Tafuta

Vatican News
Kongamano la walei  jijini  Madridi nchini Hispania kuanzia tarehe 14-16 Februari 2020 Kongamano la walei jijini Madridi nchini Hispania kuanzia tarehe 14-16 Februari 2020 

Papa Francisko:Walei enendeni kukutana na kusikiliza mioyo ya watu!

Papa Francisko ametuma Ujumbe wake kwa Kardinali Blàszquez Pérez,Rais wa Baraza la maaskofu nchini Hispania kufuatia na fursa ya Kongamano la Kitafa la Kilei huko Madrid hadi 16 Februari 2020 wakiongozwa na mada “watu wa Mungu wanaotoka nje”.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Neno hai la Mungu linahitaji kutangazwa kwa shauku na furaha kwa njia ya ushuhuda wa kikristo ili kuweza kupambana dhidi ya kuta zilizo juu zaidi ambazo zinazotengenisha na kubagua. Ni katika ujumbe wa Papa Francisko aliowatumia watu wa Mungu,walei  wa nchi ya Uhispania na kwamba wasiwe na hofu ya kukanyaga njia na kuingia kila kona ya jamii ili kufika hadi kikomo cha mji na kugusa majeraha ya watu wetu. Ujumbe huo umeelekezwa kwa Kardinali Blàszquez Pérez, Rais wa Baraza la maaskofu nchini Hispania katika fursa ya Kongamano la Kitafa la Kilei  la sikìu tatu huko Madrid hadi 16 Februari 2020 wakiongozwa na mada “watu wa Mungu wanaotoka nje” ikiwa ni  hatua mwisho wa safari ya miaka minne ya mpango wa kichungaji iliyoanza mwaka 2016.

Ni safari ndefu ya maadalizi ambapo Papa Francisko anakumbusha uzuri wa kushirikishana mawazo na uzoefu , kuanzia na hali  halisi na tofauti, mahali ambamo walei wanaishi na hatimaye kutajirisha na kufanya jumuiya ikue mahali ambamo wao wanaishi. Papa Francisko anasema “nendeni na kutangaza Injili” na ndiyo matashi mema kwa walei na kuwati moyo ili waishi wito wao kwa kujikita ndani ya ulimwengu na kwa kusikiliza Mungu na Kanisa yale mapigo ya mioyo ya  wa watu wao.

Aidha anawaalika walei waepuke vishawishi vya ukikuhani kukuhani, vya kimashindano na kikazi kazi, vya ugumu na kuwa hasi. Kanisa la Mungu linajufunga kibwewe ili kwenda kukutana na mwingine bila kumhukumu, bila kumlaani, lakini kwa kumfungulia mikono ili kumsaidia na kumtia moyo na ujasiri au kwa urahisi kumsindikiza katika maisha yake, amesisitiza Papa. Kwa kufanya hivyo na kuishi kwa uthabiti wa zawadi ya ubatizo ni msingi kuwa na dhamiri ya kuwa “sisi sote tunafanya kuwa sehemu ya jumuiya moja ya kikristo”.

Sisi siyo kikundi cha aina fulani na wala kuwa shirika lisilo la kiserikali  anasema Papa na kuongeza kuwa sisi ni familia ya Mungu ambayo kwa pamoja inamzunguka Bwana. Katika siku ambayo Kanisa linawakumbuka watakatifu Cirily na Methodius, wasimamizi wa Ulaya, Papa anasema “ kutumwa kwa wamisionari, daima ni wa sasa na unarudia kwetu kwa nguvu ile ule daima ya kufanya isikike sauti ya Injili mpya katika dunia ambamo tunaishi , kwa namna ya pekee katika Ulaya ya zamani, mahali ambamo Habari Njema inaonekana kusongwa na sauti nyingi za vifo na mahangaiko”.

 

14 February 2020, 15:32