Tafuta

Vatican News
Papa Francisko tarehe 25 Januari  amekutana na Mahakimu na Mawakili wa Mahakama ya kitume Papa Francisko tarehe 25 Januari amekutana na Mahakimu na Mawakili wa Mahakama ya kitume  (ANSA)

Papa:mfano wa Aquila na Priscilla uigwe na wanandoa wakristo!

Kanisa leo hii linahitaji wanandoa wakristo mashuhuda wa dhati wa Injili kama vile Aquila na Priscilla katika Kitabu cha Matendo ya Mitume.Ndiyo ushauri wa Papa Francisko alipokutana na mahakimu na Wawakili wa Mahakama ya Kitume Roma na kuwaalika wachungaji kutetea ndoa ya kikristo dhidi ya itikadi zinazozuka.

Wanandoa wainjilishaji, walioko katika mwendo, katikakusikiliza Roho Mtakatifu, walimu wa ukaribu na kujitoa bure, wanandoa mashuhuda  na wenye uwezo wa kuwa chachu. Ndiyo mada zilizojitokeza katika hotuba ya Papa Francisko wakati wa kufunguu mwaka wa shughuli za mahakama ya kitume mbele ya wajumbe wa Mahakama ya Kitume Roma  tarehe 25 Junauri 2020 mjini Vatican ambapo amewataja Aquila na Priscila, wanandoa wanaosomwa katika Kitabu cha Matendo ya Mitume kama mfano wa kuigwa wa utakatifu kwa wanandoa wote wakristo. Hicho ndicho kinachotakiwa kufanyika katika Parokia zetu na zaidi katika maeneo ya mijini na ambayo paroko na wahudumu wake wakati mwingine hawana hata nafasi na nguvu ya kuwafikia waamini wote  ambao licha ya kutangaza kuwa ni wakristo, inasalia kuwa na ukosefu wa kujongea sakramenti, kudharau au tuseme karibu na kutokuwa na utambuzi wa Kristo.

Ukaribu na kujitoa bure

Akwila na  Prishila, anasema  Papa, walikuwa wanainjilisha kwa kuwa walikuwa ni walimu wenye upendo mkubwa kwa ajili ya Bwana na kwa ajili ya Injili, upendo wa moyo ambao huwezi kufafanuliwa kwa maneno matupu bali kwa ishara za kweli na  pia ukaribu hasa kwa ndugu wanaohitaji zaidi, kupokea na kutunza na kujitoa bure, vitu msingi katika Mapinduzi ya Mchakato wa ndoa kwa mujibu wa Papa.  Na kwa maana hiyo Papa anauliza mahakimu waliokuwapo iwapo katika kuhukumu wamekuwa na ukaribu wa moyo na watu, ikiwa wamefungua mioyo yao ya kutoa au labda wamechukuliwa awali ya yote na matakwa ya kiuchumi na kibiashara.  Anasema Papa: “ Hukumu ya Mungu itakuwa  na nguvu dhidi ya hilo!

Msiwaache wanandoa bali kuwasikindika kama zizi na kusikiliza

Katika shughuli ya kichungaji msiache wanandoa kandoni, kwani isije kuwa ni shughuli ya kichungaji ya haraka ambayo inafanya kusahau watu, badala  yake iwe shughuli ya kichungaji inayosikiliza zizi lake  na ambao ni kuwa karibu sana na kujifunza ugha ya watu.  Wachungaji wawe na uwezo wa kusaidia watu usiku kucha na katika upweke wao, mahangaiko na kushindwa kwao: hii ndivyo Papa anawaomba  wachungaji, maaskofu, mapadri wa parokia hata kufikia mahakimu ili kupenda, kama mtume Paulo, walivyofanya, wenzi wa wa kimisionari wenye uwezo wa kufikia viwanja na majumba na miji ambayo mwangaza wa Kristo bado hauingia. Papa aidha amesema, wenzi wa Kikristo ambao wana uwezo wa kuwasha usingizi wao, kama walivyofanya Aquila na Priscilla, wenye uwezo wa kuwa mawakala, ndiyo hatujasema kwa uhuru, lakini hakika waliojaa ujasiri hadi hatua ya kuamka kutoka lepe la usingizi,  wachungaji labda waliosimama au kuzuiwa na falsafa ya mzunguko ndogo unaojifanya wa ukamilifu. Bwana alikuja kutafuta wenye dhambi, na siyo waliokamili.

Kutetea ndoa dhidi ya itikadi

Papa amewapatia wachungaji jukumu la kuangazia na kuwaelekeza wanadoa wakristokatika  kuwapa mwonekano; wa kuwafanya kuwa raia wenye uwezo mpya katika kuishi ndoa hai na kuilinda ili wasiangukie kwenye mtandao wa itikadi, ambayo inadhoofisha uthabiti wa sakramenti. Na hiyo Papa anasema: inahitaji kukesha ili wasije angukia katika hatari ya utaalam kwa kuchagua kuishi katika vikundi vilivyojichagua; Kinyume chake inahitajika kufungulia ulimwengu wa wokovu. Kwa hakika, ikiwa tunamshukuru Mungu kwa uwepo wa Kanisa, kwa ajili ya harakati na vyama na mashirika ambayo hayapuuzi malezi ya wanandoa kikristo, kwa upande mwingine lazima ikubaliwe kwamba parokia hiyo ni, mahali pa Kanisa la kutangaza na ushuhuda kwa sababu  katika muktadha huo wa eneo ambalo tayari wanando wakristo wanaishi, wanaostahili kutoa mwanga, na ambao wanaweza kuwa mashuhuda hai wa wema na upendo wa wanandoa na familia nzima.

Kurudi katika mizizi

Kuhusiana na wanandoa, Papa Francisko amesisitiza kuwa kuna haja leo hii duniani kuanzia lakini na wazo la mizizi ya kikristo, mahali ambapo Kanisa lilijifungua kila na na mamlaka ya kibinadamu, likawa maskini, likawa nyenyekevu, likawa mpole, likakandamizwa na likawa shujaa kwa kuthibitishwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, ambaye ndiye kiongozi wa kweli na injini ya uinjilishaji na ambaye ikiwa aombwi na kutajwa  bado anabaki bila kujulikana na hayupo. Papa Francisko kwa dhati anaomba kuishi katika parokia zao kama “eneo lenye nguvu” ya wokovu, nyumba kati ya nyumba nyingi, familia kati ya familia nyingi, Kanisa maskini kwa ajili ya maskini, msusuru wa wanandoa  ambao wana bidii na wanapendana na Mfufuka, kama Aquila na Priscillla, wenye uwezo wa kufanya mapinduzi mapya ya huruma na upendo, kamwe hawaridhiki na kamwe hawageuki nyuma.  “Lazima tuwe na hakika na ningependa kusema hakika, kwamba katika Kanisani wanandoa tayari ni zawadi ya Mungu na siyo sifa yetu. Hii ni kutokana na kwamba wao ni matunda ya kitendo cha Roho, ambaye hajawahi kuacha Kanisa. Badala yake, Roho anasubiri kwa hamu kwa upande wa wachungaji ili nuru waliyo nayo wanandoa hawa isije kuzimika  ndani mwao na ili iweze kuenea katika mipaka ya ulimwengu”. Papa amesema

Msijikabidhi Kanisa si la wachache

Kwa upande wa Akwila na Prishila Papa Francisko anashangazwa na ushuhuda na ambapo  anasema siyo upropagabda, bali jinsi wanavyo wavuta na kuwa kama chachu ambayo haifi namna hiyo bali inakufa wakati inaongeza ukubwa , kwa sababu Kanisa halipo na haliwezi kufanywa na wachache. Kwa njia hiyo wito wa mwisho wa papa Francisko ni kuanzia hapa:  “Wapendwa mahakimu wa kitume wa Roma , giza la imani au jangwa la imani ambalo maamuzi yenu tangu miaka ishirini ivlivyokataa kama hali inayowezekana ya kutokubaliana kubatilisha ndoa, inanipa fursa, kama ilivyokuwa tayari hata kwa mtangulizi wangu wa Papa Benedikto XVI, kutoa  mwaliko mzito ninawaalika wana wa Kanisa katika enzi tunayoishi, kuhisi wote na mtu binafsi hasa  kukabidhi uzuri wa familia ya Kikristo kwa siku zijazo”. Kanisa linahitaji wenzi wa ndoa kama Akwila na Priscilla, ambao wanazungumza na kuishi na mamlaka ya Ubatizo, ambayo si katika kuamuru na kujifanya wasikike, bali kuwa wa dhati, wenye kushikamana, kuwa mashuhuda na kwa namna hiyo kuwa wenzi katika  njia za Bwana

 

 

25 January 2020, 16:43