Tafuta

Jukwa la Uchumi duniani linafanyika jijini Davos nchini Uswiss.Papa kwa washiriki wa Mkutano huo anawaalika kuzingatia uchumi fungamani,ikiwa kitovu cha yote awe ni mwanadamu! Jukwa la Uchumi duniani linafanyika jijini Davos nchini Uswiss.Papa kwa washiriki wa Mkutano huo anawaalika kuzingatia uchumi fungamani,ikiwa kitovu cha yote awe ni mwanadamu! 

Papa kwa Jukwa la Davos:Jukwa la Uchumi duniani ni fursa za ubunifu wa kujenga dunia iwe bora!

Katika kutafuta maendeleo ya kweli tusisahau kuwa kukanyaga hadhi ya mtu mwingine maana yake ni kumshusha thamani yake.Ni wito uliomo katika ujumbe wa Papa Francisko aliomtumia Profesa Klaus Schwab Mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la Uchumi Duniani katika fursa ya Mkutano unaofanyika huko Davos nchini Uswiss kuanzia tarehe 21-24 Januari 2020.Mazungumzo yao yanaweza kuleta ukuaji katika mshikamano,hasa kwa wahitaji zaidi ambapo uwepo wao unatishiwa.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa Profesa Klaus Schwab, Mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la Uchumi Duniani katika fursa ya Mkutano   unaofanyika huko Davos nchini Uswiss kuanzia tarehe 21-24 Januari 2020. Ujumbe huo umewakilishwa  na Kardinali Peter Turkson, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la maendeleo Fungamani ya watu. Katika ujumbe huo Papa anasema, wakati Jukwaa la Uchumi Duniani linaadhimisha miaka 50 tangu kunzishwa kwake, anawatumia salama na matashi mema kwa wote ambao wanashiriki mkutano huo kwa mwaka huu. Papa Francisko anawashukuru kwa mwaliko waliompatia, ambapo kwa niaba yake amemtuma mwakilishi Kardinali Peter Turkson, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la maendeleo Fungamani ya watu. Katika miaka hii Papa amesema , Jukwa la Uchumi duniani limeweza kutoa fursa kwa ajili ya jitihada tofauti na muhimu katika tafiti  mbalimbali za ubunifu na muafaka katika kujenga dunia ili bora.

Jukwaa la kiuchumi linaweza kushinda tabia ya upweke, ubinafsi na mawazo ya kikoloni

Aidha Jukwa hili limeweza kusaidia kwa mantiki ambao wanaweza kuongozwa na kukuza utashi wa kisiasa na kuendeleza ushirikiano katika kushinda tabia za upweke, ubinafsi na mawazo ya ukoloni ambayo kwa bahati mbaya ndiyo tabia ya mijadala mingi ya sasa. Na katika mwanga wa changamoto zinazokua, daima zinasukana na ambazo ni lazima kukabiliana nazo katika dunia (rej Laudato si’, n. 138 na kuendelea.), mada ambayo wamechagua kuwaongoza mwaka huu isemayo “Stakeholders for a Cohesive and Sustainable World” yaani  ‘Wadau wa kushikamana na Ulimwengu Endelevu” inaelekeza ulazima wa kufanya jitihada kwa ngazi ya wote na hatimaye kuweza kukabiliana kwa namna hai katika masuala ambayo yanakabiliwa na ubinadamu.

Miaka 50 ya mwisho imeleta mabadiliko ya masoko ya kazi na teknolojia ya kidigitali

Katika mchakato wa miaka 50 ya mwisho, Papa anabainisha kuwa imeonekana mabadiliko mengi kisiasa na mabadiliko  yenye maana, kuanzia uchumi na kufikia masoko ya kazi, katika teknolojia ya kidigitali na mazingira. Maendeleo yaliyo mengi yameweza kuleta faida kwa binadamu, wakati mengine yamekuwa hasi na kuleta baadhi ya kasoro za maendeleo. Hata kama changamoto za sasa siyo kama zile za karne moja iliyopita, lakini mambo kadhaa yanaendelea kuwa muhimu tunapoanza muongo huu mpya. Jambo muhimu ambalo tunapaswa kuzingatia na  bila kusahau kamwe ni kwamba sisi sote ni washiriki wa familia moja ya wanadamu, Papa amesisitiza. Wajibu wa kimaadili wa kusaidiana mmoja na mwingine unatokana na jambo hili kwa hakika kama sawa na kanuni inayohusiana ya kumweka mwanadamu katika kituvu,  badala ya kutafuta tu nguvu au faida katika moyo wa sera ya umma.

 Maono ya matumizi ya kawaida au ya matumizi ya nguvu

Uwajibu huu zaidi unagusa katika sekta za kibiashara iwe kwa mataifa na ndiyo  muhimu katika kutafuta suluhisho sahihi kwa changamoto zinazotukabili. Kwa maana hiyo ni lazima kwenda zaidi ya katika mantiki za kiteknolojia au kiuchumi, kwa kifupi na kuzingatia ukuu wake kimaadili katika kutafuta suluhisho za matatizo ya sasa au kupendekeza mambo mengine ya kufanya kwa ajili ya wakati ujao. Maono ya matumizi ya kawaida au ya matumizi ya nguvu, wakati mwingine yaliyofichwa, nyakati zingine yameoneshwa, husababisha mazoea na miundo iliyohamasishwa kwa kiasi kikubwa, au hata tu, kwa maslahi yao wenyewe. Kwa kawaida hawa uona wengine kama zana za kufikia lengo lao na kusababisha ukosefu wa mshikamano na hisani na kwa sababu hiyo ufanya kuzaliwa ukosefu wa haki ya kweli na wakati maendeleo ya kweli ya  mwanadamu na fungamani yanaweza kufikia tu iwapo wajumbe wa familia moja ya kibinadamu wanaungana kwa ajili ya kutafuta ustawi wa pamoja na wanaweza kutoa mchango wao. Katika kutafuta maendeleo ya kweli tusisahau kuwa kukanyaga hadhi ya mtu mwingine maana yake ni kumshusha thamani yake.

Umuhimu wa ‘Ekolojia fungamani’ ambayo inazingatia athari zote za ugumu

Papa Francisko akijikita kutazama Wosia wake wa Laudato si, anawakumbusha kuwa, alitaka uwepo makini juu ya umuhimu wa ‘Ekolojia fungamani’ ambayo inazingatia athari zote za ugumu na muunganisho wa nyumba yetu ya pamoja. Njia hii ya ubunifu kimaadili, na fungamani inahitaji ubinadamu ambao unatoa wito juu ya taaluma tofauti hata ile ya uchumi kwa ajili ya maono zaidi kamili na fungamani ( Reh Laudato sì 141). Katika kujua matukio ya miaka 50 ya mwisho, ni matashi yake Papa Francisko kwamba, washiriki wa Jukwa la sasa na yale yatakayofuatia, wakati ujao wanaweza kuzingatia uwajibikaji mkuu wa kimaadili mbao kila mmoja wetu anawajibika kutafuta maendeleo fungamani ya kaka na dada wote, ikiwemo hata kizazi endelevu. Mazungumzo yao yanaweze kuleta ukuaji katika mshikamano, hasa kwa wahitaji zaidi, ambao wanapata dhuluma ya kijamii na kiuchumi na ambapo hata  uwepo wao unatishiwa.  Na kwa wote wanao shiriki Jukwaa hilo amerudia kuwatakia kila la heri ya Mkutano huo na uweze kuzaa matunda na kuwabariki kwa Baraka ya Mungu.

21 January 2020, 11:34