Tafuta

Licha ya uwanja kuwa mweupe bila watu siku ya Jumapili 22 Machi 2020, Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana alichungulia dirishani na kubariki Roma na ulimwengu! Licha ya uwanja kuwa mweupe bila watu siku ya Jumapili 22 Machi 2020, Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana alichungulia dirishani na kubariki Roma na ulimwengu! 

Virusi vya Corona,COVID-19:Papa Francisko anasema tuinue maombi ya ulimwengu!

Itakuwa ni kusali sala ya Baba Yetu Jumatano tarehe 25 Machi 2020 kwa wakristo wa madhehebu yote na sala nyingine siku ya Ijumaa tarehe 27 Machi 2020 saa 12 jioni katika uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo kutakuwa na kuabudu Ekaristi Takatifu na Baraka ya Urbi et Orbi.Kipofu alipata kuona kwa macho yake na baadaye akawa na imani katika Yesu.Yote hayo ni kwa njia ya mchakato wa safari na ingekuwa vizuri leo hii kusoma Injili ya Yohane.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko katika kutafakari neno la Mungu kwa kuongozwa na Injili ya siku iliyokuwa inaelezea mtu aliyezaliwa kipofu, tarehe 22 Machi 2020 akiwa katika chumba cha vitabu kwenye jengo la kitume na kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, amesisitiza ni jinsi gani Yesu anatenda shughuli yake kwa kuangazwa  na ngazi mbili. Mojo ikitazama kimwili na nyingine ya kiroho. Kipofu alipata kuona kwa macho yake na baadaye akawa na imani katika Yesu. Yote hayo ni kwa njia ya mchakato wa safari, Papa Francisko amesema na kuongeza kuwa, “ingekuwa vizuri leo hii kusoma sehemu hiyo ya Injili ya Yohane. Matendo mema anayotimiza siyo ishara ya kushangilia lakini lengo lake ni kuwafikisha katika imani kwa njia ya safari ya mabadiliko ya kiundani”

Kwa mwanga wa imani, aliyekuwa kipofu anajigundua utambulisho wake mpya, ni kiumbe mpya mwenye uwezo wa kuona tena mwanga wa maisha yake na ulimwengu unaomzunguka kwa sababu ameingia katika muungano na Kristo. Njia yake ya mwanga ni mfano wa mchakato wa hatua ya kujikomboa dhidi ya dhambi ambayo sisi sote tunaalikwa  kujikomboa.

Dhambi ni kama kitambaa cheusi kinachofunika nyuso zetu na kutuzuia kujitazama kwa dhati sisi binafsi na dunia”, amesema Papa na kuongeza, “msamaha wa Bwana unaondoa kivuli na giza hili na kutupatia mwanga mpya. Kwaresima tunayoiishi iwe kipindi muafaka na chenye thamani ya kumkaribia Bwana, kwa kuomba huruma yake katika kila mtindo unaopendekezwa na Mama Kanisa”. Kila mbatizwa anaalikwa kupokea mwanga wa Mungu na kuuonyesha katika maisha yake yote binafsi. Mbegu ya maisha mapya iliyopandwa kwetu wakati wa ubatizo ni kama cheche ya moto ambayo inatakasa awali ya yote sisi, kwa kuchoma ubaya ambao humo ndani mwetu na kutuhurumia, kumelemeta na kungaza.

Papa Francisko aidha hakukosa kuzungumza juu ya dharura ya virusi vya corona kwa kutoa pendekezo na kusema: “ili kuweza kuunganisha sauti juu mbinguni kwa wakristo wote ninawaalika viongozi wote wa Makanisa na viongozi wa jumuiya zote za kikristo kwa pamoja na wakristo wa madhehebu  mbalimbali kumwomba Mwenyezi Mungu aliye juu, kwa kusali wakati mmoja kwa sala ambayo Bwana wetu Yesu alitufundisha. Ninawaalika kusali sala ya Baba Yesu siku ya Jumatano tarehe 25 Machi saa 6.00 mchana. Ni siku ambayo wakristo wengi wanakumbuka  upashanaji wa habari kwake Bikira Maria kwa Neno aliyefanyika Mwili, ili aweze kusikiliza maombi ya pamoja na wafuasi wake wote ambao wanajiandaa kuadhimisha ushindi wa Kristo Mfufuka.

Vile vile  Papa Francisko ametangaza kuwa Ijumaa tarehe 27 Machi saa 12 Jioni masaa ya Ulaya atafanya maombi katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Papa amesema: “Tangu sasa ninawaalikeni nyote kushiriki kiroho kwa njia ya vyombo vya mawasiliano. Tutasikiliza Neno la Mungu, tutainua maombi yetu, tutaabudu Ekaristi Takatifu, ambapo hatimaye ninatoa Barala ya Urbi et Orbi na kutakuwapo na uwezekano wa kupokea msamaha wa dhambi ( Undulgenzia plenaria).

“Katika mlipuko wa virusi tunataka kujibu kwa pamoja katika ulimwengu wa sala, wa huruma na upole. Tubaki tumeungana. Tuwafanye wahisi ukaribu wetu watu walio peke yao na waliojaribiwa zaidi, madaktari, wauguzi, watu wa kujitolea, viongozi ambao wanapaswa kuchukua hatua ngumu kwa ajili ya wema wetu, polisi, wanajeshi na watu wote”. Kama kawaida ya Papa Francisko alivyofanya  Jumapili iliyopita mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana amechugulia hata katika dirisha linalotazama uwanja wa Mtakatifu Petro ambao na amebariki Roma na ulimwengu mzima.

23 March 2020, 11:00