Tafuta

Vatican News
Tangu Septemba mwaka jana moto unazidi kurarua misitu na makazi ya watu nchini Australia. Papa Fracisko anasali kwa ajili yao! Tangu Septemba mwaka jana moto unazidi kurarua misitu na makazi ya watu nchini Australia. Papa Fracisko anasali kwa ajili yao!  (AFP or licensors)

Papa yuko karibu na watu wa Australia dhidi ya moto!

Papa Francisko ametoa wito kwa kikundi cha waamini wa Australia waliokuwa katika Katekesi kuhusiana na janga la moto linalozidi kurarua nchi hiyo. Ni zaidi ya hekari milioni 8 zimeraruliwa na moto tangu mwezi Septemba mwaka jana.Aidha Askofu Mkuu Coleridge amesema kazi kubwa imefanywa na serikali na watoa huduma ya kwanza.Ni mchango mkubwa pia uliotolewa na maparokia na mashirika mengine katoliki lakini bado hautoshi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Franciko tarehe 8 Januari 2020 wakati wa kuhitimisha tafakari ya Katekesi yake, akiwalenga kikundi cha waamini kutoka katika nchi ya Aistralia amesema akisema: "Ninaomba wote tusali kwa Bwana ili aweze kuwasaidia watu katika kipindi hiki kigumu cha moto wa nguvu. Niko karibu sana kiroho na watu wa Australia". 

Hata hivyo kufuatia na janga la moto unaoendelea kurarua nchi ya Australi, naye Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Australia Askofu Mkuu Mark Coleridge, ametoa wito kwamba pamoja na kilelezo cha mshikamano kuwa muhimu lakini hautoshi  mbele ya kupoteza maisha ya watu na hekari nyingi za ardhi kuraruliwa na moto, nyumba na miji kuharibika vilevile  moshi ambao umetanda sehemu kubwa ya nchi kuwaweka katika hali mbaya ya  uchafuzi wa hali ya hewa.

Anakumbuka hata juhudi za wazima moto na uvumilivu wa hali ya juu ya Jumuiya mbele na nguvu hizi za asili ambazo anasema zinaonesha udogo na udhaifu  wetu wa kibinadamu na kwamba ni kwamba kipo kilelezo cha mshikamano ambao ni muhimu japokuwa bado hautoshi. Kwani kuna haja ya jambo jingine kubwa zaidi ya maneno hasa katika matendo ya dhati! Vile vile Askofu Mkuu Coleridge  amesema kuwa kazi kubwa imefanya na serikali na watoa huduma ya kwanza na ni mchango mkubwa pia uliotolewa na maparokia na mashirika mengine katoliki, kama ilivyo pia muungano wa kiekumene na kidini vyote hivi ni jibu kwa ngazi za kiparokia na  kijimbo. Lakini kwa ngazi ya kipeo hiki inahitaji jibu la kitaifa kwa upande wa Kanisa zima ili kuweza kufungamanisha mpango kwa kile ambacho kinaendelea kufanyika kwa ngazi mahalia.

Kuna haja ya kuwa na mtando kitaifa wa kuunganisha watu waliopatwa na mkasa wa mto na ambao wanashuguhulikia maandalizi ya chakula, kuhamisha mali za watu, kujenga upya Jumuiya na vituo vya mapokezi ya kusikiliza mahitaji na  hata vya kichungaji. Na zaidi kuna haja ya sala maalum,  kushirikiana na wadau mbalimbali wa kitaifa na vyama vya ushirika pamoja na taasisi za kitawa , sadaka ya Misa wakati wa wiki ya mwisho ya mwezi Januari nchini Australia inayotarajiwa tarehe 26 Januari 2020 ili waweze kweli kujibu wito mkuu na maombi ya Chama cha Mtakatifu Vincenzo wa  Pauli (Vinnies), ambacho kinatenda kazi yake karibu katika maneo yote yaliyokumbwa na janga la moto.

08 January 2020, 14:09