Tafuta

Vatican News
Tarehe 25 Januari 2020 jioni Papa Francisko ameongoza masifu ya sala wakati wa siku ya ongofu wa Mtakatifu Paulo Mtume wa watu ikiwa pia ni kufunga wiki ya maombi kwa ajili ya umoja wa wakristo Tarehe 25 Januari 2020 jioni Papa Francisko ameongoza masifu ya sala wakati wa siku ya ongofu wa Mtakatifu Paulo Mtume wa watu ikiwa pia ni kufunga wiki ya maombi kwa ajili ya umoja wa wakristo  (ANSA)

Papa Francisko:tudumishe ukarimu ni utamaduni wa kikristo!

Papa Francisko wakati wa kuhitimisha Wiki ya 53 ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo ameshauri kuendeleza ukarimu kwani ni utamaduni wa kikristo na kujifungulia wema.Hatupaswi kuvutiwa na mantiki za kiulimwengu bali kujikitia katika usikivu wa wadhaifu na maskini ambao Mungu anapenda kutuma ujumbe wake kwa njia yao na anataka watu wote waweze kuokoka.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika meli iliyokuwa inampeleka Paulo gerezani huko Roma  kulikuwapo na makundi matatu tofauti. Katika makundi hayo lililokuwa na nguvu lilikuwa ni maaskari chini ya mkuu wa jeshi hilo. Kuna manaodha ambao kwa asili ndiyo walioongoza meli na kutegemewa wao katika safari yao ndefu. Na mwisho walikuwapo wadhaifu na wanyonge yaani wafungwa. Ndiyo Mwanzo wa Tafakari ya Papa Francisko wakati wa Masifu kwenye Sikukuu ya Uongofu wa Mtakatifu Paulo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo nje ya Roma, sambamba na kuhitimisha Wiki ya 53 ya Kuombea Umoja wa Wakristo, wiki iliyoanza tarehe 18 -25 Januari 2020. Papa Francisko anasema: Meli ilipofika katika pwani za Malta, baada ya kukaa kwa siku nyingi na matatizo ya dhoruba, maaskari walifikiria kuwaua wafungwa kwa uhakika kuwa asije toroka hata mmoja, lakini wakakatazwa na Akida ambaye anataka kumwokoa Paulo. Kwa hakika licha ya kuwa kati ya wanyonge zaidi, Paulo alikuwa amepata jambo moja muhimu katika safari. Wakati hawa walikuwa wamepoteza kila tumaini la kuishi, Mtu alikuwa anaweza kutoa ujumbe wa matumaini usiotarajiwa. Na hii ni kutokana na kwamba Malaika alikuwa amemwakikishia kuwa “Usiogope Paulo: Mungu ametaka kuwafadhili na kuwaokoa wote unaosafiri nawe (Mdo 27,24)”.

Imani ya Paulo na miujiza 

Imani ya Paulo inajionesha kuwa thabiti na hatimaye wasafiri wote wanaokoka na mara baada ya kutua Malta, wanafanya uzoefu wa kukaribishwa na wakazi wa kisiwa, kwa ukarimu wao na ubinadamu. Kutoka hapo ndiyo kuna umuhimu kwa namna ya pekee kauli mbiu iliyoongoza Wiki ya maombi ambayo inahitimishwa. Safari inayosimuliwa katika Matendo ya mitume inazungumza hata safari yetu ya kiekumene, moja kwa moja katika muungano ambao Mungu anapenda kwa shauku kubwa. Awali ya yote inatazama wale walio wadhaifu na wanyonge, wale wasio kuwa na zana za kutoa zaidi, lakini ni thabiti katika Mungu kwa utajiri binafsi ambao wanaweza kutoa ujumbe wenye thamani kwa ajili ya wema wa wote.

Mungu anapenda kuokoa ulimwengu kwa njia ya udhaifu wa msalaba

Papa Francisko amefikiria Jumuiya za kikristo na hata zile ambazo ni ndogo na hazionekani katika macho ya dunia, ikiwa wanafanya uzoefu wa Roho Mtakatifu, ikiwa wanaishi upendo wa Mungu na wajirani, wanao ujumbe wa kutoa kwa familia nzima ya kikristo. Papa anawaalika wafikirie Jumuiya za Kiristo ambazo zimesahulika na kuteswa. Kama simulizi ya manusura ya Paulo, mara nyingi ni wadhaifu wanaobeba ujumbe wa wokovu muhimu zaidi. Na hivi ndivyo Mungu anapenda kuokoa, si kwa nguvu za ulimwengu, bali kwa njia ya udhaifu wa msalaba (1Kor 1,20-25). Kama wafuasi wa Yesu, Papa anasema ni lazima kuwa makini ili tusivutiwe na mantiki za kidunia, badala yake ni kujikita katika usikivu kwa walio wadhaifu, na maskini, kwa maana Mungu anapenda kuwatumia wajumbe wake kwa njia yao na kujifananisha zaidi na mwanaye akijifanya binadamu.

Mantiki ya pili ni ile ya  upendo wa Mungu kwa kuwakoa wote

Simulizi ya Matendo ya Mitume intukumbusha mantiki ya pili hasa ya upendeleo wa Mungu ni wokovu kwa wote.  Kama alivyosema Malaika kwa Paulo kuwa “ Mungu anataka kuwawafadhil wenzake wote  anaosafiri nao, na ni sehemu ambayo Paulo anasisitiza. Hata sisi tunahitaji kurudia  kusema kuwa “ni wajibu wetu wa sasa wa kuweka ushauri wa kwanza kwa Mungu kama anavyoandika Paulo mwenyewe “ ambaye anataka watu wote waokolewe(1Tm 2,4). Ni mwaliko wa kujikita kwa nguvu zote katika jumuiya zetu anasisitiza Papa, lakini kwa kujifungulia wema kwa wote katika mtazamo wa Mungu duniani kote, ambaye alijifanya mwili ili kukumbatia familia nzima ya binadamu na akafa na kufufuka kwa ajili ya wokovu wa wote. Ikiwa kwa njia ya neema yake tunafanana na maono yake, tunaweza kushinda migawanyiko yetu. Manusura wa Paulo, kila mmoja aliweza kuchangia wokovu wa wote, kwani akida alitoa uamuzi muhimu, mabaharia waliweka matunda yao ya taaluma na uwezo na  Mtume anakawatia moyo kwa wale ambao hawakuwa na matumaini. Hata kati ya wakristo kila jumuiya ina zawadi ya kutoa kwa wengine. Tukiweka matakwa yetu mbali zaidi na kushinda zile mantiki za kizamani na ili  kutazama yale yanayo tuunganisha, itajitokeza ile hali ya kawaida ya kutambua, kukaribisha na kushirikishana zawadi hizo, amebainisha Papa Francisko.

Mantiki ya tatu na kiini cha Wiki ya kuombea umoja wa Wakristo ni ‘Ukarimu’

Mantiki ya tatu ambayo imekuwa kiini cha Wiki ya Maombi ni Ukarimu. Papa Francisko amesema, Mtakatifu Luka katika sura ya mwisho wa Matendo ya Mitume anasema wakazi wa Malta, “ walitufadhili kwa ukarimu au tuseme “ubinadamu adimu”. Moto uliokuwa umewashwa kwa ajili ya kuwapasha joto manusura ni ishara nzuri sana ya joto la kibinadamu lilolowazunguka bila kutegemea. Hata Mkuu wa Kisiwa hicho alijionesha mkarimu kwa Paulo na ambaye baadaye alioneshwa shukrani kwa kumtibu baba yake na baadaye watu wengi wagonjwa(7-9). Mwisho wakati Mtume na wenzake waliondoka kuja Italia, Watu wa Malta waliweza kuwaandalia vitu vingi vya kula kuwasaidia njiani.

Katika wiki hii tujifunze ukarimu, kwetu sisi wakristo  na kwa madhehebu mengine

Katika Wiki hii ya Maombi Papa Francisko amesema tunataka tujifunza kuwa wakarimu, awali ya yote kati yetu wakristo na hata wale ndugu wa madhehebu mengine. Ukarimu unaanzia katika tamaduni za Jumuiya  na familia za kikristo. Wazee wetu, Papa amesema walitufundisha mifano kuwa: “katika meza ya nyumba ya mkristo daima kuna sahani ya chakula kwa ajili ya rafiki anayepita au mwenye kuhitaji anapobisha mlango”. Katika monasteri, ukarimu unazingatiwa kwa umakini zaidi. Tusipoteze utumaduni huo badala yake ni kuishi huo utamaduni ambao ni wa Injili amehimiza Papa.  Na hatimaye Papa amewageukia kuwasalimia ndugu kuanzia na Kiongozi Mkuu wa kiorthodox, mwakilishi wa Upatriaki wa Kiekumene, Grazia Ian Ernest, Mwakilishi wa Roma wa Askofu Mkuu wa  Canterbury, na wawakilishi wa makanisa yote na Jumuiya za Kikanisa zilizofika mahali hapo. Amewakumbuka pia wanafunzi wa Taasisi ya Kiekumene ya Bossey, wakiwa katika hija ya kutafakari na utambuzi wa Kanisa Katoliki; vijana wa Kiorthodox kutoka Nchi za Mashariki wanaosoma kwa ufadhili wa Mfuko wa Tume kwa ushirikiano wa Utumaduni wa makanisa ya Kiorothodox; Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo na ambao anawasalimia na kuwashukuru. Na kwa pamoja bila kuchoka Papa amehimiza kuendelea kusali na kumwomba Mungu zawadi  umoja kamili kati yetu.

26 January 2020, 09:50