Tafuta

Vatican News
Tarehe 25 Juni 2015 Papa Francisko alikutana na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Kikanisa Tarehe 25 Juni 2015 Papa Francisko alikutana na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Kikanisa  

Papa:Yatakiwa mwaka 1 wa utume kwa wanadiplomasia wapya wa Vatican!

Barua ya Papa Francisko kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Kanisa kwa ajili ya yoyote ambaye anaingia kuanza mafunzo kwa ajili ya kutoa huduma ya kidiplomasia anatakiwa awe amefanya uzoefu wa umisionari kwa mwaka mmoja katika jimbo lolote la ulimwenguni.

VATICAN

Alikuwa ametangaza hilo katika hotuba yake ya mwisho wakati wa Sinodi ya Amazonia na sasa ni utekelezaji. Papa Francisko amemwandikia barua Monsinyo Joseph Marino, mwenyekiti mpya wa Taasisi ya  Kipapa ya Elimu ya Kakanisa, ambayo ni shule ya  Mafunzo kwa makuhani wanaojiandalia na shughuli za Kidiplomasia Vatican, akiomba kuwa katika curriculum Vitae (CV) lazima ioneshwe uzoefu wa kimisionari wa mwaka mzima katika Kanisa mahalia. Katika  Barua ya Papa Francisko inayooneshwa kuandikwa tarehe 11 Februari,  anakumbuka utashi ambao Mapade wanaojiandaa katika Huduma ya kidiplomasia kwa ajili ya Vatican kwanza wajikite kwa mwaka mzima katika mafunzo yao kwenye kitihada za kimisionari katika majimbo. Papa anasema “ninaamini kwamba uzoefu huo inaweza kuwa na manufaa kwa vijana wote ambao wanajiandaa au nawaanza huduma ya kikuhani, lakini kwa namna ya pekee wale ambao wanataweza kwa namna kuweza kutumwa na Vatican katika mataifa na Makanisa maalumu”.

Papa Francisko anataja kutokana na suala hili yale ambayo aliyatamka wakati wa hotuba yake kwa Taasisi ya Kipapa ya elimu ya Kanisa kunako mwaka 2015, aliwambia: “Utume ambao mtakuwa siku moja mmetumwa kujikita nao, utawaepeleka katika pande zote duniani. Ulaya kunahitajika kuwepo na  mwamao; Afrika wanakiu ya upatanisho; Amerika Kusini wana njaa ya kumwilishwa kiundani; Amerika ya Kaskazini inahitaji kugundua kwa upya mile izizi ya utambulisho ambao hauzi na ubaguzi; Asia na Australia, changamoto  za uwezekano wa kutoa chachu ya kidiaspora na majadiliano mapana ya utamaduni wa mila za kizamani. Katika barua pia anaongeza kusema kuwa “ ili kukabiliana kwa uchanya kuhusu kuongezeka kwa changamoto za Kanisa na duniani, inahitajika kuwa na wanadipolasia endelevu wa Vatican ambao wamefanya uzoefu wa kweli zaidi ya mafunzo ya kawaida ya kikuhani- kichungaji na yale maalum yanayotolewa na Taasisi ya Elimu, lakini pia hata uzoefu binafsi wa kimisionari nje ya jimbo lake binafsi kwa kushirikishana.

Papa kwa namna hiyo katika barua yake amemwelekea Monsinyo Marino akimwomba“ kusikiliza kwa  matendo ile shauku yake ambayo inajumuishwa kwenye curriculum Vitae (CV) ya mafunzo kwa ajili ya shughuli za mwaka mzima katika  huduma ya kisimisionari kwenye makanisa maaalum yaliyoenea ulimwenguni kote. Uzoefu huo unaanza moja kwa moja kuanzia na wanafunzi ambao wataanza mwaka wa masomo 2020/2021.

Ili kufikia lengo kwa namna ya kina ya mpango huo, Papa Francisko anaandika kuwa “ inatakiwa awali ya yote kuwa na ushirikiano wa dhati na ofisi ya Katibu Mkuu wa Vatican na zaidi katika kitengo binafsi cha nafasi ya Kidiplomasia, Vatican (kitengo cha tatu cha uhusiano na ushirikiano wa nchi za nje) na zaidi kwa wawakilishi wa Kipapa ambao kwa hakika hawatakosa kutoa msaada maalum kwa kila Kanisa mahalia  ambao wako tayari kupokea wanafunzi na ili kuweza kufuatilia kwa ukaribu uzoefu wao”.

Kwa kuhitimisha Papa anandika kuwa “nina uhakika kwamba ili kuondoa wasiwasi wa kwanza, ambao unaweza kujitokeza mbele ya mtindo mpya wa mafunzo kwa wanadiplomasia wapya wakati ujao wa Vatican,  uzoefu wa kimisionari ambao unapaswa kuhamasishwa utarudia kuwa muhimu na siyo tu kwa vijana wanafunzi wa kidiplomasia , lakini pia hata kwa makanisa mahalia ambao watashirikiana na ninawatakia kwamba izaliwe shauku kwa  makuhani wengine katika Kanisa la ulimwengu ili kuwezesha jukumu la kufanya kipindi cha huduma ya utume wa kimisionari nje ya jimbo lake binafsi."

17 February 2020, 16:52