katika matendo hasa kwa roho ya huduma katika ofisi yake na kwa ajili ya wema wa Kanisa, ikiwa pia katika kujitoa za kwa walio maskini zaidi.

Kwa kushiriki pamoja sehemu ya uchungu huo, anainua sala zake kwa ajili yake na kuiombea roho yake kwa Mungu, mwenye wingi wa rehema na amani ya milele. Na kwa hisia hizo anawatuimia kwa moyo wote baraka ya kitume ili kuwatia moyo kiongozi huyo na kama ilivyo kwa familia yake inayoomboleza kwa ajili ya marehemu Fra Giacomo Dalla Torre.

Marehemu Fra Giacomo Dalla Torre alikuwa na miaka 75, ambapo ameuguwa kwa muda mfupi. Yeye alikuwa amechaguliwa kwa miaka miwili katika jimbo hilo baada ya kuongoza kwa mwaka mmoja mkuu wa chama cha kitume cha kijeshi cha Malta tangu Aprili 2017 hadi Mei 2018, kwa kuchukua jukumu kubwa katika wakati mgumu wa mgogoro kikatiba na ambao ulikuwa umesababisha hata mipasuko ya kina.

Tabia yake ya kuwa katika huduma ya chama  cha kitume hiki na kwa watu wenye shida ilikuwa mara nyingi inamfanya aonekane katika huduma kwa wasio kuwa na fursa, kwa mfano watu wasio kuwa na makazi, katika kituo vya treni cha Termini, jijini Roma, mahali ambapo yeye mwenyewe alikuwa anagawa chakula, au hata katika jitihada ya kushiriki kwenye hija mbali mbali zilizoandaliwa na  Chama Cha Kitume cha Kijeshi la Malta (Smom) na kama ilivyo ile ya kimataifa kwa ajili ya wagonjwa kwenda Lourdes,  au ile ya Italia ya kwenda Loreto na  Assisi.

 

30 April 2020, 09:45