Tafuta

Vatican News
Kardinali Timothy Dolan,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki jijini  New York aliadhimisha Misa ya Pasaka akiwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick peke yake Kardinali Timothy Dolan,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki jijini New York aliadhimisha Misa ya Pasaka akiwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick peke yake  (2020 Getty Images)

Marekani:Papa aombea nchi iliyo na maambukizi zaidi ya janga la corona!

Papa Francisko amempigia simu Kardinali Timothy Dolan,Askofu Mkuu wa New York,akionesha upendo wake,ukaribu na wasiwasi mkuu kwa ajili ya watu wote wa mji kwa namna ya pekee wagonjwa wa virusi vya corona.Ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Jimbo kuu la New York.Hata hivyo nchini Marekani ndiyo inaongoza zaidi kwa maambukizi ya virusi vya corona duniani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko katika kipindi hiki cha dharura ya afya ulimwenguni hakosi kamwe kuonyesha ukaribu wake kwa wale wote ambao duniani wanaendelea kuteseka kwa kila aina ya teso na zaidi hasa la virusi vya corona. Kufuatana na hilo tarehe 14 Aprili amempigia simu Kardinali Timothy Dolan, Askofu Mkuu wa New York, kuonesha ukaribu wake na wasiwasi wake kuhusu maendeleo ya kusambaa sana kwa janga la virusi vya corona Nchini Marekani na kwa namna ya pekee katika mji wa New York.

Habari hizi zimethibitishwa na Jimbo Kuu tarehe 14 Aprili  na Kardinali mwenyewe Dolan, kwani inasomeka: “Baba Mtakatifu Francisko  ameniita mchana wa leo saa 8.00 kamili ili kuonyesa upendo wake, wasiwasi na ukaribu wake kwa watu wote wa New York, kwa namna ya pekee wale ambao ni wagonjwa wa janga la virusi vya corona”

Kardinali Dolan, aidha amesema kuwa Baba Mtakatifu anasali kwa ajili ya wagonjwa, madkari, wauguzi na wahudumu wa afya ambao wanajikita katika kutibu wale wote ambao wameshambuliwa na virusi, lakini pia hata kwa ajili ya viongozi wa raia, ikiwa ni pamoja na makuhani, watawa na walei. Kwa mujibu wa Kardinali anamshukuru sana Papa Francisko kwa ishara ya upendo huo na kumwakikishia sala kutoka kwa watu wa Newe York,  yeye ninafsi na kwa ajili ya huduma yake ya kichungaji.

Hata hivyo Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa amesema kuwa muda mrefu Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa shirika la afya duniani (Who)na kwamba anayo matumaini kuendelea kuwa hivyo. Akizungumza na waandishi wa Habari tarehe 15 Aprili 2020 kwa njia ya video mjini Geneva Uswis baada ya Rais wa Marekani kutangaza jana Jumanne 13 Aprili kwamba inasitisha msaada kwa shirika hilo, Dk. Tedros Adhamon Ghebreyesus amesema “Tunasikitika kwa uamuzi wa rais wa Marekani kutoa amri ya kusitisha ufadhili kwa shirika la afya duniani. Kwa msaada wa watu na serikali ya Marekani, Who inafanyakazi kuboresha afya ya watu wengi masikini na wasiojiweza duniani.”

16 April 2020, 12:45