Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa wawakilishi wa Kongamano la Elimu katoliki Barani Amerika ya Kusini Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa wawakilishi wa Kongamano la Elimu katoliki Barani Amerika ya Kusini 

Papa hamasisheni utamaduni wa makutano barani Amerika Kusini!

Papa Francisko ametoa wito wa kuhamasisha utamaduni wa makutano katika Ujumbe wake aliutumowa kwa washiriki wa Kongamano la Elimu Katoliki Barani Amerika ya Kusini.Ujumbe wake umetiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.Kongamano lilifunguliwa tarehe 8 Januari na litamalizika tarehe 12 Januri 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Uongozi, mawasiliano na soko, ndizo mada msingi zinazoongoza Kongamano la 26 la Elimu Katoliki barani Amerika ya Kusini linaloendelea hadi tarehe 12 Januari 2020 na linafanyika huko Santiago ya Chile. Katika Ujumbe wa Papa Francisko uliotiwa sahini na Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican, Papa Francisko anawatia moyo wahusika wote wa shule katoliki ili kutafakari kwa kina juu ya changamoto za kukabiliana nazo na kuhamasisha katika mantiki ya mada waayojikta nayo katika utamaduni wa dhati wa makutano na hatimaye ili kuweza kufikia kuwa na mapendekezo ya dhati ya matumaini na imani ya wakati ujao.

Misa ya ufunguzi:wafuasi wa bwana tunahitaji elimu

Kongamano hili limeandaliwa na Shirikisho la Elimu Katoliki la Amerika ya Kusini ambalo limefunguliwa tarehe 8 kwa Ibada Takatifu ya Misa iliyoongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu  nchini Chile Askofu Santiago Silva Retamales. Katika mahubiri yake amesema kiini ni Yesu. “Sisi ni wafuasi wa Bwana ambao tunahitaji elimu na siyo kutaka itikadi ya mawazo yoyote yale, siyo maadili au dogma yoyote ile bali na Mtu ambaye tunahitaji kukutana Naye”. Na zaidi ameongeza Askofu  Santiago Silva Retamales “tunapaswa kujikita kwa undani juu ya mada za Kongamano hili la Injili.

Changamoto mpya

Naye Askofu Óscar Pérez Sayago, Katibu mkuu wa Kongamo la Elimu Katoliki la Amerika ya Kusini ambaye ni wa Jimbo la Mtakatifu José wa Temuco, wakati wa hotuba yake amekumbusha kuwa utume wa kimisionari katika kiungo hicho ni kutia moyo katika uinjilishaji wa watu wa Amerika kwa njia ya elimu. “Ni kipindi sasa cha kuwa na maana ya mitazamo mipya, ya changamoto mpya, ya kizazi kipya katika nchi ambazo sisi tunaishi”.  Aidha ameongeza kusisitiza kuwa lazima kuhamasisha uwepo wa uongozi mpya katoliki katika nyanja mbalimbali za maisha ya binadamu. Na kwa njia hiyo ameongeza ni lazima kuwa na mitindo mipya inayoruhusu kubadilishana wema daima iwezekanavyo na kuweza kuendeleza utambulisho wa ukristo kijamii.

11 January 2020, 11:39