Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amebainisha kwamba chumvi ina maana ya yule mfuasi wa Yesu licha ya kuanguka au kushindwa kila siku,lakini anaamka na kuanza kila mara kwa uvumilivu akitafuta majadiliano na mkutano. Papa Francisko amebainisha kwamba chumvi ina maana ya yule mfuasi wa Yesu licha ya kuanguka au kushindwa kila siku,lakini anaamka na kuanza kila mara kwa uvumilivu akitafuta majadiliano na mkutano. 

Papa:Kanisa siyo kizuizi:hutumika kuhudumia maskini

Mbele ya kunyanya,kutumia nguvu,ukosefu wa haki na msongo,Kanisa haliwezi kujifungia binafsi,bali lazima liwe kama jumuiya ya kutoa huduma kwa wote walio wa mwisho.Ni ushauri wa Papa Francisko aliotoa akifafanua juu ya zoezi la mkristo la kushinda dhambi,kutochafua maadili,kuondoa giza ili nuru ya Kristo iweze kuangaza.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Chumvi na mwanga ni vitu viwili vyenye ishara pia mantiki mbili na  tabia mbili za kweli ambazo Yesu anawakabidhi wafuasi na wale wote wenye nia ya kutaka kumfuasa ili kuwa mashuhuda wa kweli wa kutangaza  Injili. Papa ametoa mwaliko kwa wote wakati wa tafakari ya Injili kabla ya sala ya Malaika wa Bwana Jumapili  tarehe 9 Februari 2020. Pia ametoa tamko la nguvu kwa ajili nchi ya Siria na juu ya Siku ya maombi duniani kwa ajili ya kupinga biashara ya binadamu na utumwa inayoadhimishwa kila tarehe 8 Februari ya kila mwaka.

Pinga dhambi na udhalilishaji

Chumvi ni nzuri na utoa radha na pia uhifadhi vyakula visiharibike. Wafuasi wa Yesu kwa maana hiyo wanaalikwa kuweka mbali wadudu waharibifu na ambao ni hatari wa kijamii wanaopenda kuchafua  na kudhalilisha maisha ya watu. Hii inatakiwa kuwa na msimamo dhidi ya uharibifu wa kimaadili, kupinga dhambi kwa kushuhudia zile thamani za ukarimu na uaminifu bila kuangukia kwenye udanganyifu wa kidunia kama vile ya kujiweka kimbele mbele na kupenda madaraka na utajiri. Papa Francisko amebainisha kwamba chumvi ina maana ya yule mfuasi wa Yesu licha ya kuanguka au kushindwa kila siku,lakini anaamka na kuanza kila mara kwa uvumilivu akitafuta majadiliano na mkutano. Aidha amesema chumvi ni yule hasiyetamani sifa, bali ni mwaminifu katika mafundisho ya Kristo ambaye hakuja kwa ajili ya kuhudumiwa bali  kuhudumia, anajibidisha kuwa mnyenyekevu na mjenzi.

Mwanga ni tabia ya mkristo kwa mfano wa Yesu

Kuwa mwanga ndiyo tabia ya kikristo, kwa mfano wa Yesu wa kuondoa giza ambalo bado linatawala duniani na mioyoni mwa watu wengi, Papa amesema. Ni mwangaza ambao unapaswa kuonekana katika  matendo zaidi ya maneno na ambao utambue zaidi kuelekeza mwingine ili afanye uzoefu wa wema wa huruma ya Kristo. Mfuasi wa Yesu ni mwanga anapotambua kuuishi kwa imani, nje ya nafasi zilizo finyu, anapotambua kuchangia na kuondoa hukumu, masengenyo na kufanya uingie mwanga wa ukweli katika hali tofauti zilizojaa unafiki na ulaghai.

Hakuna haja ya kuogopa kuishi katika dunia hata kama imejaa migogoro na dhambi

Papa akiendelea na ufafanuzi wa tafakari anasema, hakuna haja ya kuwa na hofu ya kuishi katika ulimwengu hata kama wakati mwingine ni kuonesha hali za migogoro na dhambi, lakini ni lazima  kuwa chombo cha Yesu ili mwanga uweze kuwafikia wote. Mbele ya vurugu,ukosefu wa haki na mikandamizo, mkristo hasijifungie binafsi au kujificha katika usalama wake binafsi; vile vile hata Kanisa haliwezi kujifungia binafsi, haliwezi kuacha utume wake wa kuinjilisha na huduma.

Yesu wakati wa Karamu Kuu alimwomba Baba yake wafuasi wake walindwe dhidi ya roho za dunia

Yesu wakati wa karamu kuu alimwomba Baba yake asiowaondoe  wafuasi wake katika dunia hii, bali  wabaki ndani ya ulimwengu japokuwa  awalinde dhidi ya roho ya dunia hii. Kanisa kwa maana hiyo linajikita ndani mwake na huduma yake ya ukarimu na huruma kwa ajili ya wote walio wadhaifu na maskini. Hii siyo roho ya dunia, bali  huo ni mwanga na chumvi yake, anamesisitiza Papa.Kanisa  linasikia kilio cha walio wa mwisho na kubaguliwa,kwa maana linatambua kuwa jumuiya moja inayoalikwa kuendelea kwa muda mrefu katika historia ya wokovu wa ulimwengu.

10 February 2020, 09:53