Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amesali sala ya Baba Yetu saa sita kamili masaa ya Ulaya. Papa Francisko amesali sala ya Baba Yetu saa sita kamili masaa ya Ulaya.  (Vatican Media)

Papa Francisko amesali sala ya Baba Yetu na kuomba huruma kwa ajili ya ubinadamu uliojaribiwa!

Saa sita kamili wakristo wote duniani wameungana na Papa Francisko ili kusali pamoja.Maombi ya Papa kwa ajili ya wagonjwa,familia zao,wahudumu wa afya na vyombo vya utekelezaji na wahudumu wa kichungaji wa Jumuiya zetu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ilikuwa ni saa sita kamili masaa ya Ulaya ambapo Papa Francisko kama alivyokuwa ameomba ulimwengu mzima kuungana naye katika maombi kwa Mungu ili asitishe mlipuko wa virusi ameanza kusema kuwa: Wapendwa kaka na dada, leo tumepeana muda wa kukutana wakristo wote ulimwenguni kwa ajili ya kusali kwa pamoja sala ya Baba Yetu, sala ambayo Yesu alitufundisha. Kama watoto wenye imani tumwelekee Baba. Tufanye kila siku na mara nyingi kwa siku; lakini katika muda huu tunataka kuomba huruma kwa ajili ya binadamu wakati wa majaribu ya mlipuko wa virusi vya corona. Na tunafanya kwa pamoja, wakristo wa kila Kanisa na Jumuiya, kwa kila umri, lugha, mataifa na kila tamaduni.

Aidha Papa Francisko ameongeza kusema kuwa: Tuwaombee wagonjwa na familia zao: kwa ajili ya wahudumu wa afya na wale wote ambao wanawasaidia; kwa wenye mamlaka; vyombo vya utekelezaji wa sheria na watu wa kujitole na  kwa ajili ya wahudumu wa kichungaji wa Jumuiya zetu.

Leo hiii watu wengi wanaadhimisha Neno aliyefanyika Mungu katika umbu la Bikira Maria aliyeitikia“TAZAMA MIMI HAPA” , kwa unyenyevu wote, anaangazia ile “tazama mimi ya Mwana wa Mungu.  Kwa maana hiyo hata sisi tumkabidhi kwa imani kuu katika mikono ya Mungu na katika moyo mmoja na kwa pamoja tuombe.

Katika Sala ya Baba yetu  ametumia lugha ya kilatino na kusema: Pater noster, qui es in cælis: sanctificétur Nomen Tuum: advéniat Regnum Tuum: fiat volúntas Tua, sicut in cælo, et in terra. Panem nostrum cotidiánum da nobis hódie, et dimítte nobis débita nostra, sicut et nos dimíttimus debitóribus nostris. et ne nos indúcas in tentatiónem; sed líbera nos a Malo. Amen.

Kwa lugha ya Kiswahili ni kama ifutavyo: Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike dunian kama huko mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe wale waliotukosea usitutie katika vishawishi lakini utuopoe maovuni. Amina.

SALA PAPA
25 March 2020, 12:30