Tafuta

Licha ya matatizo ambayo yaweza kujitokeza katika maandalizi lakini matukio ya maonyesho kimataifa yana uwezo wa kuunda mitandao mizuri ya uhusiano kibinadamu na uwezo wa kudumu zaidi ya tukio lenyewe. Licha ya matatizo ambayo yaweza kujitokeza katika maandalizi lakini matukio ya maonyesho kimataifa yana uwezo wa kuunda mitandao mizuri ya uhusiano kibinadamu na uwezo wa kudumu zaidi ya tukio lenyewe. 

Papa:Maonyesho yanaweza kuonesha uzuri wa tamaduni!

Papa Francisko akikutana mjini Vatican tarehe 6 Februari 2020 na washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Maonyesho Kimataifa,amesema wao wanaweza kweli kujivunia shughuli zao hasa zinazounda utambuzi wa kuwa na msimamo wa huduma kwa ajili ya ustawi wa pamoja na maendeleo fungamani.Maonyesho ya kimataifa,yanachangia kukuza utamaduni wa makutano na kukuza uhusiano wa mshikamano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe 6 Februari 2020 amekutana na washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Maonyesho Kimataifa (UFI) wakiwa katika fursa ya Mkutano wao Kimataifa. uliofanyika mjini Roma, mji wa imani na utamaduni, mahali pa kukutana na watu na mawazo kwa karne nyingi anasema Papa. Kama kiongozi katika tasnia ya haki ya biashara na maonyesho makubwa ya biashara, wamekuja roma, si tu kama wataalam wa mashirika, lakini kwa sababu kupitia kazi yao wanatafuta kuchangia uchumi wa ulimwengu ili uwe wa haki na wa kibinadamu. Dunia yetu inakaribiana zaidi na kwa taratibu tunakuwa na utambuzi wa mantiki tofauti za maisha yetu na shughuli zetu zikiwemo zile za kijamii, kiutamaduni na kiekolojia na ambazo zinaunganika kati yao. (taz. Laudato si’, 137).

Muungano huo imesababisha makampuni, taasisi zenye kazi ya mazingira, kijamiii na watawala ambao wanaweza kuongeza na kutathimini shughuli za kiuchumi na kibiashara. Katika muktadha wa nyanja yao ya kitaaluma imetambulika kuwa maonyesho yao siyo kuwa na athari chanya tu kwenye uchumi wa kikanda na masoko ya kazi, lakini pia hata kutoa fursa muhimu za kuonyesha utofauti mkubwa na uzuri wa tamaduni kienyeji na mifumo ya ekolojia kwa ulimwengu wote. Kwa namna ya pekee katika maonyesho ya kimataifa, yanachangia kukuza utamaduni wa makutano na kukuza uhusiano wa mshikamano, kuchangia kukuza utajiri wa pamoja kati ya wajumbe wa familia moja.

Aidha Papa Francisko anasema kazi yao kwa hakika ina ukuu unaojitambulisha. Kama huduma ya ustawi wa wote  ni lazima iunganishwe, itunze nyumba ya pamoja na maendeleo fungamani ya kila mtu na watu. Wasiwasi huo wa kimaadili si tu katika kuuweka pembezoni, lakini ni muhimu katika kujenga uchumi ambapo mapato ya fedha siyo tofauti tu ya kupima mafanikio. Uzoefu wao aihdha umewafundisha kwamba katika kuandaa na kutimiza maonyesho, mambo muhimu ya ujenzi lazima yachangie kwa usawa, kutoka kwa watendaji wa binadamu hadi kufikia vifaa vya ujenzi na taa, mimea na usimamizi wa taka. Ushirikiano mkubwa katika ngazi ya kawaida na ya kimataifa, nafasi zaidi za kufaulu, kiuchumi na kwa kibinadamu vinahitajika sana Papa Francisko amesisitiza.

Maonyesho ambayo yanaunga mkono uchumi wa ndani, yanajumuisha nguvu kazi yake, yanatoa thamani na umuhimu kwa tamaduni zake na kuheshimu kabisa mazingira yake ya kibinadamu na mazingira kwa ujumla, na hatimaye wao watakuwa na mafanikio zaidi na mashuhuri. Watakuwa na athari chanya na kivutio cha ndani na kimataifa. Kwa asili kuanza nafasi ya kazi  kwa ngazi ya juu inahitaji kuwa na mtandao wa hali ya juu wa wahudumu wanahitajika waandaaji, wakuu wa serikali mahalia, wafanyakazi, viwanda vya biashara, mashirika ya raia, na mengine.

Licha ya matatizo ambayo yanaweza kuzuka katika mchakato wa maandalizi na kutimiza maonyesho ambayo yanaingia katika taaluma yao msingi, matukio haya yana uwezo wa kuunda mitandao mizuri ya uhusiano kibinadamu anasisitiza Papa, uwezo wa kudumu zaidi ya tukio lenyewe. Kwa upande wao wanapaswa kujivunia anasema Papa katika kuzalisha shughuli hizo na mshikamano wa utambuzi wa huduma ambayo lengo ni kwa ajili ya ustawi wa pamoja na maendeleo fungamani. Amehimitimsha kwa kuwatakia jitihada njima na hili hatimaye kwa kujitolea kwao ili waweze kukuza ubunifu na uvumbuzi katika sekta yao. Amewabariki kila mmoja wao na familia zao, anawaomba pia wasali kwa ajili yake.

06 February 2020, 15:08