Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ametoa sakrametni ya Ubatizo kwa watoto katika sherehe za Ubatizo wa Bwana  tarehe 12 Januari 2020 Papa Francisko ametoa sakrametni ya Ubatizo kwa watoto katika sherehe za Ubatizo wa Bwana tarehe 12 Januari 2020  (ANSA)

Ubatizo wa Bwana:msisahau kupeleka Roho Mtakatifu ndani ya roho za watoto!

Baba Mtakatifu Francisko wameongoza Ibada ya Misa takatifu na kutoa ubatizo kwa watoto wadogo 32 wakati wa Mama Kanisa anaadhimisha sherehe za Ubatizo wa Bwana Jumapili tarehe 12 Januari 2020 katika Kikanisa cha Sistina mjini Vatican.Wazo kuu la mahubiri ni nguvu ya roho Mtakatifu inayolinda,inayosindikiza na kusaidia watoto katika maisha yao yote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Katika sherehe za Ubatizo wa Bwana Jumapili tarehe 12 Januari 2020,  Papa Francisko ameongoza Misa Takatifu na kutoa ubatizo kwa watoto 32 katika Kikanisa cha Sistina mjini Vatican. Akianza mahubiri yake amesema kwamba “Kama Yesu alivyokwenda kuomba kubatizwa ndivyo hivyo nanyi mnaweza kuwapeleka watoto wenu. Yesu alimjibu Yohane: “acha itendeke kila haki (Mt 3,15). Papa ameongeza kusema, kubatiza mtoto ni tendo la haki kwa ajili yake. Je ni kwa  ababu gani? Kwa kujibu amesema, “Ni kwa sababu Sisi katika ubatizo tunampatia tunu, sisi katika ubatizo tunampatia kazi na mbayo ni Roho Mtakatifu. Mtoto anatoka katika ubatizo akiwa na nguvu ya Roho ndani. Na Roho Mtakatifu atamlinda, atamsaidia wakati wa maisha yake yote”.

Kuna umuhimu wa kuwabatiza watoto

Kuna umuhimu kuwabatiza watoto kwa sababu wanakua na nguvu ya Roho Mtakatifu amesema Papa na kusema  kwamba huo ndiyo ujumbe ambao ametaka kuwapatia leo hii. Wazazi wamewapeleka watoto wao ili waweze kuwa na Roho Mtakatifu ndani mwao. Na kuwawezesha kuwasaidia wakue na mwanga na nguvu ya Roho Mtakatifu, kwa njia ya katekisimu,kwa njia yakupta msaada kutoka kwa walimu na mifano halisi ambayo wazazi hao wataionesha ndani ya familia zao. Huo ndiyo ujumbe ambao  amewakabidhi wazazi  hao kwa kusisitiza zaidi!  Hata hiyo akiendelea Papa Francisko amesema, kutokana na nafasi waliyo kuwamo, hakutaka kuendelea zadi na mahubiri, bali  kuwataadharisha, kwamba, watoto hawajazoea kwenda Sistina. Ni  kwa mara yao ya kwanza! Hawajuhi kukaa mahali palipo fungwa na kidogo penye joto. Hawajazoea kuvalishwa jinsi walivyo na nguo za sikukuu nzuri kama hiyo. Kwa maana  halisi watoto hao watakosa utulivu ndani humo wakati wa misa.

Hata hivyo watoto ni kwaya nzuri

Kwa kuendeleza amesema katika hali hiyo akianza mmoja kulia, ni kwaya itaanza kwa wote! Lakini akianza mmoja na kufuatia mwingine, wao wasiogope sauti ya kulia kwa watoto. Na badala yake, mtoto akilia na kulalamika, labda ana joto, apunguzwe nguo mojawapo; au akiwa na njaa, basi anyonyeshwe hapo, kwani kuna amani daima”. Hili ni jambo ambalo Papa Francisko amekumbusha, alikuwa amesema hata mwaka jana na kwamba, watoto wanayo sifa kuu ya kutengeneza kwaya. Inatosha kuanza mmoja note ya ‘la’ na wote wakafuatia na kufanya kikundi cha kwaya moja. Kwa maana hiyo: “Msiogope”. Hayo ni mahubiri mazuri ya mtoto anapolia kanisani. Lakini fanyeni kwa namna ya kwamba mtoto anahisi na kujisikia vema ili kuendelea mbele na ibada". La muhimu Papa amehitimisha kukazia kuwa: "Msisahau:pelekeni Roho Mtakatifu ndani ya roho za watoto!

UBATIZO - PAPA
12 January 2020, 11:33