Tafuta

Vatican News
Papa amaekutana  na wakuu wa Polisi na viongozi wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican tarehe 8 Februari 2020 Papa amaekutana na wakuu wa Polisi na viongozi wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican tarehe 8 Februari 2020  (Vatican Media)

Papa Francisko:Jitihada zenu hazikosi hatari na ziongozwe na imani!

Katika mkutano wa Papa na wakuu wa Polisi na viongozi wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican anaelezea shukrani na utambuzi wa dhati wa huduma yao ya kila siku isiyo na kifani.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican

Tarehe 8  Februari 2020 Papa Francisko Francisko amekutana na vikosi vya Polisi na viongozi wengine wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican. Wakati wa hotuba yake amewashukuru kwa fursa hiyo ambayo ni ya utamaduni na kwamba inampatia fursa ya kuweza kutoa shukrani zake kwao katika  huduma yao  wanayoitoa katika Makao Makuu ya Kitume na mjini Vatican. Kwa namna ya pekee ameshukuru hotuba ya Mkuu wa Polisi aliyosoma kwa niaba ya wote na kumpa heri nyingi na zaidi  wito wa thamani ya uthabiti. Mungu awasaidia kwa ajili hiyo!

Kwa mara nyingine tena Papa Francisko anawapongeza na kuwatakia kazi njema yenye thamani. Mwaka 2020 tayari umeshaanza lakini bado anawatakia kuwa mwaka uwe mwema ambao Bwana amejalia ili uweze kuwa kipindi cha utulivu, amani kwa ajili yao na familia zao. Huduma yao katika mji wa Vatican ni yenye thamani kuu na isiyo na kifani.  Papa anasema kuwa siyo rahisi kufikiria jinsi wanavyo fanya kazi kila siku na watalii na wahujaju ambao wanatembelea uwanja, Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na Jumba la Makumbusho Vatican au wanakuja kukutana na Papa. Katika hali nyingine tofauti, anasema wanaalikwa kuunganisha hata dharura na uwajibikaji wa kanuni za umma na utulivu wa maisha yanayozunguka mji wa Vatican na maeneo yote ya imani takatifu katoliki. 

Papa Francisko aidha amebainisha kwamba, kazi yao pia ni muhimu wakati wa matukio ya ziara zake za kichungaji mjini Roma na Italia  na kila mahalia ambapo zoezi la huduma  inampeleka. Anathibitisha kuona kila wakati yeye mwenyewe umakini uliopo na wa dhati wa kazi yao. Papa anaongeza: “napenda kusisitia: busara; na ufanisi, umakini. Lakini ni busara. Na hii inafafanua  juu ya ukuu wa mwanadamu. Na kwa hili, asante sana”. Kazi yao zaidi ya ustadi na taaluma, inaonyesha upendo wa dhati na mshikamano kwa uaminifu wa Makao ya kitume. Zaidi ya kazi yao wanayofanywa na yenye kupongezwa, Papa anashukuru sana; katika fursa hiyo amependa kupyaisha tena kwa roho moja. Ushirikiano wa kila wakati na Vikosi vya ulinzi na usalama vingine vya Vatican ambavyo vinasaidia  kuwa kazi ya dhati na ya kupongezwa.

Mkutano wao huo na ambao karibu unafafana wa kifamilia, unageuka kuwa sehemu ya sala yake na matashi ya heri kwao. Katika mwanzo wa mwaka, anawakabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria na nia ambazo wanazo moyoni mwao, ili Bwana aweze kuzibariki  na kila shughuli yao, ya maisha yao yote, mawazo yao, mapendekezo na hata shauku zao. Mama Maria alinde kwa namna ya pekee watoto wao, wazee wao na kuwasaidia rafiki zao ambao wanaishi katika kipindi cha matatizo. Amepyasha heri nyingi na baraka katika jitihada za kila siku, ambazo mara nyingi ziko hatarini, lakini kwa kuongozwa na mwanga wa imani na matumaini na upendo. Mwanga wa unyenyekevu, urahisi lakini ulio mwema. Amewatuma wapeleke salam zake hata matashi mema kwa familia zao nyumbani . Amehitimisha kwa kuwapa Baraza za Bwana na amani .

 

08 February 2020, 15:24