Tafuta

Vatican News
Sala ya Malaika wa Bwana Jumapili 22 Machi 2020 Sala ya Malaika wa Bwana Jumapili 22 Machi 2020 

Papa Francisko atatoa msamaha wa dhambi tarehe 27 Machi!

Kutoka kwa msemaji wa vyombo vya habari amekumbusha uwezekano kwa wale wote watakao shiriki sala na maombi na Papa Francisko katika sala siku ya Ijumaa 27 Machi 2020 kwa ajili ya kupata rehema kamili kwa kufuata vigezo vilivyotolewa na kanuni ya Idara ya Kitume ya Toba.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Msemaji wa Mkuu wa Vyombo vya habari Vatican ametoa taarifa kuhusu tukio la tarehe 27 Machi 2020 saa 12 Jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati Papa Francisko katika kipindi hiki cha dharura kwa ajili ya ubinadamu, atawaalika wakatoliki wote diniani kuungana kiroho katika maombi na yeye.

Kufuatia na tukio hili kwa mujibu wa Msemaji wa vyombo vya habari Vatican anathibitisha itawezekana kufuatiliwa moja kwa moja kupitia vyombo vya mawasiliano Vatican ambapo Papa Francisko anahitimisha tukio hilo kwa kutoa rehema kamili na kwa kutoa Baraka ya Ekaristi Takatifu kwa Urb et Orbi.

23 March 2020, 10:20